mbenge
JF-Expert Member
- May 15, 2019
- 4,864
- 10,483
Sijui ni mimi pekee yangu na jirani zangu wawili ambao ndiyo tulikishudia chombo hicho, ama ilitokea pia kwa watu wengine. Ilikuwa jana yapata saa moja jioni, giza ndiyo kwanza limeingia, ile tu natoka nje ya geti la uzio wa nyumba yangu kwenda club kuangalia pambano la soka kati ya Liverpool na Arsenal, nikaanza kusikia sauti ya mvumo kama ule wa sauti za nyuki wengi wawapo angani.
Ilikuwa ni sauti ambayo haiko endelevu, bali inasikika kwa muda na hatimaye inakatika na kubakia kimya kwa kitambo. Nilitembea kama hatua kumi na tano, hivi nikawakuta jirani zangu wawili.
Baada ya kusalimiana walinionyesha kushangazwa na kitu hicho cha ajabu kilichokuwa kikitoa mlio wa ajabu. Licha ya sauti yake pia kilikuwa kikitoa mianga ya taa nyingi za rangi ya bluu.
Kwa sekunde kadhaa kilikuwa angani kikielekea uelekeo wa mawio ya jua. Lakini tofauti na ndege nyingine ziwapo angani, ambapo husafiri kwa upande mrefu kuwa ndio muelekeo wa chombo, chenyewe kilioneka kama vile kinasafiri kwa ulekeo wa mapana yake.
Je! Kuna mtu mwingine pia alilishuhudia jambo hili siku ya jana? Ingalikuwa ni mimi pekee yangu ndiye ambaye nilishuhudia jambo hili ningelipotezea, na hata ningevuta subiri ili atokee shuhuda mwingine ambaye angesimulia.
Sasa mashuhuda tulikuwa ni watatu, tena wote watu waxima. Je! Kuna mtu mwingine aliweza kulishuhudia hapa jukwaani.