Kitendo cha Museveni na Kagame kutokuja kumuaga hayati Rais Magufuli kinaashiria nini?

Hawa walikuwa ni marafiki wa mashaka tu.
 
M7 hana shida labda uzee na kuogopa msongamano ...ila huyu pK ni mnafiki flan hivi anaishi kimachale machale
 
Mataga korona yote hii bado mnajaji watu?

Meko kafa kwa korona waache watu wakae makwao
 
Wana majukum mengine mbona jpm alivyokuwa anamtuma mama samia kumuwakilisha ulikuwa huon shida
Acha uchokonoko
 
Kitendo cha hao kutokuja kinaashiria kwamba wanaheshimu taratibu za kupambana na maambukizi ya Covid-19 kwa kuepuka misongamano.
Ni kweli kabisa mkuu. Hawa jamaa wako seroius sana kwenye masuala ya kiafya.
 
Reactions: BAK
Aibu hawa ndo waliompotosha mzee wetu hakuwa vile,bila uswahiba nao mabaya yasingekuwepo,japo dakika za mwisho alianza kurejea kwenye mstari lkn ndo hivyo tena.
 
Wana majukum mengine mbona jpm alivyokuwa anamtuma mama samia kumuwakilisha ulikuwa huon shida
Acha uchokonoko
Hii haiwezi kuwa sababu mkuu. Hiwezekani marais wote wawili kutoka nchi mbili tofauti waugue kwa siku moja na kwa wakati mmoja.
 
Hakuna marefu yasiyokuwa na ncha.
Nimelipenda jina lako, lenye tafsiri kubwa sana si kwa Marekani tu bali hata kwa Dunia.

Yaani imekaa vizuri sana hiyo 911 ambayo ndiyo tarehe 9/11. Siku hiyo wamaekani walikuwa wanapiga namba 911 bila kujua ndio namba ya mafanikio kwa Magaidi katika kubadilisha historia ya Marekani. Hongera mbunifu!
 
M7 alishakwenda Chato nadhani mwaka huu huu na pengine walishaagana. Kagame hata sijui, maana jamaa huyu haeleweki. Ila nasikia huwa anaogopaga sana kwenda hata hospitali kuwaona viongozi wenzake wakilazwa huko.
 
nine one one( emergence call)
Sep(september) eleven(siku ya shambulio) 911sep11
 
Ukiusikiliza wimbo wa super matimila,Remmy ongala alishawahi kuimba,"ukiwa mtenda mabaya unapokwenda pia ni papaya na ukiwa na roho mbaya ee kweli watakuogopa...."ngoja nishie hivyo ni vzr ukausikiliza mwenyewe.
Kweli kabisa mkuu. Imebidi niudownload niusikilize vizuri.
 
[QUOTE="tpaul, post: 38454233, member: 9021"haya sema wew kama msemaji wao shida nn
Hii haiwezi kuwa sababu mkuu. Hiwezekani marais wote wawili kutoka nchi mbili tofauti waugue kwa siku moja na kwa wakati mmoja.
[/QUOTE]
 
Nchi zenye historia ngumu Kama Uganda, Burundi na Rwanda sio tu Rais Kuamka na kusema naelekea nchi flan.

Kama Hali ya Burundi na Uganda ilivyo, Rais akisepa nje ya nchi inakuwa imeisha hioo
 
Wale jamaa ni Covid conscious, Museveni akidaka hii kitu hachomoi, Kagame ni msanii.

Hawataki kufanya kosa kama la JPM kudharau na kuichukulia poa covid 19 jambo ambalo limegharimu maisha yake.
Burundi Vs Rwanda Vs Uganda

viongozi wa hizi nchi zote hawajaja maana. Inawezekana wamekwepa kukutana ana kwa ana maana wana mabifu baina yao.

Burundi Vs Rwanda

Rwanda Vs Uganda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…