Kitendo cha wachezaji wa yanga kumpiga refa hakikubaliki

kamati ya nidhamu ya TFF

Hiyo kamati ya nidhamu ndo ile inayoongozwa na Deogratias Lyato, ama ni nyengine??

Kama ndiyo hiyo, uamuzi kama huu ulitarajiwa tangu dakika ile ile ya mashambulizi kwa Refarii.

Ngoja tusubiri rufaa ya Yanga kwa kamati ya Tibaigana ndipo muone sarakasi za Tff. Mpira wetu unazidi kushuka kila kukicha kwa sababu ya ujinga wa viongozi wa soka, ujinga wa wachezaji na ujinga wa waamuzi.

Kama ingekuwa ulaya ama amerika, walioshiriki vurugu zile ungesikia wachezaji wamefungiwa mechi kati ya 5 hadi 8 pamoja na faini, na muamuzi naye anawekwa pembeni. Lakini hapa kwetu watu wanakurupuka tu kama walevi wa gongo na kumfungia mtu mwaka mmoja, kwa maana nyengine wanamtaka aache kucheza mpira na tafsiri yake ni kwamba wamesimamisha ajira yake kwa mwaka mzima, sasa sijui hiyo akili ya wapi?

Kwa aina ya viongozi tulio nao sasa tff, bora vijana wetu wajikite kwenye bongofleva ama bongo movies tu, tenga na wahuni wake wanaharibu soka letu huku watanzania tukiwaangalia.
 
viongoz wa mpira wababaishaj unamfungia mwaka 1? Ili iweje mfungie mechi 5 umkate fain hata ya milion 5
 
Okay, kwa hiyo Yanga wanakata rufaa kwa sababu tu kulikuwa na 'habari ilitoka' (bila kujali kutokea kwa nani?) kuwa refa alipewa pesa? Redcard, aliyopewa Haruna ni nyepesi kivipi? Wewe unadhani alipewa kuhusiana na kosa gani au kuvunja kanuni/sheria gani ya soka (hata katika huo wepesi wake)? Mambo haya yanaonaongozwa na sheria/kanuni, so unaposema nyepesi au nzito/inastahili redcard ama la ni lazima uongozwe na sheria/kanuni husika.

kama uliona cku ile haruna dk ya 6 alikua ana yelow kad,ya ajabu ajabu tu dk ya 15 ISRAEL anampga red katka mazingira tata so players wangefanyaje na walisha ckia refa kala hela?
 
kabla ya mech habari zilitoka kwamba ISRAEL MKOMO amepewa pesa na Azam fc ili awe upande wao hata redcard aliyopewa haruna naamini ni nyepesi kuliko zote duniani,so alichokua anafanya ISRAEL ni kuwatoa wachezaj wa yanga mchezon. Thats all
Mkuu hata habari zingezagaa kwamba wachezaji wa Yanga wamempiga refa bila kuwa na ushahidi wowote wasingepewa adhabu, kwa hiyo wewe unayetaka tuamini hizo tetesi zako peleka hizo taarifa Takukuru maana hiyo ni rushwa na naamini watazifanyia kazi na sio kulalama tu mbona refa hajaadhibiwa, aadhibiwe kwa kosa gani alilofanya?
 
tehe tehee adhabu sawa! lakini sikubaliani na mtu kufungiwa mwaka mzima huu ni zaidi ya masaburi! hivi hii kamati inajua imesitisha mzunguko wa uchumi kwa watu wangapi wanaotegemea kwa njia ningine kuajiriwa na posho ya mchezaji huyu moja kwa moja au siomoja kwamoja? mbaya zaidi wanapunguza mapato ya serikali na kwa kuwa kodi yake tunayoipata kwa manunuzi itatapungua sana!
 
Mkuu hata habari zingezagaa kwamba wachezaji wa Yanga wamempiga refa bila kuwa na ushahidi wowote wasingepewa adhabu, kwa hiyo wewe unayetaka tuamini hizo tetesi zako peleka hizo taarifa Takukuru maana hiyo ni rushwa na naamini watazifanyia kazi na sio kulalama tu mbona refa hajaadhibiwa, aadhibiwe kwa kosa gani alilofanya?

kosa lake alipewa hela na akapendelea azam
 
Okay, kwa hiyo Yanga wanakata rufaa kwa sababu tu kulikuwa na 'habari ilitoka' (bila kujali kutokea kwa nani?) kuwa refa alipewa pesa? Redcard, aliyopewa Haruna ni nyepesi kivipi? Wewe unadhani alipewa kuhusiana na kosa gani au kuvunja kanuni/sheria gani ya soka (hata katika huo wepesi wake)? Mambo haya yanaonaongozwa na sheria/kanuni, so unaposema nyepesi au nzito/inastahili redcard ama la ni lazima uongozwe na sheria/kanuni husika.

