Kitendo cha jana uwanja wa Taifa kujaa kupita uwezo wake ni Hatari

LICHADI

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2015
Posts
4,491
Reaction score
12,560
Siku ya jana uwanja wa taifa ulijaa hadi watu wakakosa siti wakaishia kukaa kwenye ngazi na wengine wakasimama huku wengine wakikosa kabisa hata kuchungulia tu uwanjani wakaishia kuzunguka nnje, na wengine wengi walikuwa nnje kabisa wakiwa kwenye foleni ya kuingia uwanjani huku ndani tu kukiwa hamna hata sehem ya kukanyaga
IMG_20190324_194609.jpeg

Ni kweli watu jana walionyesha uzalendo lakini linapokuja swala la usalama huwa ni la kwanza, ukienda katika nchi za wenzetu kote huwa wana limit ya watu kuingia uwanjani , siti zikijaa basi ndio mwisho wa ticket kuuzwa na hataruhusiwa mtu mwingine kuingia angalieni hata mechi za ulaya

Inavyoonekana huenda jana ticket ziliuzwa nyingi zaidi ya 60,000 ambazo ndio capacity ya uwanja wetu, inaonekana kulikuwa kuna tamaa katika kuuza hizi ticket, mwishowe mnaweza kuleta majanga makubwa alafu muanze kumtafuta mchawi ni nani

Kuliko kufanya kiingilio bei rahisi 2000 alafu mkaleta tamaa ni heri mngefanya 5000 watu waingie kistaharabu uwanja ujae kwa uwezo wake halisi na sio kujaza watu kama wapo kwenye daladala
, Wizara ya michezo, Tff, mjitafakari kwa hili

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna kitu kinanishangaza kama watu kuuza ticket zaidi ya uwezo wa uwanja...ushishangae kukaa kwenye ngazi hata kama umekata ticket ya VIP A

Shame on TFF
 
Siku ya jana uwanja wa taifa ulijaa hadi watu wakakosa siti wakaishia kukaa kwenye ngazi na wengine wakasimama huku wengine wakikosa kabisa hata kuchungulia tu uwanjani wakaishia kuzunguka nnje, na wengine wengi walikuwa nnje kabisa wakiwa kwenye foleni ya kuingia uwanjani huku ndani tu kukiwa hamna hata sehem ya kukanyaga
View attachment 1053462

Ni kweli watu jana walionyesha uzalendo lakini linapokuja swala la usalama huwa ni la kwanza, ukienda katika nchi za wenzetu kote huwa wana limit ya watu kuingia uwanjani , siti zikijaa basi ndio mwisho wa ticket kuuzwa na hataruhusiwa mtu mwingine kuingia angalieni hata mechi za ulaya

Inavyoonekana huenda jana ticket ziliuzwa nyingi zaidi ya 60,000 ambazo ndio capacity ya uwanja wetu, inaonekana kulikuwa kuna tamaa katika kuuza hizi ticket, mwishowe mnaweza kuleta majanga makubwa alafu muanze kumtafuta mchawi ni nani

Kuliko kufanya kiingilio bei rahisi 2000 alafu mkaleta tamaa ni heri mngefanya 5000 watu waingie kistaharabu uwanja ujae kwa uwezo wake halisi na sio kujaza watu kama wapo kwenye daladala
, Wizara ya michezo, Tff, mjitafakari kwa hili

Sent using Jamii Forums mobile app

Nasisitiza...sio jana tu.

Ila mara zote hasa kwenye mechi ya Simba vs Yanga tiketi zinauzwa zaidi ya uwezo wa uwanja....hivi kuna ugumu gani kuweka namba kwenye kila siti na kuuza accordingly?
 
Ugumu upo mkuu.....wapiga deal wanapata chao cha juu ndio maana wanajikuta tamaa inawatawala kuuza tiketi zaidi ili wapate za ziada.
 
Kibongobongo Zaidi, Mpaka Maafa Yatokee Ndiyo Kutakuwa Na La Kujifunza. Ushamba Na Tamaa Ndiyo Chanzo Ya Hayo Yote. Bongo Hatujali Viwango Vilivyokwa Kujaza. Hata Kwenye Usafiri Mambo Ni Hayohayo Kujaza Kupita Kawaida
 
Mechi ya jana wangeweka nje ya uwanja giant screen ili wale ambao hawakubahatika kuingia ndani ya uwanja wapate fursa ya kuangalia mechi live kupitia hiyo giant screen,pia ingepunguza ile fujo ya hata waliochelewa kutaka kuingia huku uwanja ukiwa umeshajaa.
 
🤔Huyo jamaa aliye simama mguu mmoja kwenye bomba ana afya katulia kama yupo kwenye siti.
 
Kuweka Kiwango Cha Juu Kiingilio Ili Kudhibiti Idadi Ya Watu Si Hoja, Hoja Ni Kufuata Idadi Ya Ujazo Wa Watu Hata Kama Ni Bure Kuingia
 
Back
Top Bottom