Kitendo cha Simba SC kumtelekeza Fraga ni cha kinyama sana

GENTAMYCINE karibu sana ulitolee ufafanuzi
Siku zingine muwe na Akili tafadhalini. Klabu ya Simba haijaachana na Mchezaji Gerson Fraga kwa Chuki, Ugomvi au Majungu bali ni kwa 'Mutual Termination of a Contract' ambayo imehusisha pande zote mbili na zikakubaliana. Hivi utawezaje Kukaa na Mchezaji ambaye hutomtumia 'for the rest of the Season' huku ukiwa unamlipa Tsh Milioni Saba kila Mwezi?

Ilichokifanya Simba SC ni kuachana nae tu 'Kiungwana' huku wakimlipa Pesa kidogo kwa 'Percentage' fulani Kimkataba kisha wanamnunua ( wanamsajili ) Mchezaji mwingine mahiri kama Yeye wa nafasi yake na ambavyo wamefanya tayari kwa Kumsajili 'Uganda's Cranes Defensive Midfielder' Thaddeo Lwanga ambaye kuna hatari kwa uwezo wake mkubwa Uwanjani Simba SC tukamsahau upesi Fraga.

Na ili uone kuwa Klabu ya Simba haina 'Uswahili' na inaendeshwa 'Kiustaarabu' huyo Frage mwenyewe ameridhia Maamuzi ya Klabu lakini kama haitoshi bado pia anaendelea Kuwasiliana vyema na Mashabiki wa Simba SC Mitandaoni huku akiwatakia Mafanikio katika kila Mechi zao. Hivi Simba SC ingemtekeleza au kumsusia kwa Mchezaji Mweledi na anayejitambua vyema Kisheria na Mikataba angenyamaza?

Acheni Majungu yenu tafadhali!
 
We

Kuambiwa ulitolee Jambo ufafanuzi ndio majungu?
Hebu tuambie majungu uliyokuwa ukiyasema kwenye post yako hapo juu Ni yepi?
 
Acha kunipotezea muda tafadhali. Sikukuomba unitaje ( uniite ) bali nimeamua kutoa Ufafanuzi ule baada ya Wewe tu Kushoboka na Kuniita sawa?
 
Ni kawaida ya Utopolo kuzusha maneno ambayo baadae huonekana kama kweli.Walizusha Simba imekula hela ya rambirambi ya Mafisango , kumbe ndugu walilishwa tango pori waseme wapewe pesa wakati uongozi uliamua rambirambi zitumike kugharamia vitu na sehemu iliyobaki ndio wapewe familia.Yanga wakazusha Simba imekula pesa ya rambirambi, wakaenda mbali na kusema laana ya kula rambirambi ndio imefanya Simba isichukue ubingwa, sasa Simba imechukua back to back mara 3 wamesahau wimbo wa laana ya Mafisango.
 
Mmechukuwa kombe Mara tatu au mmepora kombe Mara tatu kwa msaada wa tff na kamati zake ikiwemo bodi ya ligi.
 
Mashabiki wa Yanga wacheni kuchafua hali ya hewa kwa kupotosha umma....mnajuwa huyu jamaa alimalizana vipi na Simba?
 
Ama kweli tenda wema nenda zako, na Fraga alitenda wema kaenda zake, na sasa anahangaika kujitibu yeye na familia yake huku club ya Simba ikiwa imemtelekeza, kwa kweli hii ndo tabia ya Wahindi kutumikisha watu ikitokea shida kwa mfanya kazi Mhindi huwa hana time tena. Pole Fraga

View attachment 1640558

Nadhani wameachana kiungwana kwani mkataba wake ulikuwa uimalizike Jun 30, 2021
 
Back
Top Bottom