Kitendo cha Kanisa kufungisha ndoa ya Joti huku akiwa amenyoa mtindo wa kihuni ni sahihi?

Uzi wa kijinga huu,kunyoa kiduku,na kunyoa upara una tofauti gn? Kanyoa kidku nywere,chini kanyoa dongo,katoliki hata angekuwa uchi tungemfundisha ndoa ilimrad hasiwe mliwa kiboga tu!
 
weka andiko kiBiblia kuthibitisha huo mtindo wa kihuni! Hayo ni mapokeo tu ndugu. Kwa USA na jamaica unaweza kukutana na pastor amesuka dread lakini kwa Tanzania ni ishara ya uhuni, sasa mfano kama huu una uhusiano wowote na andiko la biblia?
Mambo ya walawi 19:27
 
KANISA KATOLIKI HATUANGALII MUONEKANO WA NJE HAYO MAMBO TUNAMWACHIA MUNGU.HATA BIA ZITAPIGWA LEO BILA SHIDA NA NYIE MNAOKUNYWA KWA KUJIFICHA KARIBUNI.SISI TUNAKUNYWA NA MAPADRE WETU MEZANI BILA YA KUJIFICHA FICHA.
Wee unaonekana mtu mmoja wa njaanjaa sana ndio maana unachosemea ni bia tu
 
Mipaka ni ipi? Kuna kiwango maalumu ambacho hatutakiwi kuvuka?
 
Ndoa sio lazima kufungwa ndani ya kanisa, zinafungwa beach, zinafungwa ndani ya meli, ndani ya boti, ofisini, mahospitalini n.k
 
Manifestation of what is inside of us... Nothing Will be kept as à secret .....unaamua unataka kuvaa nguo gani na vazi halikuangukii tu kama ajali. Hair style tels alot about Who you are
 
Wamekosea sana ukizingatia kuna mabango ya mavazi yasiyo ruhusiwa hapo nje
Kwani nywele ni mavazi???? Nywele zile ni ofisi yake katika matangazo.Harusi ikiisha Jumamosi,Jumatatu anatakiwa ofisini
 
Hakuna kosa lolote.Chukua Biblia soma Amri Kumi kama utaona wanaongelea habari za kunyoa nywele,kama hakuna basi si kosa
 
Watu bwana,tatizo la Watanzania ni wavivu wa kusoma na kufikiri,ukisoma biblia vizuri utaona kuna manabii wengi tu wa Mungu walikuwa Rastafarians,mfano Samson.Alafu mbona hamuwasemi wanaofunga ndoa wamenyoa Zungu?
 
Vp kinamama nao kuna utaratibu gani wa nywele,kwa maana wengine huingia na nywele sio za kwao?afadhali hata ya huyo aliyeingia hivyo.
 
swala la dini jamani tusilifanye kama la siasa kama lipo katazo basi watu wasibishane kwa kua uonekane mkanushaji au mfafanuaji ukiamua kua kwa mungu fata maandiko tuu ,ubishi ni huko huko kwenye mabao ya mikono,si nilisikia humu ndani kuna neno great thinkers ?au neno hili maana yake ni ubishi usio na mashiko,
 
Aliyekwambia huo ni mtindo wa kihuni ni nan.
Maandiko gan yanakataza?
Kuwa na nywele sio shida mradi ziwe safi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…