Kitendo cha IGP Sirro kutoa hukumu ya Ugaidi wa Mbowe huku kesi ikiwa Mahakamani ni Uhalifu. Napendekeza kesi hiyo ifutwe haraka

Kitendo cha IGP Sirro kutoa hukumu ya Ugaidi wa Mbowe huku kesi ikiwa Mahakamani ni Uhalifu. Napendekeza kesi hiyo ifutwe haraka

HIVI NYIE WATU mnaelewa mashtaka aliyoshtakiwa nayo mbowe? siyo ya katiba ni ya ugaidi aliokuwa anafanya sasa nyie mnalazimisha ni ya katiba
Wewe ndio wajitoa fahamu na kujifanya huelewi. Hamkuanza leo na mnapokaribia mwisho wenu, mtashindana na kukimbizana sana kuokoteza mashitaka. Katiba mpya haikwepeki.
 
Wote bila shaka mmemsikia Mkuu wa jeshi la Polisi wa Tanzania Mtukufu IGP Simon Sirro , kauli yake hii ni sawa na kulazimisha mahakama kutenda ayanenayo.

Sirro anafahamu kwamba Sheria inakataza yaliyo Mahakamani kujadiliwa vijiweni , na hasa kama anayejadili ana maslahi kwenye kesi iliyo mahakamani , kama yeye Sirro alivyo na maslahi binafsi kwenye kesi hii , lakini ameamua kupuuza ili kumrahisishia maamuzi hakimu wao wanayemtumia kumkomoa Mbowe na Chadema.

Sirro anapaswa kuleta ushahidi wake Mahakamani , badala ya kupiga filimbi mitaani , OMARI MAHITA alikuwa IGP Ambaye rekodi yake ya ukatili haijavunjwa hadi leo , lakini baada ya kustaafu ALISHITAKIWA MAHAKAMANI KWA KESI YA KUMBAKA HOUSE GIRL WAKE MWENYEWE, NA KUMPACHIKA MIMBA KISHA KURUKA MATUNZO YA MTOTO , wala ccm aliyoipigania haikumuokoa kwenye aibu ile , nani aliyesahau jambo hili ? Sirro ajifunze kutenda haki ili asije kudhalilika huko mbele, Cheo ni dhamana ya muda mfupi tu .

Pamoja na Omari Mahita kujenga msikiti Morogoro lakini watukufu waislam wamekataa kuutumia ili kuogopa kunajisi udhu wao kwa kuswali kwenye msikiti wa katili aliyeiona ccm ni bora kuliko Allah Subhhannah.

Mwisho napendekeza kesi ya Mbowe ifutiliwe mbali kwa maana ni ya uongo , na IGP Sirro atimuliwe kazi kabla jua halijazama.

Mama Samia hana IGP hapo. Ni takataka tupu. Kesi aliyoifungua mwenyewe ameishaiharibu. Jaji anapaswa kuifuta kesi hiyo kwa mstaki kukiuka sheria na kuisemea mtaani huku akijua fika kuwa ni makosa kisheria kwani yeye pia (jeshi la polisi) ni shahidi muhimu. Duh, polisi hakuna tena intelijensia!!!!!!!!
 
Unajitekenya halafu unalazisha ucheke mwenyewe sasa kesi ya mahita inakujaje sasa hivi mbona hujaizungumzia kesi ya lema naye ana kesi ya kubaka pia yaani jeuri yenu imekwisha sirro kasema mumuulize mshitakiwa mambo hayo aliyouliza awajibu unakuja kuharisha hapa ooo mahita alibaka hivi huja maliza kusaini yale makaratasi ya kumtoa mbowe? bado anayea ndoo mwenzio kamsaidie
Sasa na ww umeandika nn mbona muharo tu kwahiyo unasapot igp kuingilia au kuvuruga ushahidi Kwa maana hiyo akisema kuwa anaushahidi kuwa mbowe ni gaidi niwazi kuwa tayari hukumu yake wanayo mikononi sio sasa hapo nafasi ya mahakama na polisi na mtuhumiwa iko wapi
 
Ile dua iliyofanyika tarehe 27/10/2020 bado iko valid, yaani maombi tunayofanya sasa ni kama tunai refresh tu,hadi kufika 2025 tutakuwa tumewazika watesi wetu wengi sana ili iwe fundisho. Waache wademke tu kwa furaha ya muda mfupi.
 