Pamoja na kwamba siungi mkono kitendo cha wachezaji kumshambulia mwamuzi lakini kadi nyekundu aliyopewa niyonzima haikustahili, mwamuzi angeweza kumuonya kwa mdomo tu na yakaisha, kwa kuangalia mazingira yaliyokuwepo ambapo niyonzima alikuwa angombania mpira na erasto nyoni na nyoni alioneka kumchezea ndivyo sivyo hadi mpira ulipotoka nje na refa hakutoa adhabu yoyote kwa nyoni.

Na kama refa angezingatia kwamba tayari nje ya uwanja kabla ya mchezo kulikuwa na taarifa kwamba amehongwa na azm ili kuwabeba basi alitakiwa kuwa na busara ya hali ya juu katika maamuzi kwani kutoa uamuzi wenye utata lazima ungesababisha sokomoko na ndicho kilichotokea. Na utaona baada ya kutoa redcards mbili na kupata makonde alibadilika na mara nyingi akawa anaongea na wachezaji kabla ya kufikia kutoa kadi, sasa utajiuliza kwanini hakutumia busara hiyo hiyo kabla ya kuanza kutoa kadi harakaharaka hadi kusababisha vurugu?

Ni vizuri waamuzi wetu wakajitahidi kujua uzito wa mechi wanazochezesha ili kutoonekana kwamba wanapendelea timu fulani kwakuwa ligi inaelekea mwishoni na lazima waamuzi wawe makini zaidi na viongozi wa tff wawe makini zaidi.
 
Mkuu hata habari zingezagaa kwamba wachezaji wa Yanga wamempiga refa bila kuwa na ushahidi wowote wasingepewa adhabu, kwa hiyo wewe unayetaka tuamini hizo tetesi zako peleka hizo taarifa Takukuru maana hiyo ni rushwa na naamini watazifanyia kazi na sio kulalama tu mbona refa hajaadhibiwa, aadhibiwe kwa kosa gani alilofanya?

Kwa mujibu wa kumbukumbu zako unaweza kunionyesha ufanisi wa takukuru katika kupambana na kuzuia rushwa??
 
Pamoja na kwamba siungi mkono kitendo cha wachezaji kumshambulia mwamuzi lakini kadi nyekundu aliyopewa niyonzima haikustahili, mwamuzi angeweza kumuonya kwa mdomo tu na yakaisha, kwa kuangalia mazingira yaliyokuwepo ambapo niyonzima alikuwa angombania mpira na erasto nyoni na nyoni alioneka kumchezea ndivyo sivyo hadi mpira ulipotoka nje na refa hakutoa adhabu yoyote kwa nyoni.

Na kama refa angezingatia kwamba tayari nje ya uwanja kabla ya mchezo kulikuwa na taarifa kwamba amehongwa na azm ili kuwabeba basi alitakiwa kuwa na busara ya hali ya juu katika maamuzi kwani kutoa uamuzi wenye utata lazima ungesababisha sokomoko na ndicho kilichotokea. Na utaona baada ya kutoa redcards mbili na kupata makonde alibadilika na mara nyingi akawa anaongea na wachezaji kabla ya kufikia kutoa kadi, sasa utajiuliza kwanini hakutumia busara hiyo hiyo kabla ya kuanza kutoa kadi harakaharaka hadi kusababisha vurugu?

Ni vizuri waamuzi wetu wakajitahidi kujua uzito wa mechi wanazochezesha ili kutoonekana kwamba wanapendelea timu fulani kwakuwa ligi inaelekea mwishoni na lazima waamuzi wawe makini zaidi na viongozi wa tff wawe makini zaidi.

kwa jinsi ulivyoeleza unaonyesha ulikua uwanjani,na yote uliyosema ni ukweli %
 
Kwa mujibu wa kumbukumbu zako unaweza kunionyesha ufanisi wa takukuru katika kupambana na kuzuia rushwa??

takukuru hawana ufanisi wowote na refa alipewa pesa na hawajafanya chochote zaidi ya kumsumbua ulimboka mwakingwe
 
Kwa mujibu wa kumbukumbu zako unaweza kunionyesha ufanisi wa takukuru katika kupambana na kuzuia rushwa??
Ndio taasisi tuliyonayo kisheria inayoshughulikia rushwa, swala la ufanisi mimi siwezi kujua, wewe huwezi kusikia tu mtaani huyu kafanya vile na wewe unaamini hadi unaacha kufikiri, wale ni kwa tanzania ni wachezaji wakubwa hawakupaswa kuchukua maamuzi waliyoyafanya, kumpiga mwamuzi ni kosa, Mputu alifanya kama hayo kwenye kombe la kagame alifungiwa, wachezaji lazima wajifunze na wawe na lazima wabebe mzigo kwa vitendo vyao.
 
Acha habari za kusikia na kuzi'publish with confidence "eti walimpiga mtoto hadi akafariki" mtoto wa nani mkeo? ukiitwa leo Polisi ukasaidie Polisi katika hilo suala utaenda? jamani Watanzania tusiwe tunapenda kuropokaropoka bila mpangilio maalum,tutaumia!
 
Tutegee msimu huu ubingwa uende Simba or Azam!
 
Back
Top Bottom