KERO Kitengo cha Ardhi – Halmashauri ya Jiji la Dodoma kuna baadhi za huduma hazijawekwa kwenye mpangilio mzuri

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Naomba Kitengo cha Ardhi katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma kiboreshwe na watumishi wake watekeleze majukumu kwa weledi na uwazi.

Kwa baadhi ya viwanja vinavyouzwa kupitia TAUSI, taarifa muhimu kama mpangilio wa kufuatilia plan number na taarifa nyingine hazijawekwa vizuri kwenye mfumo. Hali hii inalazimu wananchi kufuatilia mara kwa mara na kusubiri kwa muda mrefu bila kupata majibu ya wazi.

Pia, kuna baadhi ya watumishi huomba username na password za waombaji ili kuingia kwenye mfumo na kuangalia hatua ya maombi. Hali hii inaibua maswali kuhusu usalama wa taarifa na uwazi wa mfumo.

Tunaomba Waziri mwenye dhamana na mamlaka husika kuangalia changamoto hizi, kuboresha mfumo na kuhakikisha kila mtumishi anayeshughulikia muamala anaonekana kwa jina lake badala ya kutumia jina la jumla la “Staff”, ili kuwepo uwajibikaji na kuzuia mianya ya rushwa.
 
Kweli,tunapoteza muda sana, Mara kiwanja Kuna Mtu amekiomba ,wakati unanyalaka zaote muhimu,kuvunjwa CDA, mambo ni zaidi ya CDA!
 
Back
Top Bottom