Amanikwenu
Senior Member
- Dec 1, 2009
- 187
- 0
- Thread starter
- #21
siungi mkono hoja kwa nini kupoteza muda na hela hizo bilioni ulizotaja itakuwa dowans nyingine kama sio kagoda kengine,kama ulifuatilia mjadala wa jmosi pale nkrumah kuna mchangiaji mmoja alisema serikali sio sikivu tutaandaa semina, warsha ,kongamano ,kigoda,mikutano,mbongi nk lakini hiyo yote haitasaidia ,cha msingi tunajua tunataka nini basi serikali ikileta ujanja ni kuandamana tu wacha wafyatue risasi tufe kwa ajili ya watoto na wajukuu zetu,kilichotokea nkruma juzi kimeshasahulika zamani lakini kilichotokea arusha tarehe 5 january hakitasahulika kamwe kimeishaingia wenye kumbukumbu za dunia so solution na peples power,
nawasilisha
Mkuu concern yako inaeleweka na ni kweli kuwa yaliyotokea Arusha siku ya tarehe 05/01/2011 hayatakaa kamwe yasahaulike katika mioyo na akili za Watanzania. Pamoja na hoja ulizozitoa, ni muhimu sana kuendeleza midahalo nchini nzima na naamini Serikali itakuwa haina njia bali kukubali kile ambacho Watanzania tunataka. Kwa upande mwingine hii ni fursa ya kipekee kwa UDASA ambayo inabidi waitumie ipasavyo kwa ajili ya Watanzania na taifa letu kwa ujumla. Pia naamini UDASA hawatakuwa na pingamizi kupokea michango ya fedha toka kwa Watanzania. Hivi Mkuu shilingi 25 unaweza kuifanyia nini kwa wiki maanake hata pipi huwezi kununua. Mkuu usikate tamaa lazima kieleweke tu CCM na Serikali hawana njia.