Kitu cha ajabu chaonekana kikiwa angani jana jioni

Nilikuwa mimi Baba , Mama na mdogo wangu wakike tukielekea shambani majira ya asubuhi.
ghafla kwa mbele yetu tuliona watu watu 3 ila sio binadamu wa kawaida, macho yao yalikuwa makubwa na nyuso za kuchongoka na zaidi hawakuwa na nguo.
tuliwashangaa kwa kuwakazia macho na wao pia walikuwa wakituangalia bila kuonyeasha wasiwasi wowote machoni mwao.
baba alisema uenda ni malaika.
baada ya miaka mingi kupita na kukutana na masimulizi ya watu ya matukio kama ilo nikagundua mimi na familia yangu tuliona Allies.

** NUKUU KUTOKA KWA JAMAA MMOJA WA BOTSWANA**.
 
Sijui ni mimi pekee yangu na jirani zangu wawili ambao ndiyo tulikishudia chombo hicho, ama ilitokea pia kwa watu wengine. Ilikuwa jana yapata saa moja jioni, giza ndiyo kwanza limeingia, ile tu natoka nje ya geti la uzio wa nyumba yangu kwenda club kuangalia pambano la soka kati ya Liverpool na Arsenal, nikaanza kusikia sauti ya mvumo kama ule wa sauti za nyuki wengi wawapo angani.

Ilikuwa ni sauti ambayo haiko endelevu, bali inasikika kwa muda na hatimaye inakatika na kubakia kimya kwa kitambo. Nilitembea kama hatua kumi na tano, hivi nikawakuta jirani zangu wawili.

Baada ya kusalimiana walinionyesha kushangazwa na kitu hicho cha ajabu kilichokuwa kikitoa mlio wa ajabu. Licha ya sauti yake pia kilikuwa kikitoa mianga ya taa nyingi za rangi ya bluu.

Kwa sekunde kadhaa kilikuwa angani kikielekea uelekeo wa mawio ya jua. Lakini tofauti na ndege nyingine ziwapo angani, ambapo husafiri kwa upande mrefu kuwa ndio muelekeo wa chombo, chenyewe kilioneka kama vile kinasafiri kwa ulekeo wa mapana yake.

Je! Kuna mtu mwingine pia alilishuhudia jambo hili siku ya jana? Ingalikuwa ni mimi pekee yangu ndiye ambaye nilishuhudia jambo hili ningelipotezea, na hata ningevuta subiri ili atokee shuhuda mwingine ambaye angesimulia.

Sasa mashuhuda tulikuwa ni watatu, tena wote watu waxima. Je! Kuna mtu mwingine aliweza kulishuhudia hapa jukwaani.
Hata Nachingwea kilionekana muda huohuo.
Kwa akili yako unadhani ukiona Kibaha na Mkuranga wanaona na Lindi wanaona, eleza wewe ulikuwa wapi, ukiona huko Kasulu unadhani na Pemba wanaona.
 
Itakua ndoto hiyo yaani zile ndoto unaota ukiwa macho mi pia ushawai kuota hivyo hivyo sema mimi ilikua ni safari ya kwenda mbingun [emoji16] yaani Kwanza movie linaanza niko zangu njiani to mbingun nikawa napita katikati ya msitu mnene nikaumaliza ule msitu ile natoka tu nikakutana na bonge la mlima nikapanda nikaumaliza ile na maliza tu nikakutana na bonge la mto yaani sion ng'ambo ya pili na kivuko sikion nikakumbuka kua huo mto ni jordan na ndio ilikua stage ya MWISHO niingie zangu mbingun MIE[emoji3059][emoji3059] nikavuka KWA kupaa nikatua ng'ambo ya pili ile natua tu hata sijapiga jicho popote nasituka saa saba mchana na hata sikulala [emoji16]mweee ndoto za mchana salute
 
Picha zikuweza kuchukua kutokana kasi ya mwendo wake. Ila suala la location mimi naishi Mbezi Beach.
Je kabla ya kutoka nje ya nyumba yako uenye ukuta ulitoka kuangalia katuni za HenryDanger au Stars pace?
 
Hivi hata kama ndio wewe unasimuliwa tukio kama hili kwa mazingira tofauti, utajihakikishiaje kwamba hiyo habari niya kweli?
 
Tatizo huwezi kuelewa, sikuwa peke yangu, bali nilikuwa na jirani zangu wawili ambao wote kwa pamoja tulishuhudia tukio hilo.
 
Tatizo sio wewe kusimulia kuonesha ulikua peke yako kwenye hilo tukio

Nachomaanisha ni kwamba leo hii mtu aje asimulie humu kwamba yeye na rafiki zake wameona kobe akikimbia kwa speed ya mwanga, utahitaji kitu gani kwenye ku support hayo maelezo ili uamini hiyo stori ni yakweli?

Je maelezo ya kusema alikua na rafiki yake, kwako yangetosha kukubaliana naye?
 
Mkuu itakua ni drone, UFO huwa hazina sauti kwa mujibu wa maelezo ya waliozishuhudia..

