Unafikiri wangemkamata kwa kosa la kuingilia msafara kuna ambaye angehoji?Kwa nini huyo kijana hakusubiri hao wakimbiza mwenge wapite halafu ndipo yy aendelee na mzigo wake? Si angeliweza kusababisha ajali. Kijana hana subira? Aliona kwamba shughuli yake ni muhimu zaidi ya kuzingatia usalama barabarani?
Sivyo kabisa. Kazi yao ni kulinda Raia na Mali zao.Polisi wa Tz ni kikundi cha KIGAIDI
Kama kuna sheria zimewekwa kwanni uvunje alafu utakwe kuonewa hurumaShauri zao hawajui hata wahenga walionya kwa mseemo wa "Mwenye nguvu mpishe".
Huo muda wa kumkamata, kumpeleka kituoni, kumfungulia jalada, kumpeleka mahakamani ungelitoka wapi? Unadhani zoezi la mwenge lingesubiri hayo yakamilike ndo liweze kuendelea? Walichofanya ni kuzuia kosa lisifanyike na kuokoa muda.Unafikiri wangemkamata kwa kosa la kuingilia msafara kuna ambaye angehoji?
Akili yako inakuambia hicho walichofanya ni sahihi?
Hapo ni matumizi ya Hekima na Maadili ya kazi. i.e. Kama wangeifuata Sheria iliyowekwa, ujue hapo kuna mlolongo mrefu hadi Haki ionekane kutendeka huko mahakamani. Mwenge hautasubiri hilo. Kwa kuzingatia Hekima na Busara na Weledi katika Utendaji ilionekana ni vyema kupotezea kosa(Funika kombe mwanaharamu apite) lakini yule kijana naye aoneshwe kwamba hapo alikosea asirudie tena siku nyingine.Kama kuna sheria zimewekwa kwanni uvunje alafu utakwe kuonewa huruma
Watu wanasema sio uungwana wakati majamaa walichokifanya mpaka nashangaa mbna wana huruma sana.Hapo ni matumizi ya Hekima na Maadili ya kazi. i.e. Kama wangeifuata Sheria iliyowekwa, ujue hapo kuna mlolongo mrefu hadi Haki ionekane kutendeka huko mahakamani. Mwenge hautasubiri hilo. Kwa kuzingatia Hekima na Busara na Weledi katika Utendaji ilionekana ni vyema kupotezea kosa(Funika kombe mwanaharamu apite) lakini yule kijana naye aoneshwe kwamba hapo alikosea asirudie tena siku nyingine.
Sio sahihi mkuu. Kwani huyo kijana angelisubiri ingemchukua dk. ngapi na huo mwenge uwe umeshapita? Hebu ona hasara aliyojipatia kutokana na kushindana na kuonesha dharau kwa jambo la muda mfupi sana i.e. mwenge kupita hapo alipopataka nae kupita. Tunagombania fito wakati tunajenga nyumba moja. Mwenge na shughulizake na boda na shughuli zake lakini barabara iliyokuwa inatumika ni hiyo-hiyo yetu sote.
Mkuu; Umesema: "Sio cha kiungwana kabisa ...." kwa mtizamo wako au tuseme ungelikuwa wewe ndo Polisi aliyekuwa on duty hapo kwenye eneo la tukio ungelifanyaje?Sio cha kiungwana kabisa .... hili jeshi bhana baadhi ya askari wanafanya kazi kubwa sana kuleta mahusiano ya jamii ila wengi wanaharibu kabisa kazi za wenzao akiwemo mkuu wao IGP , yan jamaa utadhani hayupo jeshi linajiendea lenyewe kila mtu anajiamulia tu atakavyo , sijui ni upole kupitiliza au hajali wananchi au mfumo umemharibu
Watu hujisemea hovyo tu bila kuangalia Sheria inasemaje.Watu wanasema sio uungwana wakati majamaa walichokifanya mpaka nashangaa mbna wana huruma sana.
