Kitu gani huwezi kusahau siku ambayo ulikua unafanya mtihani wa Darasa la Saba? Ndani na nje ya chumba cha mtihani

Kitu gani huwezi kusahau siku ambayo ulikua unafanya mtihani wa Darasa la Saba? Ndani na nje ya chumba cha mtihani

mens12

Member
Joined
Apr 8, 2022
Posts
69
Reaction score
143
Habari wana JF? By make a story short, let jump to the topic. Mimi kitu ambacho sintoweza sahau ni pale mshikaji (Hassan) alikuwa akichungulia majibu kwa jamaa (Boni) wa pembeni alipo mchania mkeka.

Ilikua hivi, mtihani wa hesabu. Boni alikua mzuri kwenye hesabu hivyo Hasani akawa anakopi majibu kwa Boni, kumbe Boni alikua na mpango wake.

Alikuwa akikokotoa majibu ya kweli anaya nakili kwa pembeni na penseli alafu kwenye jibu anaandika majibu ya uongo.

Jamaa akawa hajashtukia anakopy tu maana alifanya hivyo kwa mitihani mingine (mserereko), ilipofika kama bado dk 30 kuisha kwa muda akaomba booklet nyingine ya majibu nakuanza kujibu majibu ya kweli. Jamaa alichanganyikiwa aese!

Ilikua siku mbaya sana kwa mshikaji. I hope jamaa ni fund kwa sasa maana toka zamani alikua akitumiwa na shule kwa issues mbalimbali za ufundi kama mabomba nk
 
Mbele yangu alikua amekaa kipanga wa shule nzima, huyu mwamba siku ya mtihani wa Taifa hakubana hata paper moja, alikua akimaliza paper anajisogeza pembeni kidogo nipate nafasi ya kupiga chabo, aliniokoa sana, bila zile chabo sidhani kama ningefanikiwa kwenda sekondary
 
Hope ukikutana naye utamshukuru sana. 👍
 
Ni pale nilipangiwa kibonde nikae nae wakati tunapiga pepa la hesabu niliwah kumaliza kama dk 30 kabla ya muda wa kumaliza mtihan, ikanibidi nimpe booklet yangu ajaze [emoji23][emoji23][emoji23]

Hauwezi amini mwamba alijaza maswali mawili n akanirudishia akaniambia Asante [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] n jamaa elimu yake iliishia pale, hakuweza kutoboa kwenda sekondari
 
Aliingia bundi tukiwa kwenye mtihani wa mwisho ndio tulikuwa tumeanza mtihani muda mfupi tu. Ghafla tukanyanyuka wanafunzi wote tukaanza kukimbiza bundi.

Wasimamizi walizuia hawakuweza tulikimbiza bundi mpaka nje ya shule tukafanikiwa kumuua ndio tukarudi.

Wasimamizi wakagoma kutupa muda wa kumalizia mtihani wakaondoka.

Tulifaulu watu 2 tu kwenda Sekondari napo tulibebwa na masomo yaliyotangulia.
 
Halafu kuna jamaa mmoja alikua kama hajui jibu, anafunga macho alafu anadondosha kalamu itakapoangukia kama ni B au C ndio linakua jibu lake 🤣 🤣 🤣
 
Nakumbuka mwaka 2005, mtahiniwa ukiomba ruhusa ya kwenda washing room unasindikizwa na mlinzi na mkifika anakukabidhi kibomu chenye majibu ya maswali yote.
 
Habari wana JF? By make a story short, let jump to the topic. Mimi kitu ambacho sintoweza sahau ni pale mshikaji (Hassan) alikuwa akichungulia majibu kwa jamaa (Boni) wa pembeni alipo mchania mkeka.

Ilikua hivi, mtihani wa hesabu. Boni alikua mzuri kwenye hesabu hivyo Hasani akawa anakopi majibu kwa Boni, kumbe Boni alikua na mpango wake.

Alikuwa akikokotoa majibu ya kweli anaya nakili kwa pembeni na penseli alafu kwenye jibu anaandika majibu ya uongo.

Jamaa akawa hajashtukia anakopy tu maana alifanya hivyo kwa mitihani mingine (mserereko), ilipofika kama bado dk 30 kuisha kwa muda akaomba booklet nyingine ya majibu nakuanza kujibu majibu ya kweli. Jamaa alichanganyikiwa aese!

Ilikua siku mbaya sana kwa mshikaji. I hope jamaa ni fund kwa sasa maana toka zamani alikua akitumiwa na shule kwa issues mbalimbali za ufundi kama mabomba nk
Mimi nakumbuka tulipikiwa msosi mzuri na mtamu sana...(wali nyama na haragweee na soda moja moja wote.

Nilikula sana siku hiyo nilivyoshiba nikaona ngoja nijiegeshe chini ya mti na ubaya kuliwa na majani makubwa nikapitiwa na uzingizi nimeshtuka lisaa limeenda wenzagu wanaendelea na mitihani dah nililia sana wakanionea huruma nikaingia kufanya muda uliobaki..

ila nashukuru nilitoboa nikikumbuka nachekaga sana sana..wali haragwee liliniponza!😆😆😅
 
Mnanikumbusha mbali sana

Nilikaa na yule mtukutu nunda sana wa shule
Mwamba tangu darasa la kwanza na manunda wote walitokeaga tu kunikubali

Siku mbili kabla ya paper mchizi aliniita pembeni, akanipanga
Nikamuambia usiwaze, na nilikua na roho safi tu hata ile mitihani ya ndani atakae bahatika kukaa na mimi, kama masiah lazima aione pepo
Kwaio wahuni wakawa wanamtani kinoma mchizi coz walijua lazima aingie secondary

Siku ya pepa, mchizi akawa anasaidia kutoa majibu kwangu na kuwapa wengine
Alafu nilisahu kuwaambia kipindi hiko niko primary mimi nilikua jini kwenye masomo
Kama haaland anachotufanya pale EPL

Kila paper tukimaliza mchiz alikua anapewa sana heshima kwa kazi anayoipiga mule ndani ya chumba cha mtihani
Hadi paper ya mwisho, mambo yalienda fresh.
Then nikasafiri kutoka bush kuja kuosha macho jijini dar

Matokeo yaliyotoka
Watu ambao hawakuzaniwa wengi walitoboa
Mchizi nae alitoboa. Japo karibia wengi waliwaacha kata
Mimi nilitoboa ifunda, ila nilipelekwa private ()
Kila nikienda pale kijijin (now mji umekua sana)
Hadi leo classmates wangu wana respect sana na mimi[emoji120]

Mchizi alivyofika secondary aliamua kuwa serious na shule
Na yeye akajenga ufalme wake pale shule ya kata
Akatoboa form4, six pia akatoboa hadi chuo

Sasa hivi ni IT matata sana

Much respect mchiz P
 
Baada ya kujaza booklet yangu kwenye mtihani wa hesabu uliokuwa na maswali 50 ndipo nilipo mpa mwamba apige chabo,kasheshe ilipo fika ni pale zilipo baki dak 5 na msimamizi asha simama na mwamba ana booklet yangu.

Daaaaah
 
Back
Top Bottom