Kitendo cha Jaji Mugasha kukosoa mamlaka hadharani ni utovu wa nidhamu, sio ushujaa

kwani Yeye Jaji Mugasha yupo chini ya Rais au Jaji Mkuu?
je huoni Jaji Mugasha alitakiwa kwanza ashauriani na Kiongozi wake ambaye ni Jaji Mkuu kisha Jaji Mkuu ndipo aishauri mamlaka ya juu?
Taratibu za Kimahakama hauzijui...tulia endelea kuwa nduza
 
mimi ni mwananchi Mkulima, sijui sheria ila nimesema kitendo cha Jaji Mugasha kuandika Barua kwa Rais kisha kuinakilisha ktk ofisi za chini ya Rais na kusambaza kwenye vyombo na mitandao je? huo sio utovu wa nidhamu?

je? huyo Jaji hakuwa na nafasi ya kuishauri mamlaka kwa njia nyingine? je alishindwa kukutana na Jaji Mkuu aliye ongezewa muda na kumshauri? hadi akaamua kuandika mabarua na kuyasambaza?

Je, kulikuwa na haja ya sisi wananchi kujua mawasiliano yao ya kiofisi?
jaji kala kiapo kulinda na kusimamia sheria za nchi sio za Rais.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona Sinare aliteuliwa ubalozi aka kataa?
Chawa mmeshazoea uchawa akili mgando.
Huyo mama kwa umri wake asingetueliwa hiyo nafasi, na ametumia haki yake kikatiba kukumbusha kuwa katiba imevunjwa.
Hivi una fahamu kuwa hoja za Fatuma Karume zilikua na mashiko kuhusu A.G ila alikosea kuzi wasilisha?
Je ulitegemea kuna chawa yeyote ukiwemo wewe ange challenge uteuzi ule wa A.G?

Kenge bluu wewe.
Kwani katiba imeanza kuvunjwa leo? wakati wa JPM kukataza mikutano ya kisiasa alikuwa wapi? wakati wabunge 19 bila chama wanaingizwa bungeni alikuwa wapi? wakati AG anatolewa alikuwa wapi? katiba ikikugusa wewe tu ndio anakumbuka kuna katiba. hawa wote ni walewale tu
 
Ana miaka mingapi ungesema hapa halafu tujadili. Huyo anataka hata akae mwaka tu kuna maslahi makubwa kuliko kukosa hata mwaka
 
unajua ukiwa mnafiki wa viwango vya juu, tambua iko siku mungu atakuumbua tu bila wewe kujua unacho kifanya kitakuwa na madhara au la.
Rais wetu ni mtu muungwana sana ila kuna baadhi ya viongozi wanataka kutumia uungwana wake kama udhaifu wa kumpelekesha!! lakini hawajui, kamwe usijaribu kumchezea mtu muungwana, au usijifanye mjuaji sana mbele ya mtu muungwana ukadhani hajui kitu!! utaadhirika bila kujua.
Uungwana ni kitendo. Kitendo kama Cha jaji. Soma maelezo yake. Then, kaa kwa kutulia.
 
soma kwa makini andiko langu, sina tatizo na maoni ya Jaji, anauhuru wa kutoa maoni yake lkn hoja yangu ni utaratibu alio utumia kama kiongozi wa umma.

ama anatumiwa na kundi la watu? kajificha kwenye kivuli.
 
Huyo Jaji kasimamia katiba yupo sahihi sana...wanaachwa Wazee madarakani kwa muda mrefu kwa manufaa ya wachache wanajua wanachokifanya bora kaongea mimi nipo upande wake...
 
mimi ni mwananchi Mkulima, sijui sheria ila nimesema kitendo cha Jaji Mugasha kuandika Barua kwa Rais kisha kuinakilisha ktk ofisi za chini ya Rais na kusambaza kwenye vyombo na mitandao je? huo sio utovu wa nidhamu?

je? huyo Jaji hakuwa na nafasi ya kuishauri mamlaka kwa njia nyingine? je alishindwa kukutana na Jaji Mkuu aliye ongezewa muda na kumshauri? hadi akaamua kuandika mabarua na kuyasambaza?

Je, kulikuwa na haja ya sisi wananchi kujua mawasiliano yao ya kiofisi?
Dogo huna akili ya kudadavua
 
Kwani katiba imeanza kuvunjwa leo? wakati wa JPM kukataza mikutano ya kisiasa alikuwa wapi? wakati wabunge 19 bila chama wanaingizwa bungeni alikuwa wapi? wakati AG anatolewa alikuwa wapi? katiba ikikugusa wewe tu ndio anakumbuka kuna katiba. hawa wote ni walewale tu
Siamini kama huu upupu umeandika wewe...umesahau kuwa kipindi cha jiwe nyie wote mlikuwa chawa pro max!!!
 
Kitendo cha Jaji wa Mahakama ya Rufaa cha kuandika barua na kuzisambaza kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kuhusu au Kukosoa Kitendo cha Rais kumuongezea Jaji Mkuu muda wa kuendelea kuwepo kwenye kiti ni kitendo cha ukosefu wa nidhamu kwa mamlaka zilizo juu yake.

