OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 53,868
- 121,001
Jana nilipata wasaa wa kumuona Waziri Simbachawene katika shuguli za kiserikali. Katika kutupia macho dress code yake nibaini amepachika nembo katika suti yake. Kusogeza zaidi nikabaini haikuwa nembo ya taifa bali ni picha ya Samia.
Wakuu tumefika huku? Sikumbuki kama tumewahi kufika huku kabla. Hata walioanzisha uchawa hawakudhamiria kufika kiwango hiki. Hiki ni kiwango kikubwa kabisa cha kukosa uzalendo na nchi.