Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mechi ya jana wangeweka nje ya uwanja giant screen ili wale ambao hawakubahatika kuingia ndani ya uwanja wapate fursa ya kuangalia mechi live kupitia hiyo giant screen,pia ingepunguza ile fujo ya hata waliochelewa kutaka kuingia huku uwanja ukiwa umeshajaa.
YaniTamaa mbele mauti nyuma,ni hatari sana endapo litatokea tatizo uwanjani lazima maafa yatokee
Sent using Jamii Forums mobile app
Nasisitiza...sio jana tu.
Ila mara zote hasa kwenye mechi ya Simba vs Yanga tiketi zinauzwa zaidi ya uwezo wa uwanja....hivi kuna ugumu gani kuweka namba kwenye kila siti na kuuza accordingly?
Watu wa JF mimi siwaelewagi, kuna watu walibeza sana ujenzi wa uwanja wa mpira pale Dodoma ambao utakua na uwezo wa kuchukua watu 85 elfu, waliongea mengi kupita kiasi kwamba serikali inapoteza pesa ya nchi kwa kujenga uwanja mkubwa namna hio ambao hata watu watakua hawajai, sasa mmeuona mfano wa jana? Tunatakiwa tuwe tunaona mbali tusibeze kila jambo jema ambalo serikali inataka kulifanya.