Kitu cha ajabu chaonekana kikiwa angani jana jioni

Kitu cha ajabu chaonekana kikiwa angani jana jioni

Itakua ndoto hiyo yaani zile ndoto unaota ukiwa macho mi pia ushawai kuota hivyo hivyo sema mimi ilikua ni safari ya kwenda mbingun [emoji16] yaani Kwanza movie linaanza niko zangu njiani to mbingun nikawa napita katikati ya msitu mnene nikaumaliza ule msitu ile natoka tu nikakutana na bonge la mlima nikapanda nikaumaliza ile na maliza tu nikakutana na bonge la mto yaani sion ng'ambo ya pili na kivuko sikion nikakumbuka kua huo mto ni jordan na ndio ilikua stage ya MWISHO niingie zangu mbingun MIE[emoji3059][emoji3059] nikavuka KWA kupaa nikatua ng'ambo ya pili ile natua tu hata sijapiga jicho popote nasituka saa saba mchana na hata sikulala [emoji16]mweee ndoto za mchana salute
Aisee umeniacha hoi!!!!!!!!!
 
UFo! Wanakataa lakini hizi Flying Object zipo, miezi miwili nyuma, location morogoro vijijini niliiona moja mida ya saa moja jion narudi kutoka mazoezini juu ya mlima mmoja unaitwa chamanyani, sikuwa na simu wakati huo, lakini nilikuwa niiona vizuri kabisa mpaka ilipokuja kupotea, hii itakuwa ni mara ya tatu kuona hayo madubwana, kwa mara ya kwanza kwenye pori la ushirombo, mara ya dakawa center ( ukimbizini ) na mara ya tatu ni miezi miwili iliyopita...

Sehemu zenye utajiri wa madini hasa dhahabu hizi UFO zimekuwa zikionekana mara kwa mara. Naamini mara nne nitakuwa na ushahidi kabisa
 
UFO?
Kutokana na ukubwa wa galaxy na universe yetu pia wingi wa nyota na sayari zake kama tunavyoambiwa ni impossible kuamini kwamba tupo peke yetu.
Lazima kutakuwa na immense amount of intelligent life out there ila hatuwezi kunotice labda kwa sababu tuko nyuma kiupeo na kitechnology.
Au tayari kuna makundi ya watu wachache wanaojua ukweli juu ya hivi vitu lakini wameficha.

Nikianza kuandika na kufikiria kuhusu haya mambo huwa simalizi alafu naishia kuandika gazeti kubwa la conspiracy lakini ngoja niandike angalau kidogo.

Siku moja mida ya saa 9 usiku nilishuhudia kitu chenye mwanga mkali kama mwezi kikimulika angani huku kikicheza cheza huku na kule na hapo ndipo nilipogundua kwamba haukuwa mwezi, kwa uoga nikashindwa hata kuchukua simu kurekodi sababu nilikuwa nikitetemeka mpaka nikajishangaa sababu mimi sijawahi kutetemeka hata nikiogopa vipi.

Then baada ya sekunde kadhaa kikapotea and I was like WTH?
Kesho asubuhi kila nileyemwambia hakuamini nikasema potezea pote lakini kichwani bado nilikuwa nikijiuliza kile ni nini na huwezi sema nilikuwa high sababu mimi sio mtu wa mambo hayo.

Na sio mimi tu kwa wafuatiliaji wa channel yetu pedwa ya discovery science lazima mtajua kuhusu haya mambo jinsi watu wanavyotoa ushuhuda na wachambuzi mahili kuchambua haya mambo.
Youtube yapo japo mostly ni fake footage.

Mimi kwa asilimia 50% nadhani hatupo peke yetu na mataifa ambayo ni superpower kuna mambo mengi wanayajua ila ili kuzuia global panic yanafichwa kwa usiri mkubwa na sababu moja wapo ni kuwa binadamu hawako tayari kupokea habari kama hizi kwa sasa.

Mfano marekani kuna vitengo na sehemu kama The pentagon au sehemu kama Area 51 hizi sehemu bila shaka kuna siri nzito ndani yake kama hizi siri zikitoka basi duniani hapatokalika kwa amani tena.
Na ndio maana viwango vya ulinzi sehemu hizi uko juu kuliko sehemu yoyote ile duniani. wewe sogeza pua tu then baada ya sekunde utaamkia mbinguni.

Na ngoja niwe clear kidogo niposema UFO simaanishi kwamba ni aliens moja kwa moja wanapita na ndege zao hapana bali chochote kinachoruka angani bila utambulisho maalum ni UFO hata uwe ungo.

So maybe hizi UFO ni extraterrestrial beings au viumbe kutoka nyota na sayari za mbali wakifanya uchunguzi au kutalii tu kama tunavyopita mbuga za wanyama.

Imagine leo uambiwe kuna viumbe wengine ambao wapo tofauti na sisi na wametuzidi kila kitu wewe utafanyaje?
Utakuwa na amani hapo? sababu lazima utaanza kujiuliza vipi kama wana nia mbaya na sisi? na maswali mengine mengi yasiyo na majibu.
Dini na viongozi wa dini wataanguka, uchumi utaporomoka, umasikini utakithiri, watu watajiua na kuuana na mostly Amani itatoweka duniani.