Kutoa maoni ni haki ya kila raia lakini inategemea maoni unyatoa wapi na kwa njia gani, Jaji Mugasha alipaswa aishauri mamlaka kwa njia sahihi sio hii aliyo itumia.

tunafahamu kuwa Jaji Stela Mugasha ni Jaji wa Mahakama ya Rufaa hivyo kwa nafasi yake ni kiongozi mkubwa tu ambaye yupo karibu na viongozi wa juu sasa kwa nini aliamua kuandika mabarua na kusambaza?!

kwahiyo lengo lake lilikuwa sio kujenga bali itatafsiriwa kuwa alilenga kubomoa na kudhalilisha mamlaka.

Jaji Stella Mugasha alikuwa nayo nafasi ya kumshauri hata Prof. Jaji Mkuu aliyepo kabla ya kusambaza mabarua yake.

Je? kulikuwa na haja ya kuandika baru kwa Mhe. Rais na kisha kutoa nakala kila ofisi ambazo zipo chini ya Rais?! Mugasha alikuwa na lengo gani?

wakati mwengine ukijifanya mjuaji sana unakuwa na Kiburi na dharau.

mimi ni mwananchi Mkulima, sijui sheria ila nimesema kitendo cha Jaji Mugasha kuandika Barua kwa Rais kisha kuinakilisha ktk ofisi za chini ya Rais na kusambaza kwenye vyombo na mitandao je? huo sio utovu wa nidhamu?
Je, kulikuwa na haja ya sisi wananchi kujua mawasiliano yao ya kiofisi?

Pia soma: Profesa Ibrahim Juma kuendelea kuwa Jaji Mkuu, Rais Samia anavunja Katiba ya JMT?
Inabidi mtu awe na ujasiri wa uwendawazimu kuitetea katiba.
Wajinga wajinga kama mtoa mada ndio hawajui kuwa kstiba inabidi kutetewa kizalendo.
 
Ana miaka mitatu tuu kustaafu.
Sasa midogo hiyo? yeye akipata hiyo mitatu akija kustaafu ana staafu katika level nyingine kuwa mstaafu judge wa rufaa na judge kiongozi ni big different. Miaka mitatu mingi kwenye position hata miwili inatosha. mama wazi kakereka na hili personal sio kwa faida ya nchi
 
Siamini kama huu upupu umeandika wewe...umesahau kuwa kipindi cha jiwe nyie wote mlikuwa chawa pro max!!!
Hapana uko wrong nenda kwenye post zangu za wakati wa JPM labda 80% nilikuwa namshtumu sana na akifanya vizuri nilikuwa nampa sifa zake lakini sijawahi kukubali kuzuia mikutano wala sera zake za kiuchumi.
 
Kitendo cha Jaji wa Mahakama ya Rufaa cha kuandika barua na kuzisambaza kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kuhusu au Kukosoa Kitendo cha Rais kumuongezea Jaji Mkuu muda wa kuendelea kuwepo kwenye kiti ni kitendo cha ukosefu wa nidhamu kwa mamlaka zilizo juu yake.

Kutoa maoni ni haki ya kila raia lakini inategemea maoni unyatoa wapi na kwa njia gani, Jaji Mugasha alipaswa aishauri mamlaka kwa njia sahihi sio hii aliyo itumia.

tunafahamu kuwa Jaji Stela Mugasha ni Jaji wa Mahakama ya Rufaa hivyo kwa nafasi yake ni kiongozi mkubwa tu ambaye yupo karibu na viongozi wa juu sasa kwa nini aliamua kuandika mabarua na kusambaza?!

kwahiyo lengo lake lilikuwa sio kujenga bali itatafsiriwa kuwa alilenga kubomoa na kudhalilisha mamlaka.

Jaji Stella Mugasha alikuwa nayo nafasi ya kumshauri hata Prof. Jaji Mkuu aliyepo kabla ya kusambaza mabarua yake.

Je? kulikuwa na haja ya kuandika baru kwa Mhe. Rais na kisha kutoa nakala kila ofisi ambazo zipo chini ya Rais?! Mugasha alikuwa na lengo gani?

wakati mwengine ukijifanya mjuaji sana unakuwa na Kiburi na dharau.

mimi ni mwananchi Mkulima, sijui sheria ila nimesema kitendo cha Jaji Mugasha kuandika Barua kwa Rais kisha kuinakilisha ktk ofisi za chini ya Rais na kusambaza kwenye vyombo na mitandao je? huo sio utovu wa nidhamu?
Je, kulikuwa na haja ya sisi wananchi kujua mawasiliano yao ya kiofisi?

Pia soma: Profesa Ibrahim Juma kuendelea kuwa Jaji Mkuu, Rais Samia anavunja Katiba ya JMT?
Jaji ametimiza wajibu wake wa kikatiba wa checks and balances.

Kama hoja zake zina makosa, kosoa hoja zake, usikosoe yeye kutumia uhuru na wajibu wake wa kikatiba.

Wananchi pia wana haki ya kikatiba ya kujua mambo muhimu ya kuhusu nchi yao inavyoendeshwa. Jaji amewatendea haki wananchi kwa kuwatimizia haki yao ya kikatiba kwa kuweka uwazi katika jambo hili.

Tatizo letu mihimili haisimamiani. Haiwajibishani. Tunaweka hizi dhana kwenye maandishi kama urembo tu.

Spika Ndugai kasema nchi inauzwa, halafu badala ya kuisimamia kauli yake na kuibana serikali kuu, kajiuzulu. Huu ni udhaifu.

Tunataka kuona mihimili inawajibishana zaidi, ndiyo point ya kuwa na mihimili katika demokrasia.

Kama hutaki hilo, badilisha nchi iwe absolute monarchy.
 
Back
Top Bottom