Kitendo cha Putin kuiitisha jeshi la akiba ni maana yake?

Asipokuelewa hapa achana naye
Sio kama hajaeleweka ila vita ni strategic! Urusi alishapeleka jeshi la akiba mpaka Syria au Wagner Group, Pia wapo baadhi ya nchi za Africa huku waliletwa kitambo sana
Sasa nikupe hbari kuwa Russia bado hajatumia jeshi lake ila huko Ukraine ana wale ambao wakitaka kujitenga ndani ya Donbas, Luhansk wana wanajeshi tele huko Ukraine ambao wako chini ya Russia, pia wana ao Wagner Group ambao ni wanajeshi wa kukodi amba wanamafunzo yote ya kivita pia ana Chechens hawa ni wanajeshi kabisa walio ndani ya ndani ya Russia ambao Russia anawatambua kama moja ya askari wake wa akiba.
Kwaio sio kama Russia kamaliza wanajeshi wake ila bado cos Russia ana tahadhali na NATO zaidi sio Ukraine mwenyewe kama mwenyewe.
 
Urusi ni nchi kubwa kijiografia, inahitaji Askari wengi kulinda territory yake. Ina active soldiers laki tisa na reserve ya Askari milioni 1.1, inakadiriwa imepoteza Askari 54000 na wengine wapatao elfu 80 kujerehiwa katika OP ya Ukraine.

Kwahiyo siyo kaishiwa, ila anaongeza nguvu kukabiliana na hatari inayokuja Kama vita itaendelea kwa muda mrefu zaidi . Lakini pia Kama tahadhari kwa nchi za magharibi iwapo zitaamua kuwa involved directly.

Sababu nyingine ni kupata Askari zaidi wa kulinda territory mpya iliyopatikana ya Donbass, kumbuka Donbass ni kubwa zaidi ya nchi ya Hungury na ubeligiji.

Rejea pia post 21# kwa ufafanuzi zaidi
 
Habri wajomba nazn kunawale vpanga/wachambuzi wenye IQ zao tusaidiane hapa

1:- Kuiitisha jesh la akiba inamaana Jeshi kamili la urusi limemalzwa kwenye uwanja wa pambo..?
Hapana, kusema limemalizwa ni makosa maana kama ingelikuwa hivyo basi Ukraine ingeyatwaa maeneo yote yaliyochukuliwa na Urusi. Ni sahihi kusema limepungua, (hata hivyo Urusi hakupeleka askari wengi wa jeshi lake).
2:- Huu ni mwanzo wa vita kamili kwa mrusi zidi ya NATO
Hapana, vita kamili kati yao inategemea na vita itayozuka baina ya Urusi na nchi mwanachama wa NATO, kwenye hili mpaka Ukraine atakapokubaliwa kujiunga NATO wakati vita inaendelea, jambo ambalo sioni likitokea.
3:- JESHI kamili la mrusi (activ personal lipo )?
Naam lipo, na kiasi kikubwa cha askari wake hawako Ukraine, kama Urusi wanavyoona kuwa hii sio vita ila ni “Oparesheni maalum”.
Hivyo kwenye Oparesheni Jenerali makini katu haweki askari wake wote.
4:- Mrusi anawez kujishusha mwenyew kuacha vta hii au tunaenda katik vta ya maangamizi?
Urusi hawezi jishusha, maana huo ndio utakuwa mwisho wake. Kitakachotokea ni kwamba
Majimbo ya Ukraine ya Zaporizhzhia, Lugansk, Donetsk na Kherson yatapiga kura ya ndiyo kujiunga na Urusi, Bunge la Urusi litakubali kuyapokea hivyo mpaka wa Magharibi ya Urusi utatanuka mpaka kwenye majimbo hayo na Crimea.

Kutokea hapo shambulio lolote la nchi yoyote dhidi ya majimbo hayo yatahesabika kuwa ni shambulio dhidi ya ardhi ya Urusi.

