Kitendo cha Kanisa kufungisha ndoa ya Joti huku akiwa amenyoa mtindo wa kihuni ni sahihi?

Kitendo cha Kanisa kufungisha ndoa ya Joti huku akiwa amenyoa mtindo wa kihuni ni sahihi?

Natumaini mpo salama ndgu zangu wa Wana JF....,Leo Katika mitandao ya kijamii,zimesambaa picha za JOTI AKIWA kanisani akiharalisha jiko na kuliweka ndani,hapa Nampa pongezi.
Ila Huyu bwana harusi kichwani alinyoa MTINDO aina ya kiduku....Sasa nauliza KANISA KUFUNGISHA NDOA YA Mtu alionyoa MTINDO WA KIHUNI NI SAHIHI??
Au Kanisa haliangalii sana suala la maadili.??
===View attachment 619273wabobezi wa masuala ya kidini nielemisheni pengine nipo giza juu ya maadilu===
Kanisa katoliki linapaswa kujichunguza na kujirekebisha naona maadili yanazidi kumomonyoka.
Mwisho itakuwa mikusanyiko yake yake haina tofauti na Fiesta.
 
Mwenye picha ya Taribo West aliyewahi kuwa mcheza soka beki wa Nigeria nguli kisiki atuwekee hapa plz, kwa maelezo ni mchungaji yule jamaa na kijimsunyuli chake kichwani vile vile
 
Kumbuka wanufaika wa ESROW na zilipitia bank mojawapo ya akina nani ndo utajua unafiki wa kanisa la leo!
 
Kwan nan aliyeruhusu ndoa kufungwa na mawigi kichwan Kwa wanawake? Kama hakuna bas jot yupo sahh
 
Nionavyo mimi :Joti ni mfupi mke wake ni mrefu hivyo basi hiyo style ya nywele ilikua ni kusupport height ili mbele ya hadhira asioneka too short
 
KANISA KATOLIKI HATUANGALII MUONEKANO WA NJE HAYO MAMBO TUNAMWACHIA MUNGU.HATA BIA ZITAPIGWA LEO BILA SHIDA NA NYIE MNAOKUNYWA KWA KUJIFICHA KARIBUNI.SISI TUNAKUNYWA NA MAPADRE WETU MEZANI BILA YA KUJIFICHA FICHA.
Mbona kuna baadhi ya mavazi kama zinazoacha mabega au makwapa wazi haziruhusiwi kwa Wanaume?
 
Kiapo Cha ndoa nicha kiroho na kisheria pia. Hakina mahusiano na mwonekano wa mtu. Ali mradi huvunji maadili jamii
 
KANISA KATOLIKI HATUANGALII MUONEKANO WA NJE HAYO MAMBO TUNAMWACHIA MUNGU.HATA BIA ZITAPIGWA LEO BILA SHIDA NA NYIE MNAOKUNYWA KWA KUJIFICHA KARIBUNI.SISI TUNAKUNYWA NA MAPADRE WETU MEZANI BILA YA KUJIFICHA FICHA.
kama huawaangalii muonekano Jumapili moja nenda umevaa vest na bukta
 
Kanisa letu Katoliki limekuwa la Wachumia Tumbo,Linakumbatia matajiri wanaoshibisha matumbo yao huko Parokiani.

Sisemi kuhusu namna alivyonyoa,la hasha kwa kuwa Biblia inasema "tusifuatishe namna ya dunia hii" , sasa Joti alikuwa anaishi na huyu mwanamke zaidi ya miaka mitano( ambapo walikuwa wanafanya ZINAA na watoto waliopata naye ni wa Zinaa.

Kanisani wemekwenda tu kuhakalisha makande ambayo alishakula na kuyabenjua nje-ndani.

Katoliki tumebaki na Agano la kale tukiwazuia washirika wetu kusoma Biblia badala yake tunajisomea Katekismo na maandiko ya kalenda kila mwaka bila tafsiri ya Roho mtakatifu.

Ni wakati sasa wa kuokoka tukiwa huku huku na kumkiri Yesu kuwa Bwana na Mwokozi badala ya Kuabudu sanamu za Yesu na Bikira Maria na watakatifu tukiojifanyia wenyewe!
 
Kwenye Biblia sijaona sehemu wametaja mnyoo rasmi wa waumini/kanisa
 
Back
Top Bottom