Kitendo cha Jaji Mugasha kukosoa mamlaka hadharani ni utovu wa nidhamu, sio ushujaa

Aliyeapa kuitetea na kuilinda katiba ya JMT kisha kiuvunja kwa maslahi binafsi ndiye amekosa adabu na kitendo hicho ni tusi kwa watanzania wote.
 
Mahakama ni muhimili ,katika ule utatu wa Kuunda taifa kikatiba
Anapaswa kusema yanayohusu muhimili wake ukiingiliwa na mwingine.

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
 
angeanza kusema na kiongozi wake wa Mhimili sio kusambaza mabarua kila kona!!!
Aseme naye kitu gani???
Kwani huyu Jaji Mkuu alijiteua yeye mwenyewe ktk hiyo nafasi ya Ujaji Mkuu????
Aliyefanya kosa la uteuzi haramu wa Jaji Mkuu ni Rais wa nchi, na huyu Jaji wa Rufani amemlima barua huyo mkosaji(Rais), tatizo la huyo Jaji wa Rufani liko wapi??
She has done the right thing.
 
Asrme naye kitu gani???
Kwani huyu Jaji Mkuu alijiteua yeye mwenyewe ktk hiyo nafasi ya Ujaji Mkuu????
kwani Yeye Jaji Mugasha yupo chini ya Rais au Jaji Mkuu?
je huoni Jaji Mugasha alitakiwa kwanza ashauriani na Kiongozi wake ambaye ni Jaji Mkuu kisha Jaji Mkuu ndipo aishauri mamlaka ya juu?
 
Wabobevu wa sheria wanasema Rais hajavunja Katiba kwa kumuongezea Muda Jaji Mkuu.

kwahiyo Jaji Mugasha kakurupuka na kupotosha wananchi.

wakili Mgongolwa atoa ufafanuzi wa kisheria.

 
kwani Yeye Jaji Mugasha yupo chini ya Rais au Jaji Mkuu?
je huoni Jaji Mugasha alitakiwa kwanza ashauriani na Kiongozi wake ambaye ni Jaji Mkuu kisha Jaji Mkuu ndipo aishauri mamlaka ya juu?
Jaji Mkuu Prof Ibrahim Juma alipaswa amtahadharishe Rais kuwa kuongeza muda kwa Jaji aliyehudumu hadi 65 years ni violation of constitution by appointing authority
 
Wewe mleta mada ndiyo huna nidhamu na hujiamini maana unashindwa kusimamia unachoamini kwa sababu za uoga na unafiki ili upate kula.
 
Yuko sahihi ila ingekuwa na maana zaidi kama angeshauri na maeneo mengine zaidi yenye changamoto, ila ile kujikita kutoa ushauri katika tasnia yake kunaweza kuleta tafsiri ya kuwa alikuwa anakitaka hicho cheo.
 
Huna,akili
 
Unajuaje kama hajatumwa na Rais ili amwondoe AG? Washauri wa Rais ni mbumbumbu.
 
kwani Yeye Jaji Mugasha yupo chini ya Rais au Jaji Mkuu?
je huoni Jaji Mugasha alitakiwa kwanza ashauriani na Kiongozi wake ambaye ni Jaji Mkuu kisha Jaji Mkuu ndipo aishauri mamlaka ya juu?
Fanya kwanza utafiti wa kina kuhusu suala hili, inavyoonekana wewe umekurupuka na kuja kuchangia hapa jukwaani jambo ambalo huna ufahamu nalo wa kutosha.

Upo utaratibu wa uteuzi wa majaji pamoja na Jaji mkuu ambao umeainishwa kwenye Katiba ya nchi pamoja na Sheria zingine za nchi. Jaji huyu wa Rufani alichofanya ni sahihi kabisa, tena amezingatia Katiba ya nchi, Sheria zote za nchi, Kanuni na Miongozo yote ya nchi hii. Tena inavyoonekana huyu Jaji Mugasha ni KICHWA(AKILI KUBWA).
Aidha, Jaji Mugasha yupo chini ya Mtendaji Mkuu wa Mahakama, hata Jaji Mkuu naye yupo chini ya Mtendaji Mkuu wa Mahakama.
Kwa nini wewe unafikiri kwamba Jaji Mugasha alipaswa kushauriana na Jaji Mkuu kwanza (aliyeteuliwa kwa njia haramu) kabla ya kumwandikia barua Rais???
Aidha, nakukumbusha kwamba Mshauri Mkuu wa Rais wa nchi na Serikali yake yote kuhusu masuala yote ya kisheria ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), wala siyo Jaji Mkuu. Vile vile, nakukumbusha pia kwamba Jaji Mugasha hayupo chini ya Muhimili wa dola uitwao Serikali(Executive), Majaji wote wapo chini ya muhimili wa Mahakama, ambao kazi yake kuu ni KUTAFSIRI SHERIA, kazi ambayo Jaji Mugasha ameifanya kwa uadilifu mkubwa kwa kumtafsiria Sheria Rais wa nchi kuhusiana na taratibu za kumteua Jaji Mkuu.
 
Jaji Mkuu Prof Ibrahim Juma alipaswa amtahadharishe Rais kuwa kuongeza muda kwa Jaji aliyehudumu hadi 65 years ni violation of constitution by appointing authority
AG alishaishauri Ofisi ya Rais kuhusu Jambo hili, rejea barua ya AG ambayo Jaji Mugasha ameinukuu kwenye barua yake. Aidha, Jaji Mkuu kazi yake siyo kumshauri Rais kuhusu masuala ya Sheria, hiyo ni kazi ya AG.
Jaji Mkuu kazi yake kuu ni Kutafsiri Sheria (Mtawala Mtemi)
 
Uko sahihi, kwamba, Mwanasheria Mkuu ndiye mshauri Mkuu wa Rais kwenye masuala ya kisheria.

sasa Jaji Mugasha naye amekuwa mshauri wa masuala ya kisheria kwa Rais tangu lini?

lakini hoja yangu ya msingi ilikuwa ni; kama Jaji Mungasha alipaswa kuandika barua kwa Rais na kuinakilisha kila ofisi na kuisambaza kwa vyombo vya habari na mitandaoni.
alikuwa na lengo gani kufanya hivyo?!!
 
Alichofanya Jaji Mugasha ni kumkumbusha Rais wa nchi kwamba "kitu alichofanya ni kinyume kabisa na matakwa ya Katiba ya nchi ambayo Rais mwenyewe kwa kinywa chake aliapa kuitetea na kuilinda".
Aidha, alichofanya pia kililenga kuwakumbusha Watanzania wote na watu wote duniani kwamba Rais wa Tz amekiuka Katiba ya nchi yake ambayo ameapa kuitetea na kuilinda.
Je, una swali lingine???
 
Sasa atatoaje ushauri na maamuzi yashafanyika?
 
yeye ndiye mwandishi na mmiliki wa barua aliyo iandika, unadhani nani mwengine aliye isambaza barua hiyo? hawezi kukwepa labda akanushe kuwa sio baru yake.
Barua ni ya kwake hakuna tatizo.
Nikuulize wewe umeisoma? Nakala zinaenda kwa nani? Halafu wewe ndio utuambie umeipataje wakati mwandishi hajakupa nakala wala kukuadress wewe.
Kwa maneno mengine jiepushe na uchawa usio na maana. Kitendo cha Mugasha kuandika barua na baadae ukaisoma wewe wakati barua haikulengi jua kwamba serikali yako na mamlaka zake ni dhaifu sana ktk suala la usiri na utunzaji nyaraka za siri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…