Kitila Mkumbo na Issa Shivji

Kitila Mkumbo na Issa Shivji

siungi mkono hoja kwa nini kupoteza muda na hela hizo bilioni ulizotaja itakuwa dowans nyingine kama sio kagoda kengine,kama ulifuatilia mjadala wa jmosi pale nkrumah kuna mchangiaji mmoja alisema serikali sio sikivu tutaandaa semina, warsha ,kongamano ,kigoda,mikutano,mbongi nk lakini hiyo yote haitasaidia ,cha msingi tunajua tunataka nini basi serikali ikileta ujanja ni kuandamana tu wacha wafyatue risasi tufe kwa ajili ya watoto na wajukuu zetu,kilichotokea nkruma juzi kimeshasahulika zamani lakini kilichotokea arusha tarehe 5 january hakitasahulika kamwe kimeishaingia wenye kumbukumbu za dunia so solution na peples power,
nawasilisha

Mkuu concern yako inaeleweka na ni kweli kuwa yaliyotokea Arusha siku ya tarehe 05/01/2011 hayatakaa kamwe yasahaulike katika mioyo na akili za Watanzania. Pamoja na hoja ulizozitoa, ni muhimu sana kuendeleza midahalo nchini nzima na naamini Serikali itakuwa haina njia bali kukubali kile ambacho Watanzania tunataka. Kwa upande mwingine hii ni fursa ya kipekee kwa UDASA ambayo inabidi waitumie ipasavyo kwa ajili ya Watanzania na taifa letu kwa ujumla. Pia naamini UDASA hawatakuwa na pingamizi kupokea michango ya fedha toka kwa Watanzania. Hivi Mkuu shilingi 25 unaweza kuifanyia nini kwa wiki maanake hata pipi huwezi kununua. Mkuu usikate tamaa lazima kieleweke tu CCM na Serikali hawana njia.
 
Naunga mkono hoja,ila vyombo binafsi vya habari ndio vipewe malipo ila TBC walirushe matangazo BURE!
 
Naunga mkono hoja,ila vyombo binafsi vya habari ndio vipewe malipo ila TBC walirushe matangazo BURE!

Mkuu,

Kutokana na umuhimu wa jambo hili ni muhimu sana vyombo binafsi navyo vikajitolea kama mchango wao katika kufanikisha suala hili ambalo ni muhimu sana kwa ajili ya maendeleo ya taifa letu. Juzi ITV walirusha bure mdahalo mzima kwa zaidi ya saa nne. Kwahiyo itapendeza zaidi kama vyombo vingine vya binafsi vikaiga mfano huu mzuri wa ITV.
 
Naunga mkono hoja vilevile iangaliwe njia ya kuproduce CD na DVD za kongamano hilo ili ziweze kusambazwa kwa wananchi wengi.Kwa njia hii wengi watapata uelewa na kushiriki kwenye mchakato kwa umakini zaidi.
 
Naunga mkono hoja vilevile iangaliwe njia ya kuproduce CD na DVD za kongamano hilo ili ziweze kusambazwa kwa wananchi wengi.Kwa njia hii wengi watapata uelewa na kushiriki kwenye mchakato kwa umakini zaidi.

Mkuu, wazo lako kuhusu CD na DVD ni nzuri na ninaamini wahusika watalifanyia kazi. Naamini itawezekana kuipatia kila shule na taasisi nyingine za elimu angalau CD/DVD moja.
 
ni hoja nzuri. na pia kwa jambo hili kama udasa mkiwa approach donors ni rahisi kupata fedha za kutosha kueneza elimu kwa watz

Naunga mkono hoja ila donors wawe watanzania mimi nikiwa mmoja wao. Donors wazungu hapana maana wao ni sehemu ya misiba inayotupata kila siku.
 
Naunga mkono hoja na nitachangia. Binafsi nilihudhuria pale UDSM na nilinufaika sana. So, I would wish others to benefit the very same way as I did on the 15th of January, 2011 at Nkurumah Hall.
 
