Kitovu kutoka maji husababishwa na nini??

Kitovu kutoka maji husababishwa na nini??

MankaM

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2013
Posts
9,448
Reaction score
3,065
Habarini za masiku mengi wapendwa natumaini mko vizuri...

Madaktari na wadau wa hili jukwaa naombeni msaada wenj katika hili.....
Mwanangu anasumbuliwa na kitovu.. tatizo ni kwamba kinatoa maji ambapo huambatana na maumivu jaman mtoto anapata shida sana...... akianza kulia ndio kabisaaa maana kinakuwa kama kimetuna au kuvimba nahisi hii pia humuongezea maumivu ... tatizo hili huja na kupotea, mara ya mwisho kusumbuliwa na tatizo hili ilikuwa mwaka jana mwezi wa 11 na dawa ambayo tunaitumia ni Ampliclox huchanganywa na maji na kumdondoshea sehemu ya kitovu ambapo baada ya siku tatu kinakauka na anakuwa akiendelea vizuri ......
sasa hii hali imejirudia tena jana baada ya kwenda hosptali tukapewa dawa ile ile......

Wapendwa nahitaji kujua kwa undani tatizo hili la kitovu kwa watoto wadogo husababishwa na nini hasa?
Na Ipi ni dawa nzuri kuweza kufanya kitovu kikauke moja kwa moja?
Nini kinasababisha kitovu kisikauke???

maana kila mtu anaongea lake wengine wanahusisha na mambo ya kiimani sasa hapo ndio nachoka kabisaaaa. madaktar nipeni mwangaza katika hili
 
Bibie hujasema mtotowako anamiaka mingapi? uliwahi kumpeleka Hospitali gani? Je uliwahi kumpeleka hospitali ya muhimbili kuchekiwa?bibie MankaM

Hosptali alowahi kutibiwa ni K's hosptal. Marie stops na aghakhan mbeya mtoto ana miaka miwili na mwez mmoja
 
Last edited by a moderator:
Mwanao kitavu hakikukauka vizuri na kupona kabisa ushauri wangu nenda hospital kubwa watakifungua na kukifunga upya..usiafanye mzaaa katika hilo.pia jaribu kuepuka kuweka maji kwenye kitovu..
 
Hosptali alowahi kutibiwa ni K's hosptal. Marie stops na aghakhan mbeya mtoto ana miaka miwili na mwez mmoja
Tafuta Dawa mmoja inaitwa kwa jina hili habbat Sawda kipimo cha gramu 50 na ufuta mweupe gramu 50 uchanganye pamoja kisha uıwe unampatia kijiko kidogo ale hiyo dawa kutwa mara 3 asubuhi mchana na usiku kwa muda wa siku 7 kisha uje unipe feedback. Bibie MankaM Habbat swda inapatikana kwenye maduka ya dawa za kisunna Kariakoo mtaa wa Nyamwezi na Mkunguni kaulize utapata hapo. Unaweza kuitwanga kuwa unga na huo ufuta pia ukautwanga kuwa unga kisha ukachanganya pamoja. Na kumpakijiko kidogo kutwa mara 3 kwa siku 7 atapona inshallah.

attachment.php

Habbat Sawda Nyeusi na Ufuta Mweupe.
 
Attachments

  • black-white-sesame-seeds-small-bowl-isolated-overhead-view-36400200.jpg
    black-white-sesame-seeds-small-bowl-isolated-overhead-view-36400200.jpg
    146.6 KB · Views: 617
Mwanao kitavu hakikukauka vizuri na kupona kabisa ushauri wangu nenda hospital kubwa watakifungua na kukifunga upya..usiafanye mzaaa katika hilo.pia jaribu kuepuka kuweka maji kwenye kitovu..

Shukrani ndugu napata picha kukifungua na kukifunga upya mmmhhh aiseee hili sio suala la mzaha ...
Kuhusu kuweka maji huwa siwezi bali huwa na msafisha na pamba + maji ya chumvi
 
Shukrani mkuu MziziMkavu sasa iwapo siishi dar naweza kupata katika maduka gani mkuu au ndio nisafiri hadi dar??????
 
Last edited by a moderator:
Shukrani ndugu napata picha kukifungua na kukifunga upya mmmhhh aiseee hili sio suala la mzaha ...
Kuhusu kuweka maji huwa siwezi bali huwa na msafisha na pamba + maji ya chumvi

Dear.... Watoto wanapozaliwa huko hospitalini huwa tunaambiwa kitovu kisiingie maji kabisa.

