Ngongo
Platinum Member
- Sep 20, 2008
- 20,654
- 35,887
Weekend niliamua kutembelea viungo vya mitaa ya Mromboo.
Unapoitaja viungo vya mitaa ya Mromboo moja kwa moja akili inakimbilia ulaji wa Mbuzi choma.
Kwasababu zilizo nje ya uwezo wangu hasa hili gonjwa la gout nikaamua bora nitafune mbuzikatoliki.
Nikakatiza mitaa miwili mitatu nikakumbana na kijiwe safi kabisa.Nikaagiza pande zuuuri na ndizi na kachumbari ya ukweli.
Wakati nasubiri kaingia kijana wa makamo labda miaka 23 hadi 27 kavalia barakashia na kanzu kaikunja.Bila kupoteza muda kaagiza pande lake la uhakika.
Sote tumekaa tunasubiri mdudu baada ya dk 15 to 20 kila mmoja akawa anapambana na utamu wa mdudu wa taifa.
Ghafla wanaingia vijana kama wanne hivi wote wamepiga barakashia,kanzu na suruali fupi.Wote wakamvamia yule kijana aliyevalia barakashia na kuanza kumtandika bakora na kumchoma visu sehemu za mgongoni.Kipigo kiliendela kwa muda wa dk 10 to 15 huku wakitoa maneno makali Muislam gani unakula mdudu wa taifa tena umevaa kanzu na barakashia.
Niko pembeni nimetulia ladha ya mdudu siisikii tena maji yamekorogeka baada ya kumaliza kazi yao wakaondoka bila kumdhuru mtu yoyote.
Leo nimepita tena nikawauliza wahusika vipi ustadhi hali yake wakaniambia kalazwa Muriet hospital bado anapelekewa mdudu na taarifa zinadai akitoka atakuwa Mgalatia safi.
Ngongo kwasasa Kwa Mrombo.