Kitu gani kilikushangaza ulipofika Dar kwa mara ya kwanza.

Vichwa vya kuku vimetoa macho vimebanikwa watu wanagombania

Mahindi ya kuchoma yanaliwa na ndimu na chumvi

Wanaume wanagombana na wadada kwenye foleni za chips

Nk nk nk.....dar ni maajabu mengi
Wa mkoa mmeanza ligi tena.
 
Nilinyoosha moja kwa moja kuiona bahari ya Hindi ambayo Nimeiona na kuisoma ktk ramani tangu nikiwa darasa la tatu.
 
Hongera mkuu wewe ulikuwa na lengo la kujifunza, kuna wengine walitaka kufika maisha club kwanza.
Nilinyoosha moja kwa moja kuiona bahari ya Hindi ambayo Nimeiona na kuisoma ktk ramani tangu nikiwa darasa la tatu.
 
First time kufika Dar stendi ilikuwa Kisutu enzi zile barabara ya kariakoo ilikuwa vumbi tupu mvua zikinyesha vumbi linageuka uji mwepesi. Tukatoka kisutu kuja kariakoo kwa mguu, eneo la msimbazi kilichonishangaza ni antena za televishen kwenye maghorofa zilikuwa nyingi kupitiliza, vimesimikwa vimlingoti kama 200 kwenye ghorofa moja. Baadae tukapanda chai maharage kwenda masaki.
 
Za zama hizi wewe ni miongoni mwa wapigania uhuru.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…