Kitendo cha Mwigulu kumtaja Rais kuhusika na ufisadi Ripoti ya CAG ni sahihi?

Hii Nchi ina matatizo sana,sio wabunge sio Wananchi wote hawajui jinsi mifimo ya uendeshaji wa Nchi.

Nilisema siku ile kuwa SAMIA anachukulia watu kama wajinga na ni kweli ni wajinga,labda anafanya kwa malengo yake ya kisiasa.

Malipo ya projects kubwa hizo zinapitishwa na Katibu Mkuu Kiongozi,ambaye ana pata idhini moja kwa moja kutoka kwake.Sasa iweje aseme watu wanaongeza bei.
 
Hakuna mantiki kuamuangushia Mwigula Nchemboo jumba bovu wezi ni wengine ye anaingiaje? Watu wanaweka mezani documents ziko sawa utajuaje kuwa ukilipa hawatekelezi?
 
Mwigulu yupo sahihi kabisa,huyo spika wenu anayeendasha Mhimili wa Serikali lakini hajuo uendeshaji wa serikali ni matatizo.
 
ni sahihi kabisa.....inakuwaje rais unamteua chokoraa asiye na adabu kuwa mawaziri? tena waziri wa fedha na mipango?
 
Hii nchi ni majanga.

Wananchi hawajitambui na viongozi hawajitambui.

Ujinga ni furaha!
 
Hii nchi ina sheria za kipumbavu na kilofa sana zilizotungwa na malofa.Rais akikosea anajifanya hajahusika lakini akifanya cha kusifiwa anadai kafanya yeye.Mwiguku uko sahihi kabisa rais kaidhinisha na kama kukosea na yeye asijitoe.
 
"Stupid" natamani sana "Prof. Mussa Assad" ateuliwe waziri wa fedha yule bwana anahofu ya Mungu.
 
Mwigulu sio mwadilifu ila alichokisema bungeni ni cha kweli tupu ila mnataka kumtoa kafara (scapegoat) kuepuka dhahama ya siku chache zijazo kwenu ninyi watawala wezi, walafi na wabadhirifu wa mali za umma na wenye dhuluma lukuki dhidi ya wananchi wa kawaida.
 
Rais ali bariki wizi. Wale kwa urefu wa kamba yao.
 
Ww ni GT,unastahili nyota 3
 
Tatizo ni kwamba Rais huwa anapewa sifa kuwa amepeleka fedha mahali labda kujenga barabara au hospitali au shule. Kwa muktadha huo Rais ndio huidhinisha malipo hayo kwa hiyo kuhalalisha hiyo sifa anayopewa!! Sasa huo ni mtego mbaya sana!! Ukukubali sifa inabidi ukubali pia lawama kama pesa zimepigwa maana ulishakubali kuwa pesa huwa unapeleka wewe!! Taasisi ya urais iachane na sifa za binafsi ambazo siyo halisi badala yake sifa iende kwa serikali moja kwa ,moja kupitia watendaji na lawama ziende kwa serikali moja kwa moja pia kupitia watendaji!!! Ukikubali sifa ni ngumu kukataa lawama!! Maana zote zinatokana na pesa zinazodaiwa umepeleka wewe kwa maana ya kuidhinisha!!
 
Rais ali bariki wizi. Wale kwa urefu wa kamba yao.
Hapo kwa kweli alikosea!! Alilalamika tu kuwa wanakula kwa kuvuka urefu wa kamba zao hadi wanavimbiwa!! Ilitoa picha kuwa wakila kwa mujibu wa urefu wa kamba zao na wasivimbiwe hilo siyo tatizo!!
 
hakujua kama atakuwa mwizi
Mwigulu ni mwizi tangu enzi za Kikwete na kuna tuhuma ilikuwa inamhusu moja kwa moja ila kwa vile ccm imekaa kwa maslahi ya kulindana ndiyo maana unaona bado yupo kwenye Baraza la Mawaziri na kupewa Wizara nyeti ambayo ndiyo Roho ya nchi.
 
Sijui ni masikio yangu,nilimsikia Waziri wa Fedha na Mipango , wakati anajibu hoja ya Mbunge wa Simanjiro,akisema ninanukuu "Utaratibu wa malipo ya Serikali kuidhinishwa na Rais ,ulianza kipindi cha Serikali ya awamu ya nne wakati yeye akiwa naibu Waziri wa Fedha na umeendelea kwa awamu ya tano na awamu ya sita".

Maoni yangu

-Kumbe Matakwa ya Katiba yetu yameanza kuvunjwa inakaribia miongo 2,
-Viongozi wetu,wanatupiga changa la macho wanapoahidi kulinda na kutetea Katiba ya JMT., wakati wanafanya kinyume chake.

Ushauri
-Viongozi waheshimu na kulinda Katiba ya JMT kama wajivyoapa.
-Mchakato wa Katiba Mpya,uharakishwe/Ukamilishwe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…