butron
JF-Expert Member
- Jun 3, 2013
- 5,640
- 7,943
Soma vizuri hoja ya Kitila Mkumbo pamoja na upuuzi wake lakini kaongea ukweli!Kazi ya wapinzani ni kukosoa, na serikali kazi yake ni kufanyia kazi mapungufu wanayooneshwa na wapinzani, wapinzani wakiifanya hii kazi yao kwa usahihi, wataaminiwa na wananchi hiyo inakuwa tiketi kwao kushinda uchaguzi popote.
Wewe na Kitila mnaamini wapinzani hawawezi kushinda uchaguzi sio kwasababu ya kazi wanayofanya ya kukosoa, mnaamini hawawezi kushinda uchaguzi kwasababu mmezoea kuishi kwenye mazingira yasiyo na usawa kati ya chama tawala na upinzani.
Simply mmezoea kuishi kwenye tatizo mpaka sasa mmelizoea, mmeligeuza kuwa ndio sehemu ya maisha.
Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Ata Simba na Yanga wanafungana baada ya mmoja kumzidi mwenzake ufundi!
Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app