Uchaguzi 2020 Kitendo cha Tundu Lissu kukubalika Kanda ya Ziwa kwa kiwango hiki inaashiria nini?

Asante wa bongo kwa kuukataa ukabila.
 
Kwa kanda ya ziwa Tundu lisu huenda akaambulia kura kwa mashemeji zake tu pale mkoa wa mara.hao wasukuma na wahaya usiwapigie mahesabu kabisa
 
Mahela atamsave....!!
 
Mkuu unaongea kwa mahaba
 
Sina hakika sana lakini kwa maoni yangu kosa kubwa la JPM ni ama kutopenda USHAURI wa kitaalamu au Kujizungushia watu waimba mapambi

Sio kanda ya ziwa pekee, ni nchi nzima na jibu rahisi ni kwamba watu wana maumivu makubwa sana moyoni wanalilia ukombozi, uponyaji, sasa Sauti ya Lissu inajenga matumaini hayo, ni Nyota ya jaha! Na CCM na viongozi wake wajifunze kwamba ITIKADI ni IMANI, kamwe huwezi kuufuta kwa sheria kandamizi, ubabe na dhuluma, watu wataogopa, watanyamaza lakini hawatakuunga mkono na pindi wakipata upenyo watakupa pigo moja la nguvu, Pigo la Inkoskazi! Mobutu, Makaburu, Gadafi, Saddam Hussein nk ni mifano ambayo tumeishuhudia katika miongo hii 2 au 3 inayoisha sasa. Ushawishi ni bora kuliko Ukandamizaji na ubaradhuli usio na busara hata kidogo!
 
Hivi bao la mkono litawezekana mwaka huu ila ile sheria ya kunyima nakala za matokeo eti nakala zimekosekana je wapinzani wamelifanyia kazi? 'that is too technical if not sorted out'
 
Kapicha kameeditiwa weeee!

Chadema hata muhangaike vipi, Lisu haingii hata mara 10 kwenye mafuriko ya Slaa 2010 achilia mbali ya Liwasa 2015
Lakini nyomi zaidi ya Magufuli....!!
 
Mimi kuwa Nccr mageuzi sio sababu ya kutosema ukweli kwa manufaa ya taifa letu,uzalendo kwanza mambo ya vyama baadae. Kwa hiyo usijifariji kuwa Chadema ina uhai fanya tathimini uraiani utapata picha kamili.
 
Tusimshirikishe Mungu ktk chaguzi hisokuwa na Tume huru ya uru ya uchaguzi
 
Mimi kuwa Nccr mageuzi sio sababu ya kutosema ukweli kwa manufaa ya taifa letu,uzalendo kwanza mambo ya vyama baadae. Kwa hiyo usijifariji kuwa Chadema ina uhai fanya tathimini uraiani utapata picha kamili.

Sasa hivi ni wakati wa kampeni, mada zako nyingi zilipaswa zijikite kueneza hicho chama chako kitafanya nini, na sio kinyume chake. Au hicho chama chako hakina manufaa yoyote kwa taifa letu? Mtaa upi nifanye utafiti zaidi ya hraya yanayoonekana sasa? Hapa ndio ujue unafiki haulipi.
 
Acha hasira,kwani huoni Nccr wanafanya nini? Huoni mikakati yao? Huoni kampeni zao?
 
 
Dada na hii hapa chini mbona hujaileta?
 
Acha kudanganywa na wanasaccos angalia hapa alivyozomewa huko huko wanakosema amefunika. Kuna uongo mwingi sana humu.
Hahahahaha Kwa iyo hawa wahuni mliowapa hela ndo unatuletea hapa!!!
Yaani hata ivyo vibango wameshikishwa tu!! Ona wanavyoonekana wanacheka hawapo serious!

Alafu mkaandaa na camera kabisa za kuwachukua😂😂😂😂 kweli CCM mmeishiwa mwaka huu
 
ukisikia hoja ya nguvu ndo hii, yaan hauna hoja yoyote zaidi ya kulazimisha unachokiamini kiwe kweli. enewei kujipa moyo si mbaya ila ujue maneno hata kwenye kanga yapo. tunachotaka sisi ni uchaguzi huru uwazi na haki. kama kwel huyo jamaa yako atashinda bas ashinde kwa uhuru, haki uwazi na ukweli tutamshangilia; atakayechakachua aandae mapema kabisa ung'eng'e wa kwenda kujitetea the hegi. la sivyo atakoma kama ung'eng'e wake ni ule wa ze ze ze yu noo ze intapraranyua.
 
Amini usiamini watarudi na kauli ya "TUMEIBIWA KURA" wako kama wajinga tu

Siasa ni hesabu na hakuna chama hapa Afrika kinacho shinda mbinu za CCM ikifuatiwa na ZANU PF, ANC.

Zaidi ya yote wananchi hawa wameshajua wazi Magufuli ni jembe,macho na masikio vinaona na kusikia kile Rais anachofanya, leo hii aje mtu na kuanza kumponda nani atamuelewa?ni vile tu wanachi hawawezi kusimama jukwaani na wao wanadhani watu wakifika kwenye mikutano yao ni kama wameshinda na kumbe hakuna kitu

Mikoa mitano ya Mwanza,Tabora, Geita, Simiyu na Shinyanga JPM atashinda kwa 90% na ndiyo mikoa yenye watu wengi kuliko yote hapa Tanzania hasa huko vijijini ambako hawawaoni Chadema wala act

Vyama pinzani viko Twitter, Jamii foruma na youtube

Nani anakwenda twitter kujua Tundu Lisu kaongea nini

Tulioko mijini 85% tunajua Tundu Lisu ni mhaini wa nchi na tunamsikiliza,mwisho wa siku tunaenda kumpiga chini kwenye sanduku la kura

Mtu asiye tueleza atatufanyia nini,kazi yake ni wivu tu dhidi ya Magufuli na kutueleza kua alipigwa risasi, tunajua alipigwa risasi na hawezi kutulazimisha kua Serikali au Magufuli ndo alisababisha hayo

Kweni tutamuaminije kua hana maadui? Yeye ni MALAIKA?

Apite hivi[emoji117] atupishe tafadhari tuchague mpambanaji
 
ahahaaaa eti anamuonea wivu!!! kwa hiyo Lissu anamuonea wivu mzee wa ze ze ze ze ze yu nooo zeeee ze ze intaprengenyua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…