Kitu gani cha thamani ambacho panya aliwahi kukuharibia mpaka sasa unawachukia hata kuwaona

Kitu gani cha thamani ambacho panya aliwahi kukuharibia mpaka sasa unawachukia hata kuwaona

Hawa wanyama wa ajabu sana waharibifu mpaka wanakeraa, wanaweza wakaingia kwenye begi wakaacha vitu visivyo vya maana wakatafuna vyeti vya shule au hela. kwakweli mimi nikiwaona hawakai kwa amani kabisa nitafanya kila jambo kuwasambaratisha.

Yaaani Familiar Bora hata usinginikumbusha machungu aisee yaani hao panya kudaadeq zao walikula hati ya nyumba ya urithi ukatokea mtafaruko mkubwa sana mimi na ndugu zangu kisa panya
 
Kulikuwa na harusi ya shemeji yangu, basi mchango ukatolewa na rangi ya sherehe tukapewa. Katika zunguka siku hiyo nikapata kagauni kazuri ka kuchukulia msaada USAID kabisa ka rangi ya harusi.

Nikakafua nyoosha vizuri nikaweka kabatini kusubiri siku ya tukio. Imefika siku nikajiandaa kabisa naenda chukua kiwalo mweeh panya wamekula kifuani pote na mgongoni. Sikuwahi kuona panya humo ndani hata kuwaza kama wapo. Walinikata hadi mood ya sherehe.
 
Hujawawekea chakula wafanyaje sasa.
Jitahidi kupanga vitu kidistancedistance ili usione uvivu wa kusafisha sehemu iliyorundikana au imejibana...panya hapendi usafi
Nikiwawekea chakula ujue wameishaaa
 
Nimepika bonge la nguna na ndondo ili nikitoka kwa mishe zangu ntakuwa nimechoka na isitoshe ntarudi Mida mibovu
Nimefika nimeoga Nile nilale dah
Panya washapiga sarakasi Sana kwenye sufuria la maharage na kwenye nguna wamedonoadonoa kishezi
 
Nimepika bonge la nguna na ndondo ili nikitoka kwa mishe zangu ntakuwa nimechoka na isitoshe ntarudi Mida mibovu
Nimefika nimeoga Nile nilale dah
Panya washapiga sarakasi Sana kwenye sufuria la maharage na kwenye nguna wamedonoadonoa kishezi
Story Yako inataka kufanana na yangu, Kuna siku piah nimejipikia zangu samaki mchuzi kama wote, Oyaa naenda dukani kununua unga wa sembe nusu, ile narudi namkuta panya kala mchomo kwenye mchuzi wa samaki anaangaika kutoka kwenye sufuria la mchuzi aliharibu bajeti yangu na nilimgeuza kitoweo.
 
Back
Top Bottom