Kwa msingi huo Putin atapata Uhalali wa kutangaza vita rasmi ambapo jeshi (active personel) na hata la akiba ikibidi, vifaa vyote vya kisasa, miundombinu, silaha na mabomu hatari ya Nyuklia yatakuwa nk halali kutumiwa na Urusi katika ‘kuilinda ardhi yake’.

Na hapo naweza sema naam, tunakwenda katika vita vya maangamizi (audhubillahi min dhalika)
 
Ila Putingo kapatikana this time around.....
 
[emoji122][emoji122] huo ndio uhalisia hambao mazombi wa Putin hawataki kuusikia
 
Mfano wako wa mbegu na chakula cha nyumbani ni mfano dhalili sana. Hauendani na muktadha wa suala husika, hapa inazungumziwa vita, sio mbegu za chakula wala fedha za akiba, ni VITA!!

Amiri jeshi mkuu makini katu hawezi watia hatarini askari wake bora ilhali anajua fika atawahitaji.

Kwa muktadha huu, Ukraine ni kama sekunde za mwanzao ya dakika ya mwanzo kwenye siku za mwanzo za miezi ya mwanzo ya migogoro ya miaka mingi.

Kwa wataalamu wa mikakati ya kijeshi wanaelewa fika kinachofanyika.
Lakini suali linakuja je atafanikiwa? wataalamu wanatwambia ushindi kwa Putini ni 0.05%,
Wataalamu wepi hao? Weka nukuu zao hapa!
Naam kuna askari (active personel) na walienda mwanzo na wapo wanapigana ila suala ni kuwa idadi ya hao ‘active personel’ walio Ukraine ni ndogo sana na waliobaki Urusi ni kubwa mno achilia mbali jeshi la akiba, na hii ndiyo inawafanya wachambuzi baadhi kuona kuwa Urusi haijaji’Commit’ kwa 100%.
 
Mfano wako wa mbegu na chakula cha nyumbani ni mfano dhalili sana. Hauendani na muktadha wa suala husika, hapa inazungumziwa vita, sio mbegu za chakula wala fedha za akiba, ni VITA!!
Mkuu nimetumia mfano huu kwa sababu ukitoa maneno yako uliyopachika hapa Putini mwenyewe jana ametangaza wazi kwamba anaenda "ku-mobilize jeshi la lake la akiba wapatao laki 3" sasa jiulize swali hilo jeshi lake liko wapi mpaka anaenda kutumia akiba?? tena raia? wafungwa?
Amiri jeshi mkuu makini katu hawezi watia hatarini askari wake bora ilhali anajua fika atawahitaji.
Ndio mana wananchi wapatao 1000 wameandamana kupinga watoto wao kupelekwa vitani, na sasa putin amewakama waandamanaji wanaopinga na kuwaswekwa ndani kwamba ni lazima watoto wao waende kufa vitani jamaa ni katili hajali maisha ya mtu mwengine.


Hakuna Askari wa Russia aliye active ukiangalia zile clips wanajeshi wa Russia wametelekeza mitambo yao ya kivita na silaha wote wamekimbia lakini kuna miji jana juzi Ukrean walienda kwa ajili ya mapambano wakakuta jeshi la urusi tayari wameshatimua zao mbio kuokoa maisha yao hakuna active personel hata moja
 
active personel kwiyo wale.waliouwawa na maparashuti ni wa akiba
 
Kwa heshima zote, Mkuu unajua nini kuhusu mikakati ya kijeshi?
Ndio mana wananchi wapatao 1000 wameandamana kupinga watoto wao kupelekwa vitani, na sasa putin amewakama waandamanaji wanaopinga na kuwaswekwa ndani kwamba ni lazima watoto wao waende kufa vitani jamaa ni katili hajali maisha ya mtu mwengine.
Hili ni suala la kawaida sana, sidhani kama kuna mtu timamu anapenda vita, kuna mtu anapenda mwanawe, mumewe, mpenziwe, mamaye, dadaye au nduguye yeyote kufa??

