Kitu gani alitumia Hayati Magufuli kuzima maandamano ya UKUTA mwaka 2015 tena kwa tamko tu bila hata bunduki kulipuliwa?

Salute wakuu, mie mpaka leo ninakuna kichwa, ni kitu gani JPM alitumia kuzima maandamano yaliyokuwa yameitishwa na CHADEMA baada ya uchaguzi wa 2015 maarufu kwa jina la UKUTA?, kipindi kile JPM ndio tu alikuwa ameapishwa, hata baraza la Mawaziri alikuwa bado hajateua. Je ni nguvu gani ya kiupako huyu mwamba alikuwa nayo?.

Nakumbuka kipindi cha kumalizia utawala wa Jakaya Kikwete ilikuwa ni shida ,pamoja na Kikwete kuzuia maandamano lkn yalikuwa yanafanyika,mpaka ikapelekea watu kufa kwa kulipuliwa kwenye mkutano na maandamano Arusha, pia Mwangosi alikufa kwa kulipuliwa pia kwenye maandamano, je kwanini JPM yeye alitoa tamko tu na ukuta ikanywea?,

Je, ukuta walimwogopa JPM au walikuwa wanatingisha kiberiti ili kuona kama kimejaa?

Lkn pia kwanini tamko lake tu lilinyamazisha majambazi waliokuwa wanavamia mpaka mchana?, mpaka Bank na vituo vya polisi vilikuwa vinavamiwa mchana kweupe?,

Hata mauaji ya albino yalikoma!,

Ajali za ovyo ovyo zilikoma,

Je, Alikuwa na upako wa kiutawala kutoka kwa Mungu!?, au ilikuwa ni nini?!.

KARIBUNI, mapovu yanaruhusiwa kwa wale wenye hilka hiyo,na hata wenye afya mbovu za akili,

Umesahau polisi na jeshi walivyokuwa wanafanya mazoezi?. Kila mkoa walifanya mazoezi. UKUTA uliishia njiani baada ya kuona jeshi linataka kuingilia Kati maandamano.
 
Mkuu soma mada uielewa,ndio uchangie,ukuta imeitishw tu baada ya kutangazw jpm kashinda,chadema ikasema tarehe moja itakuw ni siku ya maandamano ya ukuta.niambie kipindi kile bunduki gn alilia ili kuzuia maandamano?

Kumbuka UKUTA umeitishwa baada ya Magu kukataza mikutano ya siasa na akapiga mkwara kwamba atakayefanya atalala naye mbele. Akaliingiza JWTZ kwenye mambo ya kijinga ili kuwatisha CHADEMA. Yule hakufaa kuwa Rais wa nchi basi tu.
 
Japo nilikuwa kijana mdogo sana hata sijaanza Darasa la kwanza ila kumbukumbu zangu zinaniambia kuwa kwa bahati mbaya sana ratiba ya maandamano ya UKUTA ziliingilana na ratiba ya kufanya "Fatiki" (usafi) na wale jamaa wa bakabaka bila kusahau barabara zilikuwa ziko "Busy" maana wale jamaa wa wanaovaa kofia nyekundu walikuwa wakipiga "Route March" na mchakamchaka nchi nzima.
Ila pia huenda aliyekabidhiwa jukumu la kufanikisha UKUTA unatokea alikula pesa ya Saruji.

UKUTA ulisitishwa baada ya kuona JWTZ imeingilia Kati. Lengo lilikuwa kulitumia jeshi kuzima maandamano na muelekeo ulikuwa hata kuua waandamanaji. Jeshi likishaingia kwenye siasa Hilo Jambo jingine
 
Vp kuhusu majambazi waliokuwa wanavamia bank na vituo vya polisi?, wao waligwaya nn?

Unaongelea majambazi au maandamano?. Halafu kumbe hata kwa Magu majambazi walikuwepo. Si umesema Kwenye utawala wake ilikuwa ni asali na maziwa.
 
Salute wakuu, mie mpaka leo ninakuna kichwa, ni kitu gani JPM alitumia kuzima maandamano yaliyokuwa yameitishwa na CHADEMA baada ya uchaguzi wa 2015 maarufu kwa jina la UKUTA?, kipindi kile JPM ndio tu alikuwa ameapishwa, hata baraza la Mawaziri alikuwa bado hajateua. Je ni nguvu gani ya kiupako huyu mwamba alikuwa nayo?.

Nakumbuka kipindi cha kumalizia utawala wa Jakaya Kikwete ilikuwa ni shida ,pamoja na Kikwete kuzuia maandamano lkn yalikuwa yanafanyika,mpaka ikapelekea watu kufa kwa kulipuliwa kwenye mkutano na maandamano Arusha, pia Mwangosi alikufa kwa kulipuliwa pia kwenye maandamano, je kwanini JPM yeye alitoa tamko tu na ukuta ikanywea?,

Je, ukuta walimwogopa JPM au walikuwa wanatingisha kiberiti ili kuona kama kimejaa?

