Kitendo cha Jaji Mugasha kukosoa mamlaka hadharani ni utovu wa nidhamu, sio ushujaa

Wewe embu fanya vingine huku hupawezi.
 
Hapana uko wrong nenda kwenye post zangu za wakati wa JPM labda 80% nilikuwa namshtumu sana na akifanya vizuri nilikuwa nampa sifa zake lakini sijawahi kukubali kuzuia mikutano wala sera zake za kiuchumi.
Kwahiyo wewe peke yako ndio ulikuwa chawa ila sio pro max?
Noted.
 
hilo ni fukuto la UNAFIKI hakuna ukweli juu ya kile alicho kiandika zaidi msukumo wa Jeuri, kiburi na unafiki mkubwa.
 
Kuganyaga Katiba ya nchi kwako unaona ni utii uliotukuka?
 
hilo ni fukuto la UNAFIKI hakuna ukweli juu ya kile alicho kiandika zaidi msukumo wa Jeuri, kiburi na unafiki mkubwa.
Kuna mambo mawili hapa.

Kuna mjadala kwamba jambo la kwamba kaandika tu si sahihi. Bila kujali alichoandika.

Kuna mjadala wa alichokiandika.

Haya ni mambo mawili na tofauti.

Naomba uyaelewe na uyatenganishe.

Mimi hata sijafika kwenye alichokiandika, naongelea kwamba kaandika.

Matumaini una uwezo wa kutofautisha mawili haya na kuchambua kwa nuance.

Watanzania wengi wana matatizo ya kufanya mazungumzo yenye nuance.

Natumaini wewe si mmoja wao.
 
Kwahiyo wewe peke yako ndio ulikuwa chawa ila sio pro max?
Noted.
Mimi Pro pro huko ila hatasiku moja siwezi ku support chama hujui hata ni cha siasa au mazishi. Nyinyi mmeachiwa huku mitandaoni tu mitaani mmefyeka mikia nyuma
 
Wewe embu fanya vingine huku hupawezi.
Jibu hoja nitaondoka humu siku nikisikia Jamii forum imegeuzwa jina na kuitwa Chadema forum. Eti Chadema washike dola ahhhh bora ya Zitto Kabwe na chama chake
 
umeeleweka kiranga.
hata mimi nimepata kazi kubwa sana kutoa ufafanuzi juu ya bandiko langu, wengi wao hawakuelewa kwa haraka nilicho kuwa nimemaanisha.
 
Suala la kama yupo sahihi au la litategemea namna ulivyojaliwa na Mungu katika kuchambua mambo.

Kumbuka tasnia ya Sheria tumeirithi kutoka kwa wakoloni ambao kimsingi walifanikiwa kuhakikisha Waafrika wana tunatumia mila na desturi zao katika kutatua matatizo na migogoro yetu. Wao kwakuwa ni utamaduni wao hakuna jambo la ajabu kuongea jambo ambalo unafikiri ni kinyume na taratibu hata kama ukikosea bado haki yako itaheshimiwa lakini kwetu ole wake kama alikosea atapata taabu kwa kiwango kile kile cha kukosea kwake kama ilivyo wahi kumtokea mkaguzi mmoja wa hesabu za serikali.

Lakini Mimi binafsi ninawachukia sana hawa waamuzi wa haki kwa namna walivyo jikita katika kutafuta Lacuna badala ya ukweli.Mfano MTU aliyeua na kukiri anapoachiwa eti kwasababu ushahidi unatofauti kidogo na haubadili kwamba ameua! Najua ni ngumu kuelewa mfano huu mpaka yakukute wanatamba mno kwa kutumia technicalities za kisheria ili kuamua kwa mujibu wa matakwa yao kwakweli ninawaombea kwa Mungu awape stahiki yao mila wanapotufanyia dhuluma kwa maksudi na kuimarisha maslahi binafsi.
 
nafasi yake ya kuwa Jaji ndio inamtaka awe na nidhamu pindi anapo taka kukosoa viongozi walio Juu yake.
alicho kifanya hakifai kwasababu yeye ni kiongozi
Ondoa ujinga hapa sisi tukifanya kosa mnatupa adhabu kali kupitiliza nyie mkikosea mnataka mshauriwe sirini.
 
Uungwana ni kula hela kama alivyosema CAG kwenye ripoti yke.
 
Hakuna kosa hapo,ikiwa ameongea kweli kuficha ficha mambo ndiyo huwa tunaingizwa mkenge kwenye baadhi ya mambo baadaye tunaanza lia lia hatujashirikishwa acha mh.jaji atoboe tu
 
Hakuna kosa hapo,ikiwa ameongea kweli kuficha ficha mambo ndiyo huwa tunaingizwa mkenge kwenye baadhi ya mambo baadaye tunaanza lia lia hatujashirikishwa acha mh.jaji atoboe tu
tusubiri tuone kama alicho jaribu kukisema kama kina ukweli
 
Mtoa mada utambue kuwa Jaji Mugasha Ni kiongozi wako!
Hautakiwi kumkosoa mtandaoni!
Yeye Ni mtumishi wa mahakama za Tanzania
Nenda ukamshauri huko!
 
Mtoa mada utambue kuwa Jaji Mugasha Ni kiongozi wako!
Hautakiwi kumkosoa mtandaoni!
Yeye Ni mtumishi wa mahakama za Tanzania
Nenda ukamshauri huko!
Mie kiongozi wangu ni Rais Wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

wewe kama unaitumikia mahakama nenda kamshauri kuwa kitendo alicho kifanya ni utovu wa nidhamu na anapaswa awajibike.
 
umeeleweka kiranga.
hata mimi nimepata kazi kubwa sana kutoa ufafanuzi juu ya bandiko langu, wengi wao hawakuelewa kwa haraka nilicho kuwa nimemaanisha.
Watanzania wengi ni watu wa team this or team that, one track minded, no nuance.

Ndiyo maana ukimkosoa Samia automatically unaitwa Sukuma Gang, ukimsema Magufuli automatically unaitwa chawa wa Mama, false dichotomy, no nuance.

Ukitaka kujadili kama jaji ana haki ya kukosoa serikali, hawaelewi hoja, wanakwenda kwenye content hata kabla hujaingia kujadili content, unajadili hoja tu kama jaji ana haki ya kukosoa serikali.

Yani mpaka sasa nina hakika kuna watu wanasoma hii post na hawawezi kujua tofauti.

Kukosa nuance ni tatizo kubwa sana. Na huwezi kumfundisha mtu nuance kirahisi.
 
We akili huna,mamlaka zilizojuu ni wananchi kwa ujumla wao,
Amefanya kitendo safi sana,kuonyesha uvunjifu wa katiba,
Ni wapuuzi wanaoamini siasa za kijima za chama kushika hatamu,ndio wanaona shida,
Kama upo TZ,madudu yote yaliyofsnywa na ccm,unataka watu wakae kimya?katiba imevunjwa,sio Siri!jambo lipo wazi,
Siku Moja Moja,angalia hata chanel ya citizen ya Kenya,uone serikali Yao inavyopingwa na wananchi,sio lazima ukubali kila kitu kwa vile TU upo serikalini,akili kama zako,ndio wale wanaoamini,hata polisi,jwtz,lazima waitetee ccm,na mtu akiwa upinzani,hatakiwi kuwa mtumishi wa umma.
 
Msikilizeni Rais Joe Biden wa US ananyukana na Supreme Court ya US kuhusu affirmative action.

Labda mtajifunza kitu kuhusu checks and balance.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…