Kitila Mkumbo: Tunataka kuona tunasafirisha betri za magari ya umeme na sio madini yake. Anadi umasikini utakuwa 0 mwaka 2050 nchini

Kitila Mkumbo: Tunataka kuona tunasafirisha betri za magari ya umeme na sio madini yake. Anadi umasikini utakuwa 0 mwaka 2050 nchini

Matendo yanaongea zaidi kuliko maneno.
Hatuoni hatua zozote za ujenzi wa hicho kiwanda zaidi ya mikataba tu ya makampuni ya uchimbaji ambayo huwezi kuyalimit once unapokuwa tayari umewapa leseni ya uchimbaji.

Huku mmeshachukua mikopo/ hela za watu .
 
Wakati akiongelea hali ya uchumi na mpango wa maendeleo bungeni leo Juni 13, waziri Kitila Mkumbo amesema wataendelea kuzingatia nafasi ya madini kukuza ujazo wa mauzo nje ya nchi na kuzingatia umuhimu wa madini ya kimkakati kutimiza azma ya dunia kuzalisha nishati safi na salama kwa mazingira.

Serikali imesema itaweka mazingira mahsusi kuvutia wawekezaji watakaokuwa tayari kujenga viwanda vitakavyoongeza thamani ya madini hayo nchini.

'Tunataka kuona tunasafirisha nje ya nchi betri za magari na sio madini yetu ya kimkakati. Tumesema wazi, wakati dunia inaelekea mwaka 2050 ikizungumzia kwa na 0 emission, tunataka kuona rasimali hizi zinatusaidia na sisi ifikapo mwaka 2050 tunakuwa 0 poverty' Alisema Kitila.
Ikiwa toka enzi na enzi walishauri hivyo na wasifanye , Leo itakuwaje tuwaamini.
Pili hizi ni Sera za Awamu ya Tano au Awamu ya sita.
 
Back
Top Bottom