Lkn pia kwanini tamko lake tu lilinyamazisha majambazi waliokuwa wanavamia mpaka mchana?, mpaka Bank na vituo vya polisi vilikuwa vinavamiwa mchana kweupe?,

Hata mauaji ya albino yalikoma!,

Ajali za ovyo ovyo zilikoma,

Je, Alikuwa na upako wa kiutawala kutoka kwa Mungu!?, au ilikuwa ni nini?!.

KARIBUNI, mapovu yanaruhusiwa kwa wale wenye hilka hiyo,na hata wenye afya mbovu za akili,
Polisi wasio na hatia waliuliwa ili kuaminisha umma kuwa wauaji walipora silaha za kutumia kwenye maandamano. Hivyo magu akavalisha hadi wanajeshi sare za polisi kutisha raia.
Screenshot_20230203-134313~2.jpg
 
Yule mwamba na Nyerere ndio wanaume wa nchi ya Tanzania
Muondoe huyo mwamba Bora sokoinne au Abdul Sykes. Mwamba gani ana ubaguzi wa wazi. Usiwabomolee nyumba watu wa Mwanza walinichagua ila kimara bomoa. Huyo ni Rais kweli. Tuwe wakweli.
 
Muoga aliyezuia maandamano au muoga ni yule aliyezuiwa kuandamana na akaufyata kweli

Muoga ni yule aliyezuia maandamano kwa kutumia JWTZ. Siku ya UKUTA wakatangaza Ni siku ya usafi wa JWTZ, Ina maana CHADEMA wangepambana na jeshi, Sasa hayo hayakuwa malengo ya maandamano. UKUTA ulisimama baada ya JWTZ kujiingiza kwenye siasa.
 
Kuna aliyekuwa anatumia mtutu wa bunduki kumzidi yeye?
asali ni hatare kwa uhuru wa habari kuliko risasi

Inflation ya sasa ingekuwa wakati wa Mwamba tungekoma kwa hoja nzito nzito za kina Zitto na Chadema
 
Lkn ndani ya mwezi mmoja ya utawala wa jpm? Kabla hata hajateua baraza la mawaziri,?. Kikwete aliua lkn chadema ndio ilipamba moto.

Acha uongo UKUTA umeitishwa miezi Tisa baada ya Magufuli kukaa madarakani. Halafu Magufuli mbona kamuua Akweline kwenye maandamano ya Kinondoni. Yule alipania kuwaua wapinzani Kama wangandamana. Sasa kichaa sio wa kukimbilia naye.
 
Na kikwete alishindwa kwa katiba ipi?, au swaum inakusumbua

Kikwete hakuwa mwehu Kama Magu. Magu lengo lake ni kuua. Sasa ukishamjua muuaji kwa Nini uhangaike?. Halafu Kikwete hakutumia JWTZ kwenye maandamano.
 
Salute wakuu, mie mpaka leo ninakuna kichwa, ni kitu gani JPM alitumia kuzima maandamano yaliyokuwa yameitishwa na CHADEMA baada ya uchaguzi wa 2015 maarufu kwa jina la UKUTA?, kipindi kile JPM ndio tu alikuwa ameapishwa, hata baraza la Mawaziri alikuwa bado hajateua. Je ni nguvu gani ya kiupako huyu mwamba alikuwa nayo?.

Nakumbuka kipindi cha kumalizia utawala wa Jakaya Kikwete ilikuwa ni shida ,pamoja na Kikwete kuzuia maandamano lkn yalikuwa yanafanyika,mpaka ikapelekea watu kufa kwa kulipuliwa kwenye mkutano na maandamano Arusha, pia Mwangosi alikufa kwa kulipuliwa pia kwenye maandamano, je kwanini JPM yeye alitoa tamko tu na ukuta ikanywea?,

Je, ukuta walimwogopa JPM au walikuwa wanatingisha kiberiti ili kuona kama kimejaa?

Lkn pia kwanini tamko lake tu lilinyamazisha majambazi waliokuwa wanavamia mpaka mchana?, mpaka Bank na vituo vya polisi vilikuwa vinavamiwa mchana kweupe?,

Hata mauaji ya albino yalikoma!,

Ajali za ovyo ovyo zilikoma,

Je, Alikuwa na upako wa kiutawala kutoka kwa Mungu!?, au ilikuwa ni nini?!.

KARIBUNI, mapovu yanaruhusiwa kwa wale wenye hilka hiyo,na hata wenye afya mbovu za akili,
Ukiwa dictata mfumo wote unafuata hivyo , simple kupoteza ,kupiga risasi watu inakuwa kawaida
 
Na waliokuwa wanavamia bank mchana kweupe,na waliokuwa wanavamia vituo vya polisi nao waliogopa nn? Na waliokuwa wanachinja albino je?

Mbona kipindi cha Magu benki ziliibiwa?. Unaongea kana kwamba Magu alikuwa perfect. Umesahau yule Askari mlinzi wa benki aliyepita shaba na Sniper.
 
Back
Top Bottom