Kitendo cha viongozi wa CHADEMA kupuuza kushiriki kongamano la dini ni aibu na fedheha kwa chama chao

CHADEMA ni chama cha siasa na sio chama cha Kidini, sio lazima kuhudhuria
 
Je walipewa official invitation? Kama hapana ulitaka chama kijialike? Then hii tabia ya kutumia neno uzalendo pasipo hitajika achana nayo. Hata CCM kama hawajaalikwa kweny jambo flan wasipokwenda hatuwez kuwalaumu maana kujialikisha ni kama wanajipendekeza.
 

 
... kumuombea mwendazake??? Never on earth!
 
Una hakika walialikwa?
 
Mleta mada tumia akili yako kufikiri!
Kumshukuru Mungu, hivi kweli?
Walifungwa
walibambikiwa kesi
Marisasi
Kuporwa mali zao
Kudhalilishwa
Kuonewa
Kutukanwa
Kuporwa ushindi wao
Kupotea kwa baadhi ya watu!
Chadema sio wanafiki kama walivyo ccm.
 
CDM inataka national reconciliation (Tume huru ya maridhiano) - ndiyo dawa ya kutibu majeraha...hapa tunapoongea kuna viongozi na wanachama wa CDM zaidi ya 300 magelezani nchi nzima ikiwa ni zao la uchaguzi Mkuu uliopita..zote zikiwa kesi za kubambikiziwa...
Haya yote viongozi wa dini hawayaoni wao wanachokiona ni kutumika kutengeneza legacy ya Magufuli ya haraka haraka...

CDM waende kufanya nini kwenye kongamano hilo?? Nimesikitika sana kuwaona viongozi wa dini ninaowaheshimu kabisa wakiwa hapo kutumika kisiasa.
 
Mara CHADEMA vibaraka wa mabeberu, wanapenda ushoga, wanataka kuuza, sio wazalendo... mara mbona hatuwaona kwenye shughuli za "kitaifa".

MATAGA chagueni moja, msiwe vigeugeu.
 
Wewe ni walee wanaotafuta vyeo kwa rais mpya.Hutapata.
 
Lini umetoka jando?
 
Kongamano la kumuombea marehemu, duh wacha wafu wakazike wafu wenzao
 
nyie CCM akili zenu mwazijua wenyewe, Chadema iko makini sana, huyo shibuda ni muwakilishi wa vyama vya siasa nchini ikiwemo Chadema. Sasa mlitaka Jopo la ngazi ya juu Chadema waje kushiriki Uongo?pambaneni na hali zenu.
 
Chadema na yenyewe inao viongozi wao wa dini ambao huwa nao kwenye shida na raha.Askofu Mwamakula na Sheikh Ponda,ni viongozi wa dini wanaokuwa bega kwa bega na Chadema.Hao waliokuwa kwenye kongomano ni viongozi wa dini wa CCM!
 
Yaani humu jukwaani Kuna watu wanaakili za kushikiliwa, kwa mabaya yote Magufuli aliyowafanyia wapinzani bado wajipendekeze kwa lipi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…