LICHADI
JF-Expert Member
- Feb 4, 2015
- 4,491
- 12,560
Siku ya jana uwanja wa taifa ulijaa hadi watu wakakosa siti wakaishia kukaa kwenye ngazi na wengine wakasimama huku wengine wakikosa kabisa hata kuchungulia tu uwanjani wakaishia kuzunguka nnje, na wengine wengi walikuwa nnje kabisa wakiwa kwenye foleni ya kuingia uwanjani huku ndani tu kukiwa hamna hata sehem ya kukanyaga
Ni kweli watu jana walionyesha uzalendo lakini linapokuja swala la usalama huwa ni la kwanza, ukienda katika nchi za wenzetu kote huwa wana limit ya watu kuingia uwanjani , siti zikijaa basi ndio mwisho wa ticket kuuzwa na hataruhusiwa mtu mwingine kuingia angalieni hata mechi za ulaya
Inavyoonekana huenda jana ticket ziliuzwa nyingi zaidi ya 60,000 ambazo ndio capacity ya uwanja wetu, inaonekana kulikuwa kuna tamaa katika kuuza hizi ticket, mwishowe mnaweza kuleta majanga makubwa alafu muanze kumtafuta mchawi ni nani
Kuliko kufanya kiingilio bei rahisi 2000 alafu mkaleta tamaa ni heri mngefanya 5000 watu waingie kistaharabu uwanja ujae kwa uwezo wake halisi na sio kujaza watu kama wapo kwenye daladala
, Wizara ya michezo, Tff, mjitafakari kwa hili
Sent using Jamii Forums mobile app