Kuulizwa maswali.
Yesu alikuwa haogopi kuulizwa maswali. Hata kama ni ya kijinga atatafuta namna ya kukujibu ili uache huo ujinga.
Watu wengi wanaelewa kwa njia ya maswali. Nimeona wengi wanapenda kuongea mambo yao ila hawana ujasiri wa kuwaacha wanaowasikiliza wahoji na kuuliza maswali ili waelewe kwa kina.
Hii tabia imelekea kuwa na waumini wenye uelewa finyu na mashabiki wasio na ujasiri kwa wanayoyaamini.
Hii tabia imesababisha kuwa na watumishi majasiri kwenye mimbari ila waoga sana kwenye uhalisia wa maisha.
Tujifunze kwa Yesu.
Sabato njema.
Bado siungi mkono hoja yako kwani watu(waamini na ww ukiwa mmojawapo) wanataka waulize maswali wakati wa Ibada au ndani ya muda wa kuabudu. Hao hao wenye kutaka kuuliza maswali wakipewa Fursa e.g. wakialikwa kwenye kongamano, vikao, semina au warsha hawajitokezi. Wanakuwa na madai ya kuwa eti wapo Busy.
Hao hao ni ndio wenye kupotosha Taarifa zinazotolewa katika matangazo rasmi siku ya kuabudu au Sala. Hawapo tayari kujitokeza au kutumia Taratibu zilizopo ili kuhoji,kuuliza maswali n.k. Wanakuwa na "vijiwe" na huwavuta watu kwa maneno ya kujikweza na kukosoa watu wengine(Hususan wachungaji) huwanyoshea vidole sio wachungaji tu lakini hata na viongozi wengine wa Kanisa au wale wanaohudhuria vizuri siku za kuabudu au sala kanisani kwa kudai wanazifahamu siri zao na mbinu wanazotumia kuwahadaa waamini. Hao ni Mafarisayo.
Kama kuna maswali:
1. Mfuate mchungaji au kiongozi mlengwa umuulize maswali ana kwa ana. Haifai na wala sio busara maswali yaulizwe ndani ya Ibada. Akikuambia hana nafasi omba appointment au
2. Andika Swali/Maswali na umkabidhi mchungaji au kiongozi mhusika na utake majibu ama verbally au kwa maandishi pia.
3. Usipende sana kuuliza maswali bali jaribu kutafuta majibu ww mwenyewe kwa kujisomea au hata kwenye mitandao.
4. Kumbuka mchungaji ni mtu kama ww i.e. anavionjo vyake na madhaifu yake. Wengine wanaweza kuonesha kukasirika au kuudhika na wengine kukuona ww ni msumbufu, mkorofi, una kimbelembele au mzabizabina na pengine mchungaji akajenga chuki dhidi yako.
Mwisho kumbuka hata Yesu maswali mengine aliyapotezea e.g. Pilato alimwuliza: " Je wewe ndiwe Mfalme wa Wayahudi? Yesu alimjibu kwamba wewe umesema kwamba mm ni mfalme wa ....Mat.27:11 - 66.
Tena inafaa kuzingatia kwamba kuruhusu mswali kunaweza kuamsha Roho ya mtafaruku ndani ya kanisa. Inafaa sana
ujue kwamba Ibilisi (Shetani au Roho ya Uasi) anahudhuria sana sana kanisani na huwa yupo makini sana ili asipoteze nafasi
mpenyo kuvuruga kundi. Ibilisi haendagi bar au kwenye madisco kwani kule wapo wawakilishi wake na wanapiga kazi vizuri.
Naomba niishie hapo- Ubarikiwe sana.