Kitendo cha kutengua maamuzi wafugwa wa kunyogwa ni cha kisiasa

Kitendo cha kutengua maamuzi wafugwa wa kunyogwa ni cha kisiasa

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
7,823
Reaction score
10,857
Nilisoma kwenye gazeti kwamba mkuu wetu hawezi kuuwa mtu hata waliohukumiwa kunyongwa. Tujue mpaka mtu ahukumiwe kunyogwa ni kwamba aliuwa binadamu mwingine au wengine. Kama ni kwa sababu ya dini basi upendo huo na katazo hilo basi lisingeishia kwenye wafugwa.

Kitendo cha Lissu kupigwa risasi na wanasema kwa maamuzi ya hao hao wanasema eti hawawezi kuwauwa wauaji! ni unafiki na kutafuta kupendwa kinafiki. Lakini ni unafiki hata kwa Mungu na Watanzania wanajua hilo. Wakati wa Mwinyi kuna wafugwa walinyogwa haina maana Mwinyi alikuwa hana upendo lakini alifuata maagizo ya mahakama na kuwatendea haki washitaki kama nafasi yake inavyo ruhusu. Lakini Mwinyi mzee mwenye upendo hajawahi kumpiga mwanasiasa, kuweka jela wala kutoa maagizo ya kumpiga mtu risasi kwasababu ni mashuhuri kuliko yeye!

Hivyo tusidanganyane vijana wanaita hizi ni kiki. Msishangae wanataka kubadilisha historia kwasababu tu ya upinzani na watu wamepedwa kuliko wao yaani ukipnda upinzani wanataka watoto wajue si uzalendo! kwasababu tu wana mawazo tofauti. Hao mabeberu tunaowaita mawazo tofauti ndiyo yamefanya watoto wao wawe wabunifu. Tutakuwa na vizazi ambayo havina ubunifu kama tutaanza kufundisha uongo ili tu wachache wakae madarakani.
 
Ni suala la morality, kama Magufuli yupo so religious basi agawe hayo majukumu kwa mtu mwingine.

Ila mtuu unakuta ameua mwenzake asie na silaha kwa kumchana chana na mapanga katika uporaji tu, ameukumiwa kifo halafu aachwe kwakweli hapana.

Naweza kuelewa kuna watu wameua bila ya kukusudia and feel remorse.

Lakini unakuta jambazi linabeba bastola na linakusudia kwenda kuua ili lipate mali, kama ilivyokuwa kwenye sakata la yule jambazi wa mwanza na genge lake waliokodi basi. Njiani baada ya kufika maporini dereva wakamshusha na kumtwanga risasi bahati nzuri hakufa wasamalimia wema wakamuokota.

Unajiuliza kwani wangemfunga mdomo na kitambaa halafu wakamfunga mikono na miguu wangepata kisha kumtupa wangepata hasara gani, ila kuna mijitu aijali uhai wa wenzao halafu inaachiwa.

Busara ingekuwa kusamehe based on case by case evidence na kuona wepi wanastahili msamaha, wepi kitanzi kinawahusu.

Binafsi siamini mtu anaeuwa mwenzake bila ya provocation anastahili msamaha. Magufuli kama awezi sign atoe hiyo kazi kwa wengine ila kuna watu hakuna namna ni kunyonga tu.
 
Huyu jiwe mpenda sifa alinikera Sana. Eti anadai hawezi kutia saini kunyonga watu 250. Lakini alileta mamluki toka Burundi kuuwa wazanzibar wakati wa uchaguzi mkuu.

Halafu haina maana kujimwambafai eti yeye hataki kuwanyonga wafungwa hao. Yeye siyo wa kwanza kutokunyonga. Marais wote waliopita hawakunyonga, lakini hawakuji-proud.

Nyerere katika kipindi chake cha urais cha 23 aliwanyonga watu 3 tu. Marais wengine wote hawakunyonga mfungwa hata mmoja.

Huyu mpenda sifa anajipa sifa pasipo na sifa. Rubbish!
 
Yaani kwa mfano jitu linachoma moto bweni la shule na kuua watoto halafu unajifanya eti una huruma sana?
Ina Maana Magufui ana huruma kuliko Mungu kwenye biblia na Kuruani aliyeweka adhabu ya kifo?

Ina maana Magufuli anajifanya mwi gi wa rehma kuliko Mungu?
Hayo majukumu agawe, kama hayawezi; kuna watu ni wakunyonga tu.
 
Mi naona wote humu ni wanafiki tu na mnaendeshwa na siasa.

Embu imagine badala ya kusema kuwa hao 250 kawa ondolea adhabu ya kunyongwa, angesema kuwa kawa nyonga.

Embu imagine kelele ungezipiga humu ndani. Kuwa ni katili, hana utu, hana huruma, na kadharika.

Acheni unafiki. Humpendi sema Humpendi na siyo kutafuta visingizio vya ajabu ajabu.
 
