Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
angeanza kusema na kiongozi wake wa Mhimili sio kusambaza mabarua kila kona!!!Mahakama ni muhimili ,katika ule utatu wa Kuunda taifa kikatiba
Anapaswa kusema yanayohusu muhimili wake ukiingiliwa na mwingine.
Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
Aseme naye kitu gani???angeanza kusema na kiongozi wake wa Mhimili sio kusambaza mabarua kila kona!!!
kwani Yeye Jaji Mugasha yupo chini ya Rais au Jaji Mkuu?Asrme naye kitu gani???
Kwani huyu Jaji Mkuu alijiteua yeye mwenyewe ktk hiyo nafasi ya Ujaji Mkuu????
Jaji Mkuu Prof Ibrahim Juma alipaswa amtahadharishe Rais kuwa kuongeza muda kwa Jaji aliyehudumu hadi 65 years ni violation of constitution by appointing authoritykwani Yeye Jaji Mugasha yupo chini ya Rais au Jaji Mkuu?
je huoni Jaji Mugasha alitakiwa kwanza ashauriani na Kiongozi wake ambaye ni Jaji Mkuu kisha Jaji Mkuu ndipo aishauri mamlaka ya juu?
Huna,akiliKitendo cha Jaji wa Mahakama ya Rufaa cha kuandika barua na kuzisambaza kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kuhusu au Kukosoa Kitendo cha Rais kumuongezea Jaji Mkuu muda wa kuendelea kuwepo kwenye kiti ni kitendo cha ukosefu wa nidhamu kwa mamlaka zilizo juu yake.
Kutoa maoni ni haki ya kila raia lakini inategemea maoni unyatoa wapi na kwa njia gani, Jaji Mugasha alipaswa aishauri mamlaka kwa njia sahihi sio hii aliyo itumia.
tunafahamu kuwa Jaji Stela Mugasha ni Jaji wa Mahakama ya Rufaa hivyo kwa nafasi yake ni kiongozi mkubwa tu ambaye yupo karibu na viongozi wa juu sasa kwa nini aliamua kuandika mabarua na kusambaza?!
kwahiyo lengo lake lilikuwa sio kujenga bali itatafsiriwa kuwa alilenga kubomoa na kudhalilisha mamlaka.
Jaji Stella Mugasha alikuwa nayo nafasi ya kumshauri hata Prof. Jaji Mkuu aliyepo kabla ya kusambaza mabarua yake.
Je? kulikuwa na haja ya kuandika baru kwa Mhe. Rais na kisha kutoa nakala kila ofisi ambazo zipo chini ya Rais?! Mugasha alikuwa na lengo gani?
wakati mwengine ukijifanya mjuaji sana unakuwa na Kiburi na dharau.
mimi ni mwananchi Mkulima, sijui sheria ila nimesema kitendo cha Jaji Mugasha kuandika Barua kwa Rais kisha kuinakilisha ktk ofisi za chini ya Rais na kusambaza kwenye vyombo na mitandao je? huo sio utovu wa nidhamu?
Je, kulikuwa na haja ya sisi wananchi kujua mawasiliano yao ya kiofisi?
Pia soma: Profesa Ibrahim Juma kuendelea kuwa Jaji Mkuu, Rais Samia anavunja Katiba ya JMT?
Fanya kwanza utafiti wa kina kuhusu suala hili, inavyoonekana wewe umekurupuka na kuja kuchangia hapa jukwaani jambo ambalo huna ufahamu nalo wa kutosha.kwani Yeye Jaji Mugasha yupo chini ya Rais au Jaji Mkuu?
je huoni Jaji Mugasha alitakiwa kwanza ashauriani na Kiongozi wake ambaye ni Jaji Mkuu kisha Jaji Mkuu ndipo aishauri mamlaka ya juu?