Kinatoa maji yenye harufu? Kwa watoto wachanga wanapozaliwa, hupewa dawa ya Povidone ( for external use only) pekee ndio inaweka

kwenye pamba kidogo unampakaa hapo kwenye kitovu kinapona kabisa kabisa. Tafuta daktari wa watoto mzoefu mkoa

wa Dar es salaam. Asikudanganye mtu, mikoani matibabu bado ni challenge kubwa sana. Pole dear.
 
Asante ndugu maji hayatoi harufu nakumbuka nilizingatia sana kutokuweka maji hadi kilipofunga kabisa.... Lakini tatizo ni kwamba anapona then kinaanza tena just imagine toka mwez wa 11 mwaka jana ndio alisumbuliwa na hilo tatizo baada ya kutumia dawa akawa poa lakini jana nashangaa hali imeanza tena...... Nashukuru kwa ushauri dear aisee hata mambo hayaendi kabisa
 
Pole mkuu, nina ushauri kidogo kwenye hili,
Mwanangu alisumbuliwa na hili alivyozaliwa kitovu kilichelewa sana kupona japo alizaliwa muhimbili na wao ndo walikuwa wanamtibu walituahidi kitapona tu so wakatuambia tuhakikishe hakiingii maji wakat wa kuoga japo tulijitahd ila ilichukua muda kidogo still.
What i did nilienda morroco kwa dr. Masawe huyu ni mtaalamu wa watoto alitupokea vizur akamcheki mtoto na kutushauri yafuatayo
Moja kitovu hakikufungwa vizur wakati wa kuzaliwa na pia according to yeye pia wakati kinakatika kuna kama kimfupa kama kilibaki so akasema hata kama tungempaka dawa kwa mwaka mzima kisingeweza pona mana kilikuwa kinafunga nje unaona kama kinapona ila after muda kama wiki unakuta tena kipo wazi na kidonda kibichi pamoja na kuosha kwa spirit na kuavoid maji kuingia.

Solution, what he did walifanya kama kukata na kukitoa kimfupa kile then wakapaka dawa kama ya kuchoma hvi ni dawa kama ya kuunguza ambayo hata ukimbesha mtoto nguo inachafua na kuacha doa ambalo halitoki, believe me we visited there twice and problem was solved permanently mpka kesho mtoto ana afya njema.
Kama upo Dar ni karibu mtafute dr masawe ni bingwa wa watoto atakusaidia yupo hospital yake karibu na jengo la airtel morroco pole na natumaini utatupa mrejesho.
MUNGU ni mwema jitahid ufike natumain atapona na pole sana kwa kuuguza Manka M
 
Kupata hiyo kwa hapo Mbeya jaribu kwenda kwenye duka la Mpemba mmoja soko matola. Ukifika pale ulizia kwa Mwamba.
Kila la Kheri
 
Shukrani ndugu napata picha kukifungua na kukifunga upya mmmhhh aiseee hili sio suala la mzaha ...
Kuhusu kuweka maji huwa siwezi bali huwa na msafisha na pamba + maji ya chumvi

Nenda hospital...dawa za Mzizi mkavu siziamini asilimia zote.
 
Shukrani ndugu napata picha kukifungua na kukifunga upya mmmhhh aiseee hili sio suala la mzaha ...
Kuhusu kuweka maji huwa siwezi bali huwa na msafisha na pamba + maji ya chumvi

kukifungua na kufungwa upya wala isikufanye uwaze sana maana kwa mtoto kitovu kinakutana ma utumbo tu. .
nenda hospital kubwa kama muhimbili. kwa kanda ya magharibi jaribu ile hospitali ya mission maarufu kwa jina la IKONDA, wako vizuri sana. Ipo makete kama unatokea Mbeya..
usipuuzie maana mtoto anaweza pata kilema maisha na kuleta kasoro kwenye mfumo wa mmeng'enyo wa chakula.
 
Asante ndugu yangu kwa kuwa niko mbeya ni rahisi sana kufika Ikonda
 
Nakushauri uende kuonana na madaktari bingwa wa watoto.....ni tatizo dogo lakini ukilichekea litakuletea majuto ambayo ni mjukuu....achana na mambo ya kubahatisha madawa....kumbuka afya ya mwanao ndio kila kitu kwako kwa kuwa mtoto wako ndio kila kitu kwako....nakusisitiza tena popote ulipo watafute mabingwa..........
 
Back
Top Bottom