Pole Ndugu,
Yaonekana dhahiri kuwa umepungukiwa uwezo wa kuelewa hoja iliyopo, matokeo yake washindwa kabisa kujibu wala kujenga hoja imara.
Sijui wanao watakuja kuwa wa sampuli gani.
Ee Mungu twakuomba uwaepushe na kurithi balaa hiyo.
Siyo watakuja, wanangu wapo na wana akili na IQ kubwa kushinda mlevi Mbowe aliyeanguka kwenye ngazi zake mwenyewe na kusingizia serikali.
 
Nyerere angekuwa na mawazo ya kindezi kama yako nchi hii isingepata uhuru milele
Umezidi!! Mbowe, Mbowe, mbowe! Utadhani uko ktk mchaka-mchaka. CHADEMA hakuna wengine unaoona wanastahili kuzungumziwa, ni Mbowe tu!! Mbowe mwanza, mbowe, shinyanga, mbowe arusha, mbowe mahabusu. Ukaishiwa sijui uliachwa Mwanza? Sasa umeanza, Mbowe Mahabusu, mbowe anaonewa, mbowe bhla! Bhla! Hata Sabaya umemsahau. Do reasoning!! CHADEMA is more than Mbowe!
 
Umezidi!! Mbowe, Mbowe, mbowe! Utadhani uko ktk mchaka-mchaka. CHADEMA hakuna wengine unaoona wanastahili kuzungumziwa, ni Mbowe tu!! Mbowe mwanza, mbowe, shinyanga, mbowe arusha, mbowe mahabusu. Ukaishiwa sijui uliachwa Mwanza? Sasa umeanza, Mbowe Mahabusu, mbowe anaonewa, mbowe bhla! Bhla! Hata Sabaya umemsahau. Do reasoning!! CHADEMA is more than Mbowe!
😆😆😆 Usichokijua ni hiki , Mbowe ndiye mtoa dira wa nchi hii

Pole sana kwa maumivu kijana
 
Bando langu
Simu yangu,
Halafu unipangia cha kuandika!!
Kama unaumia acheni ugaidi.
Hata tukiumia huwezi jua na Wala kuumia na sisi. Mateso haya tunayapokea kwa hiari ambayo inatupa matumaini kwamba hatuna budi kukinywea kikombe ili kuifikia nchi ya ahadi.
Nyie mnaotutesa mnateseka zaidi katika nafsi zenu na mbaya zaidi hamna amani Wala matumaini ya siku zijazo badala yake mmejawa na hofu.
Sie we are already dead so nothing will stop us.
 
Kama inavyo semekana Mbowe alikuwa anaajiri/recruits askari na wanajeshi waasi kwa lengo la kuhujumu serikali na kuuwa viongozi wa serikali, basi kwakweli Mbowe alifika pabaya sana, siajabu ange ajiri hata wahamiaji haramu kwa lengo baya zaidi.
Matendo haya hayana tofauti na yale wanayo yafanya Bokoharam.
hata hivyo Jeshi la Polisi wakishirikiana na vyombo vyote vifanye upelelezi wa kina na kwa weledi wa viwango vya juu.
 
Kuunda njama na vijana wa waliofukuzwa jeshini nayo ni madai ya katiba sio?
Kwahiyo unataka kusema like tukio mlitengeza ....sasa kumbuka hao vijana wameisha kana ilo tukio ata kama wamekua tortured kivile.
 
Back
Top Bottom