Kitenge ana shughuli gani Marekani?

[emoji38] [emoji38] [emoji38] Ndugu yangu yani naonaga hizo ni tabia za wakina dada zetu, sisi wanaume hayo mambo ya nini sasa, yani huwa inakera watu wenye hiyo tabia huwa kwenye whatsap ninawa mute
Wewe maisha mafupi haya. Kama nafsi yake inasuuzika wacha afanye. Ni njia mojawapo ya kuepusha nafsi na misongo ya mawazo isiyohitajika.
 
Sema nimegundua Kitenge hizo safari huwa zinaambatana na matangazo ya biashara bidhaa mbalimbali
 
Sema aliomba ukamkandamize
 
We ni mshambaaa sana kama huna kazi tulia wenye kazi zao waache wafanye...dunia ni kijiji kwaiyo usiwe na mawazo ya kindeziii....we mkudaa
 
Mkuu tafuta kwanza maendeleo ya ndugu zako huko Sigimbi, mambo ya Kitenge wala hayawezi kukusaidia lolote.
 
Ana shaba wake huko...miaka ya nyuma ilivuma sana...
 
Kitenge ni mwakilishi wa chapa mbalimbali hapa nchini na anaenda nje kuzitangaza na ndio maana picha zake anakuwa amepiga akiwa ameshika baadhi ya chapa{brands} anazoziwakilisha, kila mtu ana njia zake za kupata mkate wa kila siku kwa hiyo kuuliza kuwa kitenge anaenda kufanya nini huko Marekani ni ujuha mwenzenu anatengeneza pesa na kitenge ni mjanja kila anapoenda ana network ya Watanzania na nina wasiwasi kuwa hata kufikia hafikii kwenye mahoteli bali kwa marafiki zake. WaTz tumekuwa wajinga na umbeya wa kutaka kujua huyu anafanya nini,sijui inatusaidia nini, mbona watu wengi wamefanya Marekani kama Kibaha.Kuna wakati nae Ali Choki alikuwa akienda uingereza utadhani anaenda Kisarawe,yote ni sehemu ya maisha.
 
Ni haki yake kusafiri anakotaka na kuruhusiwa kwa hati yake na visa.

Ila Marekani miji mingi kuna Covid-19 sana, hata wakazi wenyewe tumejifungia majumbani mwetu. Hapo Atlanta Georgia alipotoka palikuwa na wimbi la Covid-19 kubwa sana.

Hivyo ninaposikia mtu anakuja Marekani, kama si safari ya lazima kindakindaki, inaweza kumhatarisha bila ulazima.
 
Mbona ni mara nyingi tu huwa anasafiri mara zingine na mtoto wake
Tangu nianze fatilia nadhNi hii ni safati yake yanne kama sio ya 3 huko marekani akitembelea states mbalimbali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…