Kiti cha plastiki chakatisha maisha ya Kijana Steven Mbomambuzi, Moshi

Kiti cha plastiki chakatisha maisha ya Kijana Steven Mbomambuzi, Moshi

Ndagullachrles

JF-Expert Member
Joined
Jun 20, 2023
Posts
256
Reaction score
259
IMG-20260914-WA0304.jpg


Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro linachunguza tukio la mauaji ya kijana Steven Karakira Kaaya, (24), Mkazi wa Mtaa wa Boma Mbuzi, Wilaya ya Moshi,

Steven alifariki Dunia kutokana na majeraha aliyoyapata baada ya kushambuliwa na watu mbalimbali kwa tuhuma za kuhusika na wizi wa kiti cha plastiki.

Taarifa ya jeshi la polisi mkoani Kilimanjaro iliyotolewa kupitia kamanda wake (SACP),Simon Maigwa imeeleza kuwa tukio hilo limetokea Septemba 13, 2026, majira ya saa 11:00 jioni, katika eneo la Mtaa wa Spencorn, Kata ya Bomambuzi, Wilaya ya Moshi, Mkoa wa Kilimanjaro.

Inadaiwa kuwa, wakati wa tukio hilo, kijana huyo alishambuliwa katika sehemu mbalimbali za mwili wake kwa kutumia kitu butu na watu ambao majina yao yanahifadhiwa kwa sababu za kiuchunguzi ambapo hali yake ilizidi kuwa mbaya na hatimaye alifariki dunia.

Kufuatia tukio hilo, Jeshi la Polisi linamshikilia mtuhumiwa mmoja kwa mahojiano zaidi, huku uchunguzi ukiendelea ili kuwabaini na kuwakamata watu wengine wote watakaobainika kuhusika na tukio hilo.

IMG-20260914-WA0277.jpg


Aidha, baada ya tukio la mauaji kutokea, baadhi ya wananchi walijichukulia sheria mkononi kwa kufanya vurugu na kusababisha uharibifu wa mali, ikiwemo kuchoma moto gari aina ya Mitsubishi Centa lenye namba za usajili T.119 ATV kwa madai kwamba mmoja wa watuhumiwa wa tukio hilo la mauaji anatoka katika familia ya mmiliki wa gari hilo.

Vilevile, baadhi ya mali zilizokuwa ndani ya chumba cha duka linalomilikiwa na Thelesia Omary Nyambuleki Mwikoma ziliharibiwa katika vurugu hizo.

Wito kwa wananchi

Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro linawataka wananchi kutokujichukulia sheria mkononi, bali kutoa taarifa kwa vyombo vya dola pale wanapobaini au kushuku kuwepo kwa vitendo vya uhalifu ili hatua stahiki za kisheria zichukuliwe.

Chanzo na mazingira halisi ya tukio hili bado vinaendelea kuchunguzwa kwa kushirikiana na taasisi na mamlaka nyingine zinazohusika na uchunguzi utakapokamilika, hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya watu wote watakaobainika kuhusika na tukio la mauaji, vurugu na uharibifu wa mali.

IMG-20260914-WA0301.jpg


Chini picha ya marehemu Steven

Picha ya gari lililochomwa moto

Picha ya afande RPC (SACP),Simon Maigwa

IMG-20260914-WA0303.jpg
 

Attachments

  • IMG-20260914-WA0300.jpg
    IMG-20260914-WA0300.jpg
    39.8 KB · Views: 13
Kifo uwa kinakuja kikauzu sana aisee...kuna dogo mbeya katoka kulewa kakosea njia kaingia uhani kwa watu kapigwa mpaka kifo.

May all beings attain enlightenment.

Hivi vifo vinaonesha jamii haijali maisha ya mtu.

Mtu kalewa kapotea njia, anauawa.

Mtu ana matatizo ya akili kakutwa anatembea bila nguo, anauawa.

Bodaboda zinachinja watu kama kuku, hakuna anayejali.

Ni dalili ya jamii iliyojaa ujinga, umasikini na kutojali maisha ya mtu.
 
Nchi hii kwa sasa inahitaji sana utawala utakaojali na kuthamini sana uhai wa binadamu, maana hali ilivyo kwa sasa, baada ya kywapata watawala wauaji, ni kuwa uhai wa mwanadamu, umekuwa hauna thamani. Hali hii ikiachwa iendelee kama ilivyo, huko mbeleni nchi hii itakuja kutambulika rami Duniani kuwa ni nchi inayokaliwa na viumbe wanaofanana na wanadamu, lakini hawajulikani ni viumbe gani!!
 
May all beings attain enlightenment.

Hivi vifo vinaonesha jamii haijali maisha ya mtu.

Mtu kalewa kapotea njia, anauawa.

Mtu ana matatizo ya akili kakutwa anatembea bila nguo, anauawa.

Bodaboda zinachinja watu kama kuku, hakuna anayejali.

Ni dalili ya jamii iliyojaa ujinga, umasikini na kutojali maisha ya mtu.
Kabisa..ni jamii ambayo hai reason linapotokea jambo, ustaarabu upo mbali sana!
 
Back
Top Bottom