Realman unena la maana maana hata Babu Shivji hataki kusikia foreign donors. Nimefanya kazi na huyu mzee ni mzalendo na mwanazuoni na mwanasiasa wa ukweli. Na ndiyo maana alihimiza kuwa watu wapewe elimu kwanza kabla hata ya kutoa maoni ya maudhui ya katiba. Siyo wafikirishwe kuwa katiba ni mbovu inapaswa kuwa hivi ama vile Rwaitama anasema tusiwasemee watu wao wafundishwe wajisemee wenyewe kulingana na mahitaji ya kila mtu na hivyo wazo la mtoa mada ni la muhimu sana ili kila mtanzania apate ujumbe na hilo naamini Shivji yupo tayari mfano mnaofuatilia jana alikuwa kwenye daladala akiendeleza libeneke kwa umma. Mambo ya maandamano au mauji hayatawezaleta katiba ya wananchi yataleta katiba ya CCM, CHADEMA, CUF, NCCR nk. tuwe makini sana na mmamuzi yetu na ndiyo maana waliyomsikiliza mzee shivji na Ulimwengu vyema utagindua kuwa wanawasihi watu wasikurupuke kutengeneza katiba kwa nia fulani ya binafsi maana itakuwa ya muda bila tija.
 
kila la kheri, mtakapo kuwa mnawazika watoto wa masikini ambao ndio huwa chambo mnapoandamana kama ilivyokuwa arusha, mimi nitakuwa home na watoto wangu tunaangalia cartoon ya wacky races, mkipata hicho mnachokitafuta kama kinafaida na mimi nitakuwa mstari wa mbele katika kufaidi.

na wewe pia na wanao tutawazika! Kwani waoga siku zote ndio waadhirika wakubwa katika mapambano!
 
siungi mkono, serikali itenge na kutumia rasilimali zetu, hakuna haja ya kuwabebesha mzigo wa tz wachache au labda serikali iwalipe hawa walimu kama konsaltants.

katiba si ya serikali,kushirikisha wananchi ndio jambo la kushikia bango.watu wakiweza kuchangia itasaidia kuonyesha muitikio wa wananchi katika swala hili la katiba.
 
Naunga mkono hoja ila donors wawe watanzania mimi nikiwa mmoja wao. Donors wazungu hapana maana wao ni sehemu ya misiba inayotupata kila siku.

Umenena vizuri na pia nakubaliana na aliyoyasema Mabulangati hapo juu. Hatuhitaji hata shilingi moja ya mzungu katika hili. Natumaini UDASA hawatatuangusha.
 
mambo matatu waliyosema wana jf wengine ni ya msingi sana! Moja kuwaepuka wahisani ni mkakati mzuri wa kuondokana na fikra tegemezi hasa kwenye jambo la utaifa wetu! Pili wananchi washirikishwe iwezekanavyo mana katiba ni yao! Tatu, matumizi ya viyombo vya habari ni muhimu sana hasa redio maana zinawafikia watu wengi zaidi nchini, ikichanganywa na tv, magazeti, nk tutafanya jambo zuri kwa TAIFA LETU!
 
Prof, shivji na Kitila.

mawazo yao ni ya msingi sana juu ya katiba mpya. pia nawapongeza Raia mwema gazeti kwa kuichapisha katiba ili watanzania walio wengi wapate angalau kuisoma tukiachilia mbali kuielewa.

Angalizo lan gu ni kwa Rais na wadau wengine ni kuwa kama nchakato wa katiba mpya hautakuwa makini katiba hiyo itakayoundwa italeta mzozo zaidi.


BY sandefs@yahoo.com
 
mambo matatu waliyosema wana jf wengine ni ya msingi sana! Moja kuwaepuka wahisani ni mkakati mzuri wa kuondokana na fikra tegemezi hasa kwenye jambo la utaifa wetu! Pili wananchi washirikishwe iwezekanavyo mana katiba ni yao! Tatu, matumizi ya viyombo vya habari ni muhimu sana hasa redio maana zinawafikia watu wengi zaidi nchini, ikichanganywa na tv, magazeti, nk tutafanya jambo zuri kwa TAIFA
LETU!

Ni kweli kwiifoenda Redio ni muhimu sana katika kuwafikia Watanzania wengi zaidi.
 
Back
Top Bottom