Mkirua
JF-Expert Member
- Sep 9, 2010
- 5,647
- 2,505
Mkirua asante ila tunarudi pale pale kwamba kama ni utamaduni unaenda ukibadilika na muda...yani nao unaenda na wakati.Hivyo basi huu nao umeenza kujiingiza kwenye utamaduni wetu...hata kama sio wa Kitanzania bali ni wa kundi fulani ndani ya Tanzania ...kama ambavyo mila na tamaduni za baadhi ya makabila zikivyo. Kwasababu tu baadhi ya mila na tamaduni za makabila mengine hazinihusu mimi siwezi kukataa kwamba nazo ni sehemu ya utamaduni wetu japo sio taifa zima linazozikubali na kuzifuata.
Hivyo hivyo kwa hawa watu...ndio maana siku hizi hata nguo wanaweza vaa vile wanavyopenda..kutembea tofauti na inavyoaminika mwanaume anatakiwa atembee...kuongea kwa madaha ya kike n.k mbele za watu...mitaani na hata majumbani.
Inawezekana wakawa hawakubaliki kwa asilimia kubwa ya Watanzania ila wapo watu wanaowakubali...na wao kama kundi wameufanya huu utamaduni kua wao.Kadiri kundi litakavyoongezeka ndivyo na utamaduni wao utavyoshika kasi ya kua kwenyr chati sawa na tamaduni zetu nyingine.
Uko sahihi kwa kiasi kikubwa Lizzy. Utamaduni umegawanyika katika makundi mengi na kila kabila and some times ukoo wana utamaduni ambao in a way unatofautiana na mwingine na actually ndio sababu ya tofauti zetu.... Pengine Lugha yangu na baadhi ya mila zangu na eneo ninalotoka ndivyo vinavyonifanya niitwe/nijiite Mkirua na wewe "Mmachame" a.ka. Mpalestina.. (a joke plz).
Katika Level ya Taifa si rahisi kuwa na vitu vingi... Mkusanyiko wa yale yoote tunayokubaliana nayo ndio msingi wa utamaduni wa Taifa..Mathalan lugha ya Kiswahili ni kielelezo mojawapo.
Tuje kwenye utamaduni wa mashoga sasa yaani kuongezeka kwa hao watu wanaowaunga mkono then ikawa part and parcel ya huo utamaduni.... Mungu apitishe mbali ... Think of a situation una kaka yako unayemuheshimu sana mathalan ndo kaka pekee nyumbanni then siku ukakuta ameshikishwa ukuta..... Huku tuendako nakubaliana na wewe kwa kizazi tulicho nacho na kasi ya kuiga mambo ya wazungu... uvivu wa kujishughulisha... maendeleo ya teknolojia ... Muingiliano wa watu though Globalization..... huenda Tanzania nayo ikaangukia kwenye "utamaduni huo.".... Mungu Ibariki Tanzania...