View attachment 2018708

View attachment 2018709
Hata mimi nakubaliana na uwezekano wa kuwa ni "drone" kutokana na sauti yake, lakini kumbuka hatukusikia upepo wote upulizao kutokana na uwepo wake angani.

Aidha, kwa ukubwa wake na wingi wa taa zake zake kidogo ndipo muonekano wake ulipitutatiza. Maana kwa umbali kilipokuwa juu ni sawa kabisa na umbali wa ndege zipitapo juu angani.
 
Tatizo sio wewe kusimulia kuonesha ulikua peke yako kwenye hilo tukio

Nachomaanisha ni kwamba leo hii mtu aje asimulie humu kwamba yeye na rafiki zake wameona kobe akikimbia kwa speed ya mwanga, utahitaji kitu gani kwenye ku support hayo maelezo ili uamini hiyo stori ni yakweli?

Je maelezo ya kusema alikua na rafiki yake, kwako yangetosha kukubaliana naye?
Mkuu, isiwe shida. Ni mimi ambaye ndiye nimeshuhudia. Lakini pia sikuwa peke yangu. Kwa mtu yeyote anayejali anaweza kufanya kile ambacho mimi nimekifanya, kwa kuwa naamini kupashana habari kunafumbua akili kwa mtu aliye mdadisi.

Ebu tuchukulie ningeamua kuuchuna, sidhani kama miongoni mwetu kuna mtu angalijua nini ambacho kilitokea. Lakini pia tujiongeze na tuchukulie pengine jambo hilo lina tishio la kiusalama, huoni kuwa kwa kulisema linaweza kutoa "elerts" fulani.
 
Natambua umuhimu wa kuchukua picha, lakini mazingira niliyokuwepo ilikuwa ni vigumu kufanya hivyo.
Hayo mambo yapo sana kwa mtu anayetumia muda kidogo kuangalia anga ataona maajabu mengi. Pia kuna mavyombo yasiyojulikana yanasafiri angani, wakati mwingine na vitu vya kiroho ambavyo havikusitirika kikamilifu mbele ya wanadamu.
 
Mkuu, isiwe shida. Ni mimi ambaye ndiye nimeshuhudia. Lakini pia sikuwa peke yangu. Kwa mtu yeyote anayejali anaweza kufanya kile ambacho mimi nimekifanya, kwa kuwa naamini kupashana habari kunafumbua akili kwa mtu aliye mdadisi.

Ebu tuchukulie ningeamua kuuchuna, sidhani kama miongoni mwetu kuna mtu angalijua nini ambacho kilitokea. Lakini pia tujiongeze na tuchukulie pengine jambo hilo lina tishio la kiusalama, huoni kuwa kwa kulisema linaweza kutoa "elerts" fulani.
Nadhani maana yangu hujaielewa

Maana yangu haikuwa wewe kutoshea na sisi hiyo habari

Maana yangu ni kwa namna gani unaweza kuwahakikishia wasomaji kua tukio hilo ni kweli

Au kwa maoni yako ni kipi ambacho ukikisoma kwenye hayo maelezo yako kinakupa confidence inayoipa nguvu habari hiyo ionekane ni kweli?
 
Sijui ni mimi pekee yangu na jirani zangu wawili ambao ndiyo tulikishudia chombo hicho, ama ilitokea pia kwa watu wengine. Ilikuwa jana yapata saa moja jioni, giza ndiyo kwanza limeingia, ile tu natoka nje ya geti la uzio wa nyumba yangu kwenda club kuangalia pambano la soka kati ya Liverpool na Arsenal, nikaanza kusikia sauti ya mvumo kama ule wa sauti za nyuki wengi wawapo angani.

Ilikuwa ni sauti ambayo haiko endelevu, bali inasikika kwa muda na hatimaye inakatika na kubakia kimya kwa kitambo. Nilitembea kama hatua kumi na tano, hivi nikawakuta jirani zangu wawili.

Baada ya kusalimiana walinionyesha kushangazwa na kitu hicho cha ajabu kilichokuwa kikitoa mlio wa ajabu. Licha ya sauti yake pia kilikuwa kikitoa mianga ya taa nyingi za rangi ya bluu.

Kwa sekunde kadhaa kilikuwa angani kikielekea uelekeo wa mawio ya jua. Lakini tofauti na ndege nyingine ziwapo angani, ambapo husafiri kwa upande mrefu kuwa ndio muelekeo wa chombo, chenyewe kilioneka kama vile kinasafiri kwa ulekeo wa mapana yake.

Je! Kuna mtu mwingine pia alilishuhudia jambo hili siku ya jana? Ingalikuwa ni mimi pekee yangu ndiye ambaye nilishuhudia jambo hili ningelipotezea, na hata ningevuta subiri ili atokee shuhuda mwingine ambaye angesimulia.

Sasa mashuhuda tulikuwa ni watatu, tena wote watu waxima. Je! Kuna mtu mwingine aliweza kulishuhudia hapa jukwaani.
Weya izi pikiture?
 
mbezi beach kuna mauchawi mengi sana usione majumba mazuri ukajua tu yamepatikana bure bure.

its a process
Muulizeni Bujibuji na mauchawi ya mbezi beach.

Back
Top Bottom