Hii nchi tangu ilivyoingia mikataba ya kimataifa ya haki za binadamu hukumu ya kunyongwa mpaka kufa ilikua haitekelezwi badala yake mtu aliyehukumiwa hivyo alikua anakaa kusubiri sahihi ya raisi ambayo haiwezi kuja kutokana na hiyo mikataba.

So mtu hujikuta amekaa kifungo cha maisha.

Nyerere na Mwinyi labda na Mkapa kwa mbali ndiyo waliwahi kutia sahihi za hukumu ya kunyongwa mpaka kufa. So Magufuli amefanya rasmi ambacho wenzake walikua wanakifanya kwa usiri.

Tunavyokua tunalilia haki za binadamu lazima tujue nini na nini vinakuja na hiyo package.
 
Hii nchi tangu ilivyoingia mikataba ya kimataifa ya haki za binadamu hukumu ya kunyongwa mpaka kufa ilikua haitekelezwi badala yake mtu aliyehukumiwa hivyo alikua anakaa kusubiri sahihi ya raisi ambayo haiwezi kuja kutokana na hiyo mikataba....
Issue hapa sio human right, rather ‘corrective justice’ an eye for an eye, a tooth for a tooth; and criminal should not benefit for their wrong doings.

Ukikusudia kuchukua uhai wa mtu na wako uchukuliwe vivo hivyo; hiyo ndio namna pekee ya kupata usawa kwenye haki.

Kama serikali haidhani kunyonga ni sahihi basi wafute sheria hiyo; otherwise kuna watu kitanzi kinawahusu.
 
Nilisoma kwenye gazeti kwamba mkuu wetu hawezi kuuwa mtu hata waliohukumiwa kunyongwa. Tujue mpaka mtu ahukumiwe kunyogwa ni kwamba aliuwa binadamu mwingine au wengine. Kama ni kwasababu ya dini basi upendo huo na katazo hilo basi lisingeishia kwenye wafugwa...
Nyerere aliposamehe tulisifia

Huyu tunatafuta blames

Don't hate the player, hate the game
 
Yaani kwa mfano jitu linachoma moto bweni la shule na kuua watoto halafu unajifanya eti una huruma sana?

Ina Maana Magufuli ana huruma kuliko Mungu kwenye biblia na Kuruani aliyeweka adhabu ya kifo?

Ina maana Magufuli anajifanya mwingi wa rehma kuliko Mungu?

Hawezi kuidhinisha hao kunyongwa maana hawana madhara kwenye madaraka yake, lakini tumeona wapinzani wakiuwawa wakati wa uchaguzi na nje ya uchaguzi chini ya vyombo vinavyochukua maagizo toka kwake.

Anataka kuhadaa Umma kuwa ni mtu mwema kwa kutoasaini hao waliohukumiwa, lakini watu wanauliwa kwa amri za kisiasa probably kwa maagizo yake.
 
Ukute huwa wananyongwa ila hatutangaziwi Kuna makala iliandikwa na mwananchi na kumhoji aliyekuwa ananyonga watuhimiwa, hata Uzi upo JF
 
Mi naona wote humu ni wanafiki tu na mnaendeshwa na siasa.

Embu imagine badala ya kusema kuwa hao 250 kawa ondolea adhabu ya kunyongwa, angesema kuwa kawa nyonga...

Ni kweli kabisa angesema wanyongwe, angetusaidia zaidi sisi kusema yeye sio mtu mwenye roho nzuri, lakini kutoka hadharani kuwa hawezi kutia saini ili mtu kunyongwa kwakuwa hataki kuua ni hadaa ya mchana kweupe.

Kuna watu wanaomkosoa na wanaompinga kwenye eneo la kisiasa, mfano uchaguzi wa juzi wameuwawa na vyombo vya dola, je hao wamepata amri ya kuua toka kwa nani? Kama hapendi kuua tungeona uchunguzi dhidi ya askari walioua raia wasio na silaha.
 
Issue hapa sio human right, rather ‘corrective justice’ an eye for an eye, a tooth for a tooth; and criminal should not benefit for their wrong doings...
Mzee wapi hujanielewa?
 
Mzee wapi hujanielewa?
Unachanganya human rights law though still part of justice but has to do with morality and inalienable rights ‘what society believe to be right and wrong’

Whereas corrective justice is to do with distribution of ‘even-handedness’.

Isitoshe kama unadai maraisi wa awali walikuwa awaamini kwenye ‘capital punishment’ kitu gani kiliwazuia kuifuta?

Provided sheria ipo na mahakama inaitumia maana yake Tanzania ni nchi inayonyonga bado kwa baadhi ya makosa.
 
Hapo hapo mabeberu wakisema tuondoe sheria ya kunyonga utasikia watuache sisi ni taifa huru.
 
Back
Top Bottom