Hata Ujerumani wakati inajiandaa kuunganisha jamii za wajerumani wote Wanasiasa wengi wa Prussia waliitaka vita dhidi ya Austria lakini Otto Von Bismarck alisimama bungeni mwaka 1850 akawaambia
“Woe to the statesman whose arguments for entering a war are not as convincing at its end as they were at the beginning”

“Ole wake mtawala ambaye hoja zake za kuingia katika vita hazitakuwa na mashiko vita ikiisha kama zilivyokuwa na mashiko vita ilipoanza”
Akawaonya kwa kuwauliza watawajibu nini wakulima ambao mashamba yao yataharibiwa? Wazazi ambao watoto wao watauwawa?

Lakini amini usiamini miaka michache baadae Bismarck aliamuru jeshi kuingia vitani na Austria, alikua anakula ‘timing’ tu.
Unajua maana ya ‘active personel’?
Ni askari ambaye muajiriwa na ‘Full-time’ analitumikia jeshi.

Sasa Ukraine hakuna hata ‘active personel’ mmoja wa jeshi la Urusi?
 
active personel kwiyo wale.waliouwawa na maparashuti ni wa akiba
Hapana si wa akiba tu, na ‘active personel’ wapo.

Hoja yangu ilikuwa juu ya idadi yao. ‘Active personnel’ walio Ukraine ni wachache kulinganisha na waliobaki Urusi mkuu.
 
Miji gani ebu nitajie
 
sasa we mzee hao wagner na checheny plus jeshi la urus si ndo walikua wavamizi wa kwanza kuingia ukraine wakachezea kipigo mpaka wamerudi mipakan uko watakua na maajab gan tena wakirud kulinda hiyo miji yao wakiwa na hao wafungwa na raia wenye mafunzo ya siku chache waki kabidhiwa hizo silaha??
 
Kama na hapa hajakuelewa Basi, hatakaa aelewe tena, labda Kama analeta ushabiki maandazi
 
Wagner group ni PMC, army for hire.
 
Kwa heshima zote, Mkuu unajua nini kuhusu mikakati ya kijeshi?
Hakuna kuhusu mikakati usitoke kwenye mada tunasema sasa tuko mwezi 7 kwenda wa 8 toka february kwa hiyo muitayo operation eleza kwanini "Putini amelzaimika kutumia jeshi la ziada?" Kwanini?
Hili ni suala la kawaida sana, sidhani kama kuna mtu timamu anapenda vita, kuna mtu anapenda mwanawe, mumewe, mpenziwe, mamaye, dadaye au nduguye yeyote kufa??
Mulituambia Urusi ni super power imewezekana vipi vita munaiyoiita operation ambayo si vita kamili miezi 7 tu munalazimika kuhamasisha raia kuvaa gwanda kwenda vitani? hata mwaka mmoja haujafika ni kwa kiwango kipi Urusi imefilisika kijeshi na kuamua kuwapeleka raia vitani kwa miezi 7 tu.
Unajua maana ya ‘active personel’?
Ni askari ambaye muajiriwa na ‘Full-time’ analitumikia jeshi.

Sasa Ukraine hakuna hata ‘active personel’ mmoja wa jeshi la Urusi?
Kwa tafsiri hiyo unataka kuniambia kwamba Ukrean ilikuwa ni nchi ya kwanza ulimwenguni ambayo haikuwa na active personal? otherwise ndio kwanza naskia kwao
 

kichekesho kingine hiki huku.
kwahio uto tu javeline na Himars nne na propela gan sjui ndio combination ya nchi 30. ?
kua siriaz bro. tumia common sense bas
 
Sasa nini kinamfanya atutangazie kuwa anapeleka jesh la ziada....c angepeleka tu ili impact yake iongee?....actions speak lauder than words...hayo mengine ni kelele tu za kubanwa pumz....... sasa vita kaamua kuiamishia.mdomoni kama wafuasi wake wa buza na kwa mtogole
 
Kwa kifupi hivi vita vimewakuta Warusi, tulikua tunaambiwa kwamba Warusi wanakula bata huku vita vikiendelea, sasa imewakuta, watalazimishwa kwenda kupigana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…