Kitu gani cha ushujaa umewahi fanya katika maisha yako??

Kitu gani cha ushujaa umewahi fanya katika maisha yako??

Kama alichofanya yule Msenegali jana kule nchini Ufaransa na tofauti yake tu ni kwamba Yeye alimuokoa Mtoto kutoka katika ghorofa ili asianguke na Kufa ila Mimi nilimuokoa Mlevi wa ' Mataputapu ' aliyepanda katika Mti mrefu wa Mnazi na nikafanikiwa Kumuokoa japo tulipofika nae chini na Mimi nilijikuta tayari nimeshalewa kidogo.
Hhaha hongera
Ila ilibidi na wewe uwe promoted mkuu
 
Asalam Jf

Kama heading inavyojieleza hapo
Katika maisha yako yote tangu umezaliwa mpaka hapa ulipofikia
Je ni kitu gani cha ushujaa umewahi kukifanya??

Mimi nilizuia rungu kwa mkono wangu ambalo lingeweza kumuua yule aliyekusudiwa kupigwa.. i got hurt bt i never regret for what i did.
Kulala na maiti...!
 
Mkuu ulijisikiaje??
Maana me mara ya kwanza kuona maiti live mwili ulisisimka tena niliicheki kwa mbali aisee
Mkiwa pekeyenu wawili kibandani usiku porini halafu mwenzako akafa.. Utakimbia? Hata kama ni muoga utabaki naye
 
Mkiwa pekeyenu wawili kibandani usiku porini halafu mwenzako akafa.. Utakimbia? Hata kama ni muoga utabaki naye
Daah hapo kweli hamna namna
Ila inategemea na roho ya mtu mkuu
Mwingine anakimbia tu
 
Nilikataa kwenda kwa mganga wa jadi, hii ni baada ya kuugua mfululizo miaka 2 mzazi mmoja akashawishiwa nimelogwa ila kila nikicheki naona tatizo la hispital hili but hawanipeleki,
Tuligombana home ilikuwa likizo ya chuo kiufupi niliondoka nikaomba kibarua shule fulani cha week 2 nikafundisha nikalipwa elfu 30.

Tulivyofungua chuo niliondoka na elfu 30 bila mawasiliano na wazee nikiwa nishaamua sirudi home for life nitafanya vibarua kwa watu hata kuwafulia hadi nimalize chuo.
Baada ya miezi 2 mzazi mmoja alinitafuta nakujuta sana huku wakiwa na hofu labda nimezidiwa sana Ngoja niishie hapa.
 
nilitembea na mke wa mwanajeshi na alivyogundua aliapa angeniangamiza endapo angenishika lakini hata hivyo nilikimbia mji
 
Nilikataa dili HARAMU la milioni moja wakati nimelala njaa.
 
Ubarikiwe mkuu
Kama unachoongea kinaukweli mkuu
Sina sababu ya kuongea, Yeye aliyembinguni anajua. Sikupaswa kulisema hili ila nimefanya hivyo kuwahamasisha watu bali sio kwa cheap popularity kwakuwa aliyejuu atanilipa.
 
Back
Top Bottom