Kitila Mkumbo: Soko la kimataifa EACLC Ubungo watakaopangishwa asilimia 95 ni watanzania

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,186
Reaction score
4,940
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Profesa Kitila Mkumbo, amesema kuwa serikali inaendelea kuvutia wawekezaji kutoka mataifa mbalimbali na ndani ya Tanzania, huku akisisitiza kuwa Watanzania ndio wanaofaidika zaidi na uwekezaji huo.

Profesa Kitila ameyasema hayo alipoungana na Kituo cha Biashara na Usafirishaji Afrika Mashariki (EACLC - East Africa Commercial and Logistic Centre) pamoja na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Wilaya ya Ubungo katika hafla maalumu ya Iftar na dua kwa ajili ya kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan. Hafla hiyo imefanyika Ijumaa jioni katika eneo la Kituo hicho kilichojengwa Ubungo, Dar es Salaam, kwenye eneo la zamani la Stendi ya Mabasi ya Ubungo.

Akiendelea kufafanua kuhusu uwekezaji wa EACLC Profesa Kitila amesema kuwa kituo hicho kina maduka 2060, na serikali iliweka masharti kuwa asilimia 95 ya wapangaji wake wawe Watanzania. Hata hivyo, amesema kuwa hadi sasa karibu asilimia 99 ya waliochukua maduka hayo ni Watanzania.

Ameongeza kuwa maduka makubwa ya kimataifa yanatarajiwa kufunguliwa ndani ya kituo hicho, na kwamba raia wa mataifa mbalimbali, badala ya kusafiri hadi China kwa ajili ya biashara, watakuja moja kwa moja EACLC, akieleza kuwa hatua hiyo ni kubwa katika kubadilisha mandhari ya biashara na uwekezaji nchini.

Profesa Kitila amesisitiza kuwa serikali iko makini kuhakikisha kuwa masilahi ya wananchi wa Tanzania yanapewa kipaumbele, akisisitiza kuwa uongozi wa Rais Samia unajali masilahi ya wananchi wake. Pia ameeleza kuwa ni dhamira ya serikali kuendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji, jambo ambalo limezidi kuvutia wawekezaji wakubwa ndani na nje ya nchi.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa EACLC, Cathy Wang, amesema kuwa amefurahishwa na hafla hiyo ya Iftar, akieleza kuwa haikuhamasisha mshikamano wa kidini pekee bali pia maendeleo ya biashara na uwekezaji nchini Tanzania.

"Uwekezaji ni nguzo muhimu katika maendeleo ya taifa, na mchango wa serikali katika kuimarisha mazingira ya biashara unazidi kuleta mafanikio makubwa," amesema Cathy Wang.
 
Duuh sawa,kwa hiyo ndoto zangu za kwenda China ,zimefeli!
 
Hivi ni sifa kuwa mpangaji.viongozi wetu bure sijui huwa wanawaza nini kabla ya kuongea.kwa hilo duka hapo ubungo inamaanisha tutabaki kufanya biashara za reja reja tu.
 
Back
Top Bottom