Kitu gani cha kawaida hujawahi kufanya?

Kitu gani cha kawaida hujawahi kufanya?

Uwiii!! Hadi dada yako nimekushinda mana kimtaani mtaani nliwahi kupigana na mvulana kipindi hicho niko mdogo wee alinidunda nakumbuka kulikuwa na mtaro mdogo tu pembeni akanidumbukiza humo nikaanza kulia hadi dada zangu wakaja kunitowa mana sikupigana tena ikabakia nalia tu huku huyo mvulana ananisubiria kwa juu nitoke aniongeze.

Ila toka hapo sijawahi kupigana mana nikawa mwoga hadi kwa wanawake wenzangu kwa hofu nikipigana nao watanipiga. 😅😅
Ulimsamehe?
 
Kucha bandia ama chochote cha bandia mwilini kwangu, kubandika makope and the like

Kuvaa wigi, nilishawahi once sikurudia maana niliona kama nimebeba dunia kichwani

Kubeba ndoo kubwa ya maji, ni kitu cha kawaida kwa wanawake wengi ila me siwezi...naiona nzito

Kuepua sufuria jikoni bila mshikio ama cha kushikia
Wigi/ weaving/kubandika kucha/kope.....
In general "fake zones" sio muumini kabisa, sijui ushamba[emoji849]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom