Kitimoto kupatikana Zanzibar ni ishara ya uvumulivu

Kitimoto kupatikana Zanzibar ni ishara ya uvumulivu

Japo Zanziba ni sehemu ya Tanzania, inafahamika kuwa asilimia kubwa ya wakazi wake ni Waislamu. Na inafahamika kuwa nguruwe, au MBUZI KATOLIKI kama inavyoitwa na baadhi ya watu, ni wanyama haramu kwa Waislamu.

Lakini unajua hiyo mboga inapatikana hata Zanzibar? Kwa ambaye hajawahi kufika huko, anaweza asiamini. Hata mimi nilikuwa na mtazamo huo. Ulibadilika baada ya kushuhudia kwa macho yangu na kinywa changu.

Ilikuwa mara yangu ya kwanza kufika Zanzibar. Nilipoulizia gesti iliyopo sehemu tulivu, baada ya kutoridhishwa na zilizopo maeneo ya Darajani, niliambiwa niemde kwa BI JANETH, mahali wanakouza kitimoto. Ipo Mbwe, Unguja.

Nilitilia mashaka hayo maelezo, lakini nikaamua kujiridhisha. Hata baada ya kufika kwa BI JANETH, na kuulizia vyakula vinavyopatikana hapo, bado sikuamini nilipotajiwa mpaka kitimoto. Lakini nilipojionea mwenyewe kwa macho yangu na kinywa changu, sikuwa na sababu tena ya kuwa na mashaka, badala yake, nilibaki na mshangao. Niligundua kuwa Mzanzibar si kama nilivyokuwa nikiifahamu, kwa kuambiwa.

Sijui ilifika fikaje hapo kwenye hiyo lodge! Sijui kama nguruwe wanafugwa huko Zanzibar au wametolewa bara.

Lakini naamini Serikali na Raia wanafahamu kuwa kuna biashara kama hiyo huko Zanzibar. Kitendo cha kuruhusu watumiaji wa hiyo mboga kujinafasi bila kubughudhiwa, hata kama ni katika baadhi ya maeneo tu, kinaonesha wazi kuwa Wazanzibar ni watu waelewa na wavumulivu pia.

Wameonesha kwa vitendo kuwa japo wao (wengi wao) hawaitumii kitimoto, wanaheshimu Imani za wengine. Ndiyo maana hawajaweka ukwazo kwa wanaohitaji hiyo mboga. Huo ni ustaarabu wa hali ya juu!!!

Hongereni sana Wazanzibar!
Uvumilivu gani wakati walaji wakubwa ni Wazanzibari wenyewe? Tena pale inapotengenezwa pana lodge ambapo wale viongozi na watu maarufu wasiopenda kuonekana wanapoagiza watengenezewa kitimoto huweka na booking ya chumba kabisa ili walie vyumbani wasionekane?
Vijana wa kipemba na wakiarabu waliojizira wale huwa ndiyo wanailia palepale nje ( bar )
 
Hivi jina la mbuzi katoliki lilipatikanaje?
Nafikiri ni kwa sababu ilikuwa kati ya miradi pendwa ya Mashirika ya Kanisa Katoliki. Inasemekana Seminary nyingi za KATOLIKI zilikuwa na mradi wa ufugaji nguruwe.
 
Uvumilivu gani wakati walaji wakubwa ni Wazanzibari wenyewe? Tena pale inapotengenezwa pana lodge ambapo wale viongozi na watu maarufu wasiopenda kuonekana wanapoagiza watengenezewa kitimoto huweka na booking ya chumba kabisa ili walie vyumbani wasionekane?
Vijana wa kipemba na wakiarabu waliojizira wale huwa ndiyo wanailia palepale nje ( bar )
Aisee!!!
 
Back
Top Bottom