Kitimoto ya sikuhizi nani kairoga? Harufu yake imepotelea wapi?

Ni aina ya nguruwe fulani wanafugwa siku hizi, hawana mafutafuta mengi kama ile mbegu ya zamani kubwa kubwa ndefu. Hawa nguruwe wa sasa hivi ni wadogodogo wafupi. Siku hizi si nyama tu hata mchele na mahindi imepoteza harufu nzuri na ladha kama zamani, ni mbegu mpya hizi
 
Hapo kwenye size ni kweli, nguruwe wa sikuhizi wadogo sana, miaka ile kile dude hilo miguu imejaa matope
 
Kitimoto kitamu sana!
 
Mwenyewe nlinotisi hili ila Kwa uchunguzi mfupi ni vile wanavyokula ,nlienda kaskazini juzi kati kuna sehemu bush wanaharufu tamu ajabu,ila Kwa Hawa wa kibongo wanaokula kiepe,harufu mtaiskia bombani
 
Ng'ombe wenyewe nao siku hizi hawana nyama tamu mpaka kuna mbunge juzi kati kalalamika kuwa ng'ombe wetu hawana nyama nzuri
 
Umeanza kula kitimoto huku unajitambua mwaka gn?

Kama ni 2000 kuja mbele basi hutoelewa hio harufu

Ile ngoma ilikua ikikaangwa nyumba hii inasikika within 1km radius


Mungu ameanza kuiharibu harufu ya kitimoto ili muache kula ila hamtaki kuelewa somo.
 
Ni almost kila kitu hakina ladha tena

Mchele
Enzi izo wali ukipikwa nyumbani hata kama haupo ukirud lazima ujue hapa leo pamepikwa wali na ukila ladha unaihisi Hadi vidoleni ila siku hzi ni kama tunakula wali jina Tu ila ladha hamna kitu

Nyama
Enzi izo nyama ya ng'ombe ni tam kweli kweli na hapo inakuwa imeungwa na kitunguu na nyanya tu ila ni kipindi nyama inapikwa kwa maji mara mbili ...ila siku hizi pamoja na kuongeza viungo vingi lakini ni kama unakula nini sijui

Mboga za majani
Yaani imenibidi niache kabisa kula mchicha siku hizi, maana nastaajabu mchicha umekuwa wa uchungu
Matembele nayo ni ivoivo
Yaan siku hizi unaweza ukala mboga ya majani na ukashindwa kuitambua ni mboga ya majani gani hadi uulize

So sad [emoji26] kwakweli
 
vyakula vingi vya siku hizi vitamins content ni kidogo sana, ukiangalia feeding formula nyingi ni wanga, protein na madini. Vyakula vya vitamins km mbogamboga, majani na baadhi jamii ya mizizi ni ngumu kupatikana kwa wafugaji wengi.

Hata kuku wa kienyeji ukimfungia na kumlisha km broiler, nyama yake hutapata ile ladha ya ukienyeji kama suala la vitamins halikuzingatiwa.

Kale kitimoto kijijini anayepewa majani utaona utofauti
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…