Hii kama kweli ni siri nzito basi wataishikilia lakini ipo siku itafuchuka yenyewe lakini kwa sasa binadamu hawako tayari kupokea habari kama hizi.
 
Msimlaumu huyu jamaa Kwa kukosa picha, Mimi niliwahi kuona kitu Cha ajabu angani, nikajitahidi kupiga picha, Cha ajabu picha ilitokea isiyoonyesha chochote!!

Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
 
J
Sijui ni mimi pekee yangu na jirani zangu wawili ambao ndiyo tulikishudia chombo hicho, ama ilitokea pia kwa watu wengine. Ilikuwa jana yapata saa moja jioni, giza ndiyo kwanza limeingia, ile tu natoka nje ya geti la uzio wa nyumba yangu kwenda club kuangalia pambano la soka kati ya Liverpool na Arsenal, nikaanza kusikia sauti ya mvumo kama ule wa sauti za nyuki wengi wawapo angani.

Ilikuwa ni sauti ambayo haiko endelevu, bali inasikika kwa muda na hatimaye inakatika na kubakia kimya kwa kitambo. Nilitembea kama hatua kumi na tano, hivi nikawakuta jirani zangu wawili.

Baada ya kusalimiana walinionyesha kushangazwa na kitu hicho cha ajabu kilichokuwa kikitoa mlio wa ajabu. Licha ya sauti yake pia kilikuwa kikitoa mianga ya taa nyingi za rangi ya bluu.

Kwa sekunde kadhaa kilikuwa angani kikielekea uelekeo wa mawio ya jua. Lakini tofauti na ndege nyingine ziwapo angani, ambapo husafiri kwa upande mrefu kuwa ndio muelekeo wa chombo, chenyewe kilioneka kama vile kinasafiri kwa ulekeo wa mapana yake.

Je! Kuna mtu mwingine pia alilishuhudia jambo hili siku ya jana? Ingalikuwa ni mimi pekee yangu ndiye ambaye nilishuhudia jambo hili ningelipotezea, na hata ningevuta subiri ili atokee shuhuda mwingine ambaye angesimulia.

Sasa mashuhuda tulikuwa ni watatu, tena wote watu waxima. Je! Kuna mtu mwingine aliweza kulishuhudia hapa jukwaani.
Zinaitwa drones
 
Binadamu tupo tofauti sana. kwa mimi inaweza pita miezi hata kumi 10 siwezi angalia ANGANI zaidi ya sec 15 yani zimezidi sana sec 7
 
Izo story kila nkisikia bd zinabak na maswali meng sana yasiyo na majib
 
Binadamu tupo tofauti sana. kwa mimi inaweza pita miezi hata kumi 10 siwezi angalia ANGANI zaidi ya sec 15 yani zimezidi sana sec 7

kaka hilo dude nililoliona mimi linawaka kama jua. huna aja ya kuangalia juu ndio uone. Linapita chini na lina mwanga wa hatari
 
Sijapaelewa hapo
Mfano mshale husafiri kwa urefu wake. Sasa uwe unasafiri kwa mapana yake. Ndege (aeroplane) huruma kwa urefu wake, na badala yake iruke kwa mapana yake.
 
Kwa kifupi hiyo ni drone hakuna kitu zaidi ya hicho, alafu hata drone zipo kubwa.

Jana nikiwa viwanja vya Mao hapa unguja uwanja wa juu nimekaa jukwaa kucheki mazoezi ya mpira muda wa 2100hrd niliona kitu kama but baadaye niligundua ni drone.
 
Kama vile ambavyo niliahidi siku za nyuma, jana niliweza kukutanana na mmoja wa jirani zangu ambaye tuliweza kwa pamoja kuliona tukio la Jumamosi jioni. Katika mazunguzo yetu tuliweza kuwa na vitu kadhaa ambavyo wote tulivishuhudia, lakini pia kulikuwa na maelezo zaidi kutoka kwake ambayo mimi sikuweza kuyaona.

Tukianza na vitu tulivyoviona kwa pamoja juu ya chombo hicho, ni kuhusu ukubwa wake, mvumo wa sauti ambayo ulisikika, mianga ya taa zake nyingi za rangi ya bluu, uelekeo ambao kikielekea na pia kasi ya chombo hicho.

Ila yeye alikuwa alikuwa na maelezo zaidi. Yeye alipata muda wa kukiona kikienda, kikiganda hewani kwa muda na kisha kubadilisha muelekeo. Aidha anasema kile chombo kimuundo kwa vyovyote vile hakiwezi kuwa "aeroplane" ya kawaida ama "helicopter" kutokana na kile alichokiona.

Kuhusu kuwa "drone" hilo jambo anakubaliana nalo, ingawaje kuhusu kasi na ukubwa wake ni kitu ambacho bado kinamchanganya kidogo. Hata yeye pia yupo "interested" kujua zaidi juu ya kitu hiki.

Wakuu kilichobakia sasa tutarajie maelezo zaidi kutoka kwa jirani aliyebakia. Natambua wanaume wengi ni "blind in colours". Kwa kuwa huyu wa pili ni mwanamke, na pia ndiye aliyekuwa wa kwanza kukiona chombo hiki, basi maelezo yake natarajia yatakuwa na mambo mengine zaidi.

Nawatakia siku njema.
 
Back
Top Bottom