Hvi ingekua wanajeshi je
Hawakuwa na namna.Walikuwa wanaenda na muda. Hapo ujue walimsamehe kiania tu; wangeliweza kumweka hifadhini kituo chochote kilicho karibu kwa muda hadi zoezi la mwenge lipite ndipo warudi kuendelea naye. Usicheze na mamlaka.
alikamatwa pia.
Kuajiriwa kwako serikaln kusikutie upofu ww ajira mpyaaaaaaWatu hujisemea hovyo tu bila kuangalia Sheria inasemaje.
Ingekuwa ni wanajeshi(JW); nadhani huyo kijana mida hii angelikuwa na POP miguu yote miwili kwani MP huwa hawana muda wa maswali na wa kutupa viroba mtaroni. Hawacheki na kima hata dk. moja.
La; sivyo kabisa. Pamoja na upofu wangu na wala sio mwajiriwa serikalini lakini kwa upendo tu nimewawekea hadi kifungu cha Sheria ambayo ikisimamiwa ipasavyo na kwa ukamilifu wake, lazima mtu aombe poo.Kuajiriwa kwako serikaln kusikutie upofu ww ajira mpyaaaaaa
Mkuu; Umesema: "Sio cha kiungwana kabisa ...." kwa mtizamo wako au tuseme ungelikuwa wewe ndo Polisi aliyekuwa on duty hapo kwenye eneo la tukio ungelifanyaje?
Huyo kijana unayemtetea, kwani aliona shida gani kuyachukua maharage yake kutoka kwenye mtaro? (kumbuka yy hakukamtwa.)
Mbona Mtaro ulikuwa mkavu hakukuwa na maji machafu na isitoshe maharage pia yalifungwa vizuri kwenye kiroba kisichoweza kuingiza maji?.
Ukizingatia kiukweli na kiuhalisia, huyo kijana alivunja Sheria na alistahili kushtakiwa kwa mujibu wa sheria aliyoivunja na mchakato wa kisheria dhidi yake ungemtia Hatiani na angeweza kupewa adhabu ya kifungo gerezani. Zoezi la kumkamata, kumweka rumande asubiri hadi zoezi la mwenge lipite sio chini ya mwezi mmoja-hakuna mdhamana kwani wanaweza kumzushia kesi ya Ugaidi. Je Familia yake/wale wanaomtegemea ingekuwaje? Zoezi la mwenge likipita wahusika kurudi vituoni mwao, wangelimfungulia jalada (kwa huruma) kosa la kuingilia Msafara wa Rais (Kumbuka mwenge unamwakilisha Rais) halafu ndipo awajibike kutoa maelezo..., kufikishwa mahakamani ,kesi ipangiwe tarehe na n.k. n.k........Huoni inachukua muda mrefu na Mtuhumiwa atakuwa ameathirika mno kwa kupoteza muda usio na ulazima halafu baadaye aje kufungwa gerezani (kuanzia 1yr - 5yrs wweza pia kusoma kifungu cha 43 cha Sheria ya Usalama barabarani sura ya 168). ujiridhishe zaidi kuhusu ni kitu gani hao polisi walimwepushia huyo kijana na ndo uone kama kweli walitenda visivyo.
Unaona kuwa kwa Polisi kufanya uungwana wa kuyatupa maharage ambayo yangelitumika kama kithibiti mahakamani walikosea?
Unaona pilisi walikosea kumpotezea kosa lake ili baadaye e.g. baada ya dk. 10-15 mwenge utakuwa umeshapita na yy kijana aweze kuendelea na shughuli yake kusaka riziki ya kila siku?
Unashangaa maharage kutupwa mtaroni? Je, umewahi kupitia mafunzo Jeshini (Ulibahatika kushiriki mafunzo yoyote ya Kijeshi walau hata JKT ?) au hata kuona clips za mazoezi ya kijeshi? Kama hayo hujawahi kushuhudia then una haki ya kushangaa na kusikitika sana mahararage kutupwa mtaroni tena mtaro mkavu na hayo maharage yamefungwa kwenye kiroba kisicho pitisha maji