Kitu gani cha kawaida hujawahi kufanya?

Kitu gani cha kawaida hujawahi kufanya?

Wakuu,

Kuna vitu katika maisha ambavyo ni kawaida kufanywa na watu kila Siku,lakini inawezekana kwa wengine wakawa hawajawahi kufanya kabisa.

Sababu inaweza kuwa kutopenda,kukosa muda,sababu za kiimani nk.

Nikianza na mimi:

1. Sijawahi kabisa kutengeneza juisi ya matunda (Shalubati) katika maisha yangu, pamoja na kwamba huwa natumia ila ni ile iliyotengenezwa na wengine.

2. Sina kabisa akaunti kwenye mitandao maarufu hii mitatu ya Facebook, Instagram na Twitter, habari nyingi napata JF na vyanzo vingine.

Je, wewe ni kitu gani ambacho wengine huona ni cha kawaida kufanya ila kwa upande wako hujawai kufanya?

Kwenda cinema,Kumwabudu Boss,Kumpiga makofi mwanamke(Mke/Mpenzi),Kutongoza Mke wa mtu,na kubwa kuliko sijawahi kuonea wivu maisha ya watu walionizidi elimu,mali n.k

Sent from my VF-795 using JamiiForums mobile app
 
Actually ni sijui kuendesha baiskeli, ila zile spinning bike za Gym aah safii tu
 
Back
Top Bottom