Kitendo cha makumi ya watu kujitokeza kuwania nafasi moja tu uspika kimedhihirisha kuwa Taifa hili halina dira wala halijitambui

Nothing to do with ujamaa or ubepari on this. Kuna mambo machache unaweza kusema kuhusu utitiri wa watu wanaochukua fomu:

1. Waliochukua fomu mpaka sasa na wapo competent hawazidi watano
2. Inawezekana watu wameona uspika ni cheo cha kawaida sana, pengine kwa kuangalia jinsi spika aliyepita alivyojirahisisha na kukidharau kiti cha uspika, mpaka kila mtu anaona anaweza kuwa spika.
3. Kwa kuwa wanaochukua fomu za kugombea wanatangazwa sana, watu wanachukulia hii ni stepping stone kwa jili ya nafasi zijazo ndani ya Chama au hata ubunge
4. Chama husika kinatakiwa mbali na hiyo milioni moja kiwe na masharti mengine magumu kwa wenye nia ya kweli na kabla ya kulipia na kuchukua fomu mtu akaguliwe ndio aruhusiwe kulipia.
 
I concur with you on some points. Kikubwa hapa watu wanawaza matumbo yao na siyo utumishi katika nafasi wanayowania!
 
Watu wanataka kula bila kunawa!
 
Ndio ilipaswa kuwa hivi hata kwa nafasi ya uRais kupitia CCM mwaka 2020. Hakikuwa kwa sababu kulikukwa na mwamba aliyemteua Dr. Ackson na kumfanya kuwa naibu wa Spika. Katika hali ya kawaida mtu ambaye hakuwahi kuwa hata mbunge kwa siku moja kupata kuwa naibu Spika huku akishindana na wabunge wengine wazoefu!

Hii ni trailer ya Uchaguzi Mkuu 2025! Itakuwa sawa na 2015!!

Hata CCM uoga umewapungua kulinganishwa na kipindi 2015-2021.
 
Hakuna tofauti na utitiri wa vyama vya siasa uliopo sasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…