Kitendo cha kuongeza muda ndicho kitakachowaunganisha Watanzania kupinga bila kujali itikadi zao

Magu ataaibika na kutolewa kabla hata ya 2022.
 
Shida ni kwamba ukipima ccm alafu ukapima na upande wa nje unaona bora mara mia ccm, ccm tatizo lao kubwa kabisa ni upigaji lakini ni watu wanaofanya maamuzi.

Huwezi kuwapima ccm vizuri wakiwa madarakani, ngoja siku itoke madarakani ndio tuone uimara wao. Hata KANU ya Kenya wakati iko madarakani kilionekana na chama imara, siku kilitolewa madarakani ndio udhaifu na uimara wake ulifahamika.
 
tuprotest then whats next? nan ambae kweli anaweza kufumua kila kitu na kuweka base nzuri? mbowe?

Kwa taarifa yako nchi hii inaweza kuongozwa na mtanzania yoyote mwenye akili timamu.
 
Huwezi kuwapima ccm vizuri wakiwa madarakani, ngoja siku itoke madarakani ndio tuone uimara wao. Hata KANU ya Kenya wakati iko madarakani kilionekana na chama imara, siku kilitolewa madarakani ndio udhaifu na uimara wake ulifahamika.

katika utimamu wa kawaida, kuipima chadema ni wazi haihitaji uphd, tayar kuna unganganiaji wa madaraka kama ccm! tafauti ni kwamba ccm inangangania serikali na mbowe anangangania uenyekiti, tamko zake nyingi znaonyesha chadema huenda likawa ni bomu kubwa zaidi ya ccm. mfano ndani ya masaa 72 naenda kua waziri mkuu! nani alimpitisha? antoa wap mandatory hio? then kama ni ivi ni bora ccm waendeleee tu
 
Mungu atuepushie mbali hii adhabu. Miaka yake 10 inatosha sana. Kwa maumivu na dhuluma aliyotufanyia wafanyakazi, ni wakati sasa wa kuomba kupatikana kwa Rais Mpya Muislamu.

Wakatoliki wanatusulubisha sana mara zote wawapo madarakani. Mimi ni Mkatoliki pure! Ila ukweli lazima usemwe. Wenzetu wa upande wa pili wanajitahidi sana kwenye suala zima la UTU na UUNGWANA. Kuanzia Mzee wa ruksa, Jk, wale wa visiwani, nk.
 
Mnajiongelesha tu. Muda ataongezewa na kakuna lolote litafanyika. Sasa hivi mnaandaliwa tu ki-saikologia. Mtazoe
 
Ni kweli ni makosa Mbowe kuendelea kukaa madarakani zaidi ya miaka 10. Na mimi ni mmoja kati ya watu wasioamini kiongozi yoyote kukaa madarakani zaidi ya miaka 10, na hilo la Mbowe kuendelea kuwa mwenyekiti huwa nalipinga waziwazi hapa jukwaani na popote pale niwapo. Lakini inaonekana kama umeishiwa na hoja kwa kusema Mbowe alisema atakuwa waziri Mkuu ndani ya saa 72, kile ni kipindi cha kampeni kila mtu lazima aongee anachoamini. Sasa kutumia maneno yale kama mashaka yako kwake ya kuhusu madaraka ni kama hujui usemalo, au unashindwa kuweka vizuri unachotaka kutuambia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…