Kitendo cha makumi ya watu kujitokeza kuwania nafasi moja tu uspika kimedhihirisha kuwa Taifa hili halina dira wala halijitambui

Hatuwezi kujisifu kuwa hii ni demokrasia bali ni fujo na ukosefu wa mwelekeo na sera za Taifa. Hadi sasa kama Taifa hatujui kama tunafuata ujamaa au ubepari.

Viongozi huandaliwa, hufunzwa na kulelewa. Haiwezekani mtu anakurupuka usingizini akiwa na matongotongo machoni anachukuwa fomu ya kuwania uspika! Hii ni hatari kubwa kwa mustakabali wa Taifa kwani tutakuja kupata viongozi wehu ilimradi tu kwa ushabiki wa kipumbavu wakapata kura za kutosha.

Aidha tamaa ya watu wengi kupata manufaa ya kiuchumi na kuondokana na umaskini uliotopea ndiyo kishawishi kikubwa kuwania nafasi za uongozi katika siasa. Wakati umefika tufanye jitihada za kuondokana na umaskini huu ili watu wengi wajikite katika shughuli za kuzalisha mali na kuinua uchumi vinginevyo Taifa litaangamia na kuishia kugombana sisi kwa sisi.

Wakati umefika tuache kufanya nafasi za uongozi wa kisiasa kama ajira za kujipatia utajiri na badala yake ziwe nafasi za kujitolea. Hii ifanyike kwa vyama vyote vya siasa tuwe na viongozi wanaokerwa na maisha duni ya watu na siyo wanaotaka kujineemesha kiuchumi. Hivi sasa tumefika mahali ambapo vijana wote wanataka kuwa viongozi wa kisiasa na siyo wavuja jasho!

TUJISAHIHISHE!
Nothing to do with ujamaa or ubepari on this. Kuna mambo machache unaweza kusema kuhusu utitiri wa watu wanaochukua fomu:

1. Waliochukua fomu mpaka sasa na wapo competent hawazidi watano
2. Inawezekana watu wameona uspika ni cheo cha kawaida sana, pengine kwa kuangalia jinsi spika aliyepita alivyojirahisisha na kukidharau kiti cha uspika, mpaka kila mtu anaona anaweza kuwa spika.
3. Kwa kuwa wanaochukua fomu za kugombea wanatangazwa sana, watu wanachukulia hii ni stepping stone kwa jili ya nafasi zijazo ndani ya Chama au hata ubunge
4. Chama husika kinatakiwa mbali na hiyo milioni moja kiwe na masharti mengine magumu kwa wenye nia ya kweli na kabla ya kulipia na kuchukua fomu mtu akaguliwe ndio aruhusiwe kulipia.
 
I concur with you on some points. Kikubwa hapa watu wanawaza matumbo yao na siyo utumishi katika nafasi wanayowania!
 
Nothing to do with ujamaa or ubepari on this. Kuna mambo machache unaweza kusema kuhusu utitiri wa watu wanaochukua fomu:

1. Waliochukua fomu mpaka sasa na wapo competent hawazidi watano
2. Inawezekana watu wameona uspika ni cheo cha kawaida sana, pengine kwa kuangalia jinsi spika aliyepita alivyojirahisisha na kukidharau kiti cha uspika, mpaka kila mtu anaona anaweza kuwa spika.
3. Kwa kuwa wanaochukua fomu za kugombea wanatangazwa sana, watu wanachukulia hii ni stepping stone kwa jili ya nafasi zijazo ndani ya Chama au hata ubunge
4. Chama husika kinatakiwa mbali na hiyo milioni moja kiwe na masharti mengine magumu kwa wenye nia ya kweli na kabla ya kulipia na kuchukua fomu mtu akaguliwe ndio aruhusiwe kulipia.
Watu wanataka kula bila kunawa!
 
Ndio ilipaswa kuwa hivi hata kwa nafasi ya uRais kupitia CCM mwaka 2020. Hakikuwa kwa sababu kulikukwa na mwamba aliyemteua Dr. Ackson na kumfanya kuwa naibu wa Spika. Katika hali ya kawaida mtu ambaye hakuwahi kuwa hata mbunge kwa siku moja kupata kuwa naibu Spika huku akishindana na wabunge wengine wazoefu!

Hii ni trailer ya Uchaguzi Mkuu 2025! Itakuwa sawa na 2015!!

Hata CCM uoga umewapungua kulinganishwa na kipindi 2015-2021.
 
Hakuna tofauti na utitiri wa vyama vya siasa uliopo sasa
 
Back
Top Bottom