AG alishaishauri Ofisi ya Rais kuhusu Jambo hili, rejea barua ya AG ambayo Jaji Mugasha ameinukuu kwenye barua yake. Aidha, Jaji Mkuu kazi yake siyo kumshauri Rais kuhusu masuala ya Sheria, hiyo ni kazi ya AG.Jaji Mkuu Prof Ibrahim Juma alipaswa amtahadharishe Rais kuwa kuongeza muda kwa Jaji aliyehudumu hadi 65 years ni violation of constitution by appointing authority
Uko sahihi, kwamba, Mwanasheria Mkuu ndiye mshauri Mkuu wa Rais kwenye masuala ya kisheria.Fanya kwanza utafiti wa kina kuhusu suala hili, inavyoonekana wewe umekurupuka na kuja kuchangia hapa jukwaani jambo ambalo huna ufahamu nalo wa kutosha.
Upo utaratibu wa uteuzi wa majaji pamoja na Jaji mkuu ambao umeainishwa kwenye Katiba ya nchi pamoja na Sheria zingine za nchi. Jaji huyu wa Rufani alichofanya ni sahihi kabisa, tena amezingatia Katiba ya nchi, Sheria zote za nchi, Kanuni na Miongozo yote ya nchi hii. Tena inavyoonekana huyu Jaji Mugasha ni KICHWA(AKILI KUBWA).
Aidha, Jaji Mugasha yupo chini ya Mtendaji Mkuu wa Mahakama, hata Jaji Mkuu naye yupo chini ya Mtendaji Mkuu wa Mahakama.
Kwa nini wewe unafikiri kwamba Jaji Mugasha alipaswa kushauriana na Jaji Mkuu kwanza (aliyeteuliwa kwa njia haramu) kabla ya kumwandikia barua Rais???
Aidha, nakukumbusha kwamba Mshauri Mkuu wa Rais wa nchi na Serikali yake yote kuhusu masuala yote ya kisheria ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), wala siyo Jaji Mkuu. Vile vile, nakukumbusha pia kwamba Jaji Mugasha hayupo chini ya Muhimili wa dola uitwao Serikali(Executive), Majaji wote wapo chini ya muhimili wa Mahakama, ambao kazi yake kuu ni KUTAFSIRI SHERIA, kazi ambayo Jaji Mugasha ameifanya kwa uadilifu mkubwa kwa kumtafsiria Sheria Rais wa nchi kuhusiana na taratibu za kumteua Jaji Mkuu.
Alichofanya Jaji Mugasha ni kumkumbusha Rais wa nchi kwamba "kitu alichofanya ni kinyume kabisa na matakwa ya Katiba ya nchi ambayo Rais mwenyewe kwa kinywa chake aliapa kuitetea na kuilinda".Uko sahihi, kwamba, Mwanasheria Mkuu ndiye mshauri Mkuu wa Rais kwenye masuala ya kisheria.
sasa Jaji Mugasha naye amekuwa mshauri wa masuala ya kisheria kwa Rais?
lakini hoja yangu ya msingi ilikuwa ni; kama Jaji Mungasha alipaswa kuandika barua kwa Rais na kuinakilisha kila ofisi na kuisambaza kwa vyombo vya habari na mitandaoni.
alikuwa na lengo gani kufanya hivyo?!!
Abayango
Sasa atatoaje ushauri na maamuzi yashafanyika?Mamlaka yoyote ya kibanaadamu inapaswa kukoselewa ila mimi nimeuliza namna au njia aliyo tumia Jaji Mugasha kukosoa kwa kuandika barua na kunakilisha na kisha kuzisambaza kwenye vyombo mbalimbali je huo sio utovu wa maadili?
Kumbuka Jaji Mugasha ni kiongozi pia, na anaweza kumshauri hata Jaji Mkuu aliye ongezewa muda kwanini hajatumia nafasi hiyo?
Barua ni ya kwake hakuna tatizo.yeye ndiye mwandishi na mmiliki wa barua aliyo iandika, unadhani nani mwengine aliye isambaza barua hiyo? hawezi kukwepa labda akanushe kuwa sio baru yake.