Sio cha kiungwana kabisa .... hili jeshi bhana baadhi ya askari wanafanya kazi kubwa sana kuleta mahusiano ya jamii ila wengi wanaharibu kabisa kazi za wenzao akiwemo mkuu wao IGP , yan jamaa utadhani hayupo jeshi linajiendea lenyewe kila mtu anajiamulia tu atakavyo , sijui ni upole kupitiliza au hajali wananchi au mfumo umemharibu
Mkuu; Umesema:
"Sio cha kiungwana kabisa ...." kwa mtizamo wako au tuseme ungelikuwa wewe ndo Polisi aliyekuwa
on duty hapo kwenye eneo la tukio ungelifanyaje?
Huyo kijana unayemtetea, kwani aliona shida gani kuyachukua maharage yake kutoka kwenye mtaro? (kumbuka yy hakukamtwa.)
Mbona Mtaro ulikuwa mkavu hakukuwa na maji machafu na isitoshe maharage pia yalifungwa vizuri kwenye kiroba kisichoweza kuingiza maji?.
Ukizingatia kiukweli na kiuhalisia, huyo kijana alivunja Sheria na alistahili kushtakiwa kwa mujibu wa sheria aliyoivunja na mchakato wa kisheria dhidi yake ungemtia Hatiani na angeweza kupewa adhabu ya kifungo gerezani. Zoezi la kumkamata, kumweka rumande asubiri hadi zoezi la mwenge lipite sio chini ya mwezi mmoja-hakuna mdhamana kwani wanaweza kumzushia kesi ya Ugaidi. Je Familia yake/wale wanaomtegemea ingekuwaje? Zoezi la mwenge likipita wahusika kurudi vituoni mwao, wangelimfungulia jalada (
kwa huruma) kosa la kuingilia Msafara wa Rais (Kumbuka mwenge unamwakilisha Rais) halafu ndipo awajibike kutoa maelezo..., kufikishwa mahakamani ,kesi ipangiwe tarehe na n.k. n.k........Huoni inachukua muda mrefu na Mtuhumiwa atakuwa ameathirika mno kwa kupoteza muda usio na ulazima halafu baadaye aje kufungwa gerezani (kuanzia 1yr - 5yrs wweza pia kusoma
kifungu cha 43 cha Sheria ya Usalama barabarani sura ya 168). ujiridhishe zaidi kuhusu ni kitu gani hao polisi walimwepushia huyo kijana na ndo uone kama kweli walitenda visivyo.
Unaona kuwa kwa Polisi kufanya uungwana wa kuyatupa maharage ambayo yangelitumika kama kithibiti mahakamani walikosea?
Unaona pilisi walikosea kumpotezea kosa lake ili baadaye e.g. baada ya dk. 10-15 mwenge utakuwa umeshapita na yy kijana aweze kuendelea na shughuli yake kusaka riziki ya kila siku?
Unashangaa maharage kutupwa mtaroni? Je, umewahi kupitia mafunzo Jeshini (Ulibahatika kushiriki mafunzo yoyote ya Kijeshi walau hata JKT ?) au hata kuona clips za mazoezi ya kijeshi? Kama hayo hujawahi kushuhudia then una haki ya kushangaa na kusikitika sana mahararage kutupwa mtaroni tena mtaro mkavu na hayo maharage yamefungwa kwenye kiroba kisicho pitisha maji.
Ni hayo tu.