WomanOfSubstance
JF-Expert Member
- May 30, 2008
- 5,457
- 963
HEBU TUJULISHENI MLIOKO KIPAWA...mabomu ya machozi huko...ni aje wamemzuia mkuu wa nchi asipite?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Yeah,Kulikoni tena wakuu. Ni maswala ya upanuzi wa airport au ni nini?
Ngongo,Bila shaka ni masuala ya fidia.Wengi wanapinga kulipwa fidia kwa kutumia sheria ya zamani wakati tayari ipo sheria mpya.
Walioko uko tafadhali tupeni habari kamili
Great,HAli kidogo imetulia ila sie tulio jirani nao tumeyapata hayo machozi
Great,
Afadhali umetufahamisha walau kama hali imetulia. Ilikuwaje? Nani alikuwa anapiga mabomu hayo? Ili iweje? Kwanini wananchi watawanyishwe? Kwanini rais asiwasikilize kabla ya kuendelea na safari yake? Kipi muhimu kwake?
Great,
Afadhali umetufahamisha walau kama hali imetulia. Ilikuwaje? (Watu wamechoka)
Nani alikuwa anapiga mabomu hayo? (Wale jamaa wa "Ndio afande")
Kwanini wananchi watawanyishwe? (Mkuu anawahi matibabu)
Kwanini rais asiwasikilize kabla ya kuendelea na safari yake? Kipi muhimu kwake? (Afya yake kwanza)
Ahsante kwa taarifa mkuu BornTown.kwa hesabu za haraka haraka yamepigwa zaidi ya kumi tulikuwa tunawachungulia kwa dirishani tu vijana wa ukonga walivyokuwa wanakimbizana na wakazi hao waliogoma kulipwa pesa zao leo sababu kubwa ni huo mfumo wanaotaka kuutukia.
Ila kuna bango moja limenifurahisha linasema "HATUDANGANYIKI NA VIJISENTI VYENU"
lakini watalipwaje kwa sheria mpya wakati uamuzi umefanyika kwa sheria ya zamani? wenye kufahamu sheria nifafanulieni tafadhali...