Kitila Mkumbo: Hakuna chama chochote cha siasa Duniani kimeshinda uchaguzi kwa kuwa ni bingwa wa kukosoa

Kitila Mkumbo: Hakuna chama chochote cha siasa Duniani kimeshinda uchaguzi kwa kuwa ni bingwa wa kukosoa

Kazi ya wapinzani ni kukosoa, na serikali kazi yake ni kufanyia kazi mapungufu wanayooneshwa na wapinzani, wapinzani wakiifanya hii kazi yao kwa usahihi, wataaminiwa na wananchi hiyo inakuwa tiketi kwao kushinda uchaguzi popote.

Wewe na Kitila mnaamini wapinzani hawawezi kushinda uchaguzi sio kwasababu ya kazi wanayofanya ya kukosoa, mnaamini hawawezi kushinda uchaguzi kwasababu mmezoea kuishi kwenye mazingira yasiyo na usawa kati ya chama tawala na upinzani.

Simply mmezoea kuishi kwenye tatizo mpaka sasa mmelizoea, mmeligeuza kuwa ndio sehemu ya maisha.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Soma vizuri hoja ya Kitila Mkumbo pamoja na upuuzi wake lakini kaongea ukweli!
Ata Simba na Yanga wanafungana baada ya mmoja kumzidi mwenzake ufundi!

Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
 
"Ukisoma literature utaona kwamba hakuna chama chochote cha siasa duniani ambacho kimeshinda uchaguzi kwa kuwa tu kimekuwa ni bingwa wa kukosoa.

"Chama kinashinda uchaguzi kwa kuwa kimeweka sera mbadala na kikaonekana, kina safu mbadala ya uongozi, kuwa na mikakati mbadala ya ya kutatua changamoto za wananchi na kuonesha uzoefu katika kutatua changamoto za wananchi." - Prof. Kitila Mkumbo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji

Jambo TV
amegonga kweli haswaaaaa
 
Hii ni principle pia kwenye maisha.... Blaming and complaining doesnt solve problems.

Wanaojiita wapunzani tanzania ni wakosoaji badala ya kuwa wana preach solutions zaidi.

Wakosoe ila pia watoe na solutions
wapinzani watoe ushauri gani kwenye ripoti ya cag na mkataba wa bandari
 
Hii ni principle pia kwenye maisha.... Blaming and complaining doesnt solve problems.

Wanaojiita wapunzani tanzania ni wakosoaji badala ya kuwa wana preach solutions zaidi.

Wakosoe ila pia watoe na solutions
Hakuna mazingira ya wapinzani kuonyesha wanachoweza kufanya ili kuonyesha wawezacho. Nakumbuka wakati fulani Mzee Ndesburo RIP, akiwa mbunge alipendekeza elimu iwe bure kwenye manispaa ya Moshi, serekali ilimgomea na kusema haiwezekani. Baadae bila aibu ccm wakapora ajenda ile!

Kuna wakati cdm walisema watashusha bei ya vifaa vya ujenzi ili kuondoa nyumba za tembe, ccm walipinga Hadi kumleta mmilki wa kiwanda Cha cement kukanusha kuwa bei haiwezi kushuka. Huo ni mfano kuwa wapinzani wanaonekana wakati ww kukosoa tu, lakini wakitaka kufanya jambo kwenye jamii hawaruhusiwi. Ni mara moja au mbili tumeoano wakuu wa taasisi kadhaa wakigomea kupokea michango ya wapinzani kwenye jamii? Hivi mnadhani hatujui utendaji ukoje kwenye nchi hii?
 
Pamoja na ujinga wake ila kaongea ukweli!

Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
Kaongea ukweli, ila yeye mwenyewe anakiri kuwa hapa nchini hatushindanishi sera! Mshindi anatangazwa nje ya maamuzi halisi ya box la kura, bali anatamgazwa mshindi kwa maagizo na utashi wa kikundi Cha ccm kijiitacho system. Ingekuwa mshindi anapatikana kwa ubora wa sera, leo hii ccm isingekuwa madarakani. Wala tusingekuwa na chama kimoja madarakani muda wote.
 
"Ukisoma literature utaona kwamba hakuna chama chochote cha siasa duniani ambacho kimeshinda uchaguzi kwa kuwa tu kimekuwa ni bingwa wa kukosoa.

"Chama kinashinda uchaguzi kwa kuwa kimeweka sera mbadala na kikaonekana, kina safu mbadala ya uongozi, kuwa na mikakati mbadala ya ya kutatua changamoto za wananchi na kuonesha uzoefu katika kutatua changamoto za wananchi." - Prof. Kitila Mkumbo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji

Jambo TV
Vyama vya upinzani huko duniani huwa vinashinda kwa kuwa kuna ulingo sawa wa kufanya siasa na huwa hakuna Chama Dola !!
 